Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
sasa mwenye hoja si upunguze mihemko na makasiriko gentleman đLudicrious. Huna hoja sasa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa mwenye hoja si upunguze mihemko na makasiriko gentleman đLudicrious. Huna hoja sasa.
Tena mboga za asili kule ndio Zina Bei juu, wanaita organic food,Kwanini Wamarekani wanatumia mbolea kutoka kwenye Vinyesi vya Binadamu?
Kule kwao wamestuka na kurudia asili,Mbegu za asili zina ladha nzuri, ugali ni mzuri, matunda ni mazuri, mchele ni mtamu una harufu na ladha nzuri, mihogo na viazi ni mzuri. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mbengu za asili na za kisasa
Tupe Maarifa,Anayejua hili jengo ni la nini Kule Sweden na Nia yake,atamuelewa mleta mada.
View attachment 3232802
Janga kubwa.Hili suala ni janga la ARV jingine huko mbeleni. Imagine jamaa mmoja anakata supply ya mbegu, mbolea na viuatilifu ndani ya mwaka mmoja tu.
Cancer kuongezeka ni sababu ya vyakula hivyo visivyo organic,Wamarekani wanakufa na mavyakula ya GMO na huo ndio Ukweli Gentleman.
Unataka Watanzania nao wafe?
huna hoja .sasa mwenye hoja si upunguze mihemko na makasiriko gentleman đ
Ndicho nilichomaanisha,Badala ya kuweka ulinzi kwenye mbegu za asili kwanini usiseme serikali iwekekeze na sisi tutengeneze mbegu zetu ambazo ni za kisasa pia? Technology Kila siku inaenda mbele hairudi nyuma. Mbegu za kisasa ni Bora kuliko za kizamani. Zinaweza kuvumilia ukame na magonjwa. Ukitaka kutumia mbegu za zamani tumia lakini siku nchi yako ikipata upungufu ww chakula msianze kulaumu kina trump kwamba hawatumi misaada.
Usijali,Hebu rudisha hii kadamnasi kwenye mada. Uzi unaharibika kwa sababu ya Wapuuzi.
Moderate au uombe mods wafute tu
Njaa inayokuja mbeleni,Mkuu ajenda kama hizi zinajadiliwa kwenye nchi ambayo viongozi wake wapo makini, maslahi ya taifa yanawekwa mbele kuliko maslahi ya kiongoz.
Ajenda kama hizi kwa nchi yetu ni kama vile unawapigia kelele, Tena ukipeleka bungen asilimia kubwa ya wabunge watasinzia watahisi kama unawabembeleza walale
Hili pia linawagusa usalama wa taifa, kitengo ambacho kwasasa watu wanamashaka nacho.
Liko mji gani?Anayejua hili jengo ni la nini Kule Sweden na Nia yake,atamuelewa mleta mada.
View attachment 3232802
Huwezi kuingia JF ukatoka mtupu. Moyo unauma kuona wakulima wetu hawajui madhara ya mbegu hizi. Hiv ikitokea siku mbegu asili zote zimetoweka na hawa mabwana wakagoma kutoa mbegu itakuaje? Si tutawasujudia? Kinachokera zaidi mbegu za GMO hazina ladha nzuri. Tunakulaga tu. Acheni mzaha jamani!!! Michele wa asili mtamu. Miaka ya nyuma ukipikwa wali mtaa mzima hoi kwa harufu maridhawa.
Na Mungu aliagiza WANADAMU tule vyakula vitoavyo mbegu katika kitabu Cha Mwanzo chapter 1&2.Zamani za kale watu walikuwa wanaishi hadi kufikia miaka 900 sababu watu walikuwa wanakula vyakula vinavyotokana na mbegu asilia zilizoumbwa na Mungu.
Sasa hivi mtu kufikia miaka 80 amejitahidi sana. Binadamu wenye kiherehere kama Bilgate na genge lake la watu wenye roho mbaya wanapanga mipango yao ya kupunguza watu duniani ndo maana wanakuja na miradi yao ya mbegu wanazozitengeneza maabara.Mbegu hizi za maabara si rafiki kwa mwili wa binadamu. Zinamfanya binadamu kuandamwa na magonjwa kama kansa na magonjwa mengine.Siku hizi hata watoto wa kike wanabalehe kabla ya muda wao.
Tusipostuka na kuchukua hatua,miaka ya baadae binadamu atakuwa akifikisha miaka 10 tayari atakuwa amezeeka.
Well said mkuu, ila ni ngumu sana kwa watu kufahamu nini hasa kinaendelea katika huu ulimwengu itabidi itumike nguvu ya ziada kuelewesha watu angalau madhara yasije kuwa makubwa sana kwetu huko mbeleni. Kwa wenye ufahamu na udhalimu huu unaoendelea tujitahidi kusambaza elimu kwa wanaotuzunguka.
Haya ni madini,Ukiachilia mbali kunyangâanywa aridhi, kuachilia mbali madhara mbegu hizi zinazotuachia kwenye miili yetu baada ya kutumia nafaka zake, mbegu hizi pia zinaweza kuifanya ardhi kuwa ni tasa katika uzalishaji kwa miaka 10. Na ikiwa kwa miaka 10 aridhi yako haitaweza kutoa kitu, jiulize mkulima atapatia wapi fedha za kuweza kulipa mikopo yake, hapo ndipo jamaa wanapokuja na kuichukua ardhi yako.
Nchi za Ulaya bado kwa kiasi kikubwa zinaitegemea Afrika kwa malighafi, tunajua walizibeba kwa wingi sana wakati wa ukoloni na hata baada ya uhuru waliendelea kufanya hivyo kwa kupitia viongozi ambao wengi walikuwa ni vibaraka wao, ambao waliwapatia nchi hizi baada ya uhuru, na wale ambao waliwapinga na kukataa kuwa vibaraka waliuwawa kwa namna mbalimbali, sote tunajua hili, walio bakizwa madarakani ni wale waliokubali kwenda sambamba na sera zao, na wao wakazifikisha nchi zetu hapa zilipo.
Hivyo nchi nyingi za Ulaya na Marekani si kwamba tu zinatizama bara hili la Afrika kama sehemu ya kuchota rasilimali mbalimbali, lakini pia kama shamba ambalo watakuja kupanda mazao yao mbalimbali na kuyasafirisha kwenda katika nchi zao. Ndiyo maana Green Revolution inafanya kazi nzuri ya kuwapokonya wakulima wadogowadogo aridhi zao.
Katika vita hivi vya kutunyangâanya aridhi zetu, Gate Foundation, nyuma ya Bill Gate anayetoa mabilioni ya dola zake huku akitabasamu ili aonekane ni malaika na binaadam mzuri kushinda wote mwenye moyo wa pekee katika kuisaidia Afrika, huyu ndiye askari mwenye bunduki iliyo jaa risasi za mbegu za kisasa kwa ajili ya kutuangamiza ili aweze kuchakua aridhi zetu juu ya miili yetu iliyo lala kwenye aridhi yetu ikiwa imekauka kwa njaa kutokana na aridhi yetu kufanywa tasa na risasi za mbegu za kisasa kutoka kwenye bunduki ya Bill Gate na wenzake.
Asilimia 55 ya aridhi yote Afrika leo hii haifai kwa kilimo baada ya kulimwa kwa miaka mingi aina moja ya mazao kwa ajili ya watu wa Ulaya na Marekani. Aridhi hiyo imekuwa ni tasa na Mwafrika bado anavaa suruali yenye viraka matakoni, wakati Bill Gate na wenzake wanatembelea âPrivate Jetâ.
Wakati wa kuwa wabinafsi na aridhi zetu umefika. Sema hapana kwenye âUchukuaji Huruâ wao wanaita uwekezaji, mpaka sera zake zibadilishwe.
Kwa hiyo tunaishi miaka 80 kwa agizo la Mungu au gmo? Mnatuchanganya sasaNa Mungu aliagiza WANADAMU tule vyakula vitoavyo mbegu katika kitabu Cha Mwanzo chapter 1&2.
Kutuletea gmo ni Mpango wa yule Mwovu Ili kufupisha maisha Kwa magonjwa kama kansa.
Ndoto za mchanaUkiachilia mbali kunyangâanywa aridhi, kuachilia mbali madhara mbegu hizi zinazotuachia kwenye miili yetu baada ya kutumia nafaka zake, mbegu hizi pia zinaweza kuifanya ardhi kuwa ni tasa katika uzalishaji kwa miaka 10. Na ikiwa kwa miaka 10 aridhi yako haitaweza kutoa kitu, jiulize mkulima atapatia wapi fedha za kuweza kulipa mikopo yake, hapo ndipo jamaa wanapokuja na kuichukua ardhi yako.