Agenda ya kubadili Katiba si ya Rais Magufuli, ni agenda ya wapambe

Agenda ya kubadili Katiba si ya Rais Magufuli, ni agenda ya wapambe

Deogratias Mutungi

Senior Member
Joined
Oct 1, 2019
Posts
140
Reaction score
181
AGENDA YA KUBADILI KATIBA SI YA RAIS MAGUFULI, NI AGENDA YA WAPAMBE.

Nawasalim wana JF

Nimeamua kuandika andiko hili ili kutoa ufafanuzi wa maneno na taarifa zinazosambaa mitaani, mitandaoni na viunga mbalimbali vya taifa letu kuwa Rais Magufuli ana mpango wa kubadilisha “ Katiba ili aweze kutawala milele” Hoja hii ni ya uongo, upotoshaji na iliyojaa chuki na uzandiki wa hali ya juu sana, na ni hoja ya kipambe zaidi kuliko ukweli mwenyewe, aidha huu ni uvumi wa kisiasa usio kuwa na tija kwa taifa letu na unastahili kupuuzwa kwa nguvu zote.

Rais Magufuli kila mara amekuwa akikanusha taarifa hizi kwa kusema na hapa namunukuu “ Baada ya muda wangu kuisha sitaongeza hata dakika” Je taarifa hizi za kuongeza muda zinatoka wapi au ni agenda ya nani? Bila shaka ni agenda ya wapuuzi wanaotaka kumchonganisha Mkuu wa nchi na watu wake. Rais Magufuli ni kiongozi mwema mwenye haiba ya usikivu na “Kiongozi mwenye kuheshimu Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ Aidha ni mwenye busara anayetambua umuhimu wa kuilinda na kuiheshimu katiba ya nchi.

Wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati tuache kutoa taarifa za uongo zenye uchonganishi wa rais na watu wake, Hakuna taarifa rasmi au hotuba yoyote ambayo mkuu wa nchi aliwai kusikika akisema ana mpango wa kuongeza muda wa madaraka au kubadili katiba ya nchi hakuna kabisa, lakini kwa sababu ya ukosefu wa agenda kisiasa kumekuwepo na uvumi wa kiudaku udaku juu ya dhana hiyo isiyo na mashiko ya aina yoyote.

Aidha wote wanaozusha jambo hilo hawana ushahidi wa aina yoyote isipokuwa tu wanaongozwa na mihemko, chuki na propaganda za kishamba katika kuchonganisha mtu na mtu, tujenge hoja na kuendesha siasa safi tunapokuwa majukwaani na si kuzusha wala kukashifu rais na kumsemea mambo ambayo hajawai kuyasema.

Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli amefanya makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano bila shaka wana JF wanakubaliana na mimi kuwa uchumi wa vitu na watu uliofanywa na serikali ya JPM umenoga na pengine ndio sababu ya kuanza kuzusha mambo ambayo hayana tija katika ustawi wa maendeleo ya Mtanzania wa kawaida, Nashauri wana JF tupingane na wazushi wanaomzushia rais wetu kipenzi na tushikamane kutangaza mema ya John Pombe Magufuli.

Nawatakieni Jnne njema.

Deogratias Mutungi

0717-718619
 
Hao unaowaita wapambe wanatekeleza mkakati maalum uliopangwa na aliyewatuma na mwisho aliyewatuma atasema baada ya maombi mengi kutoka makundi mbalimbali naye amekubali
Mipango mikakati kwa kinyakyusa tunaita ' Strategy formulation'
 
Mtu mwenye nia ovu hawezi sema anafanya jambo fulani hadarani. Mengi yanafanywa kwa siri, ila kuna baadhi ya watu watatumika kuyasema kwa mifano au kutoa mawazo ili wale wahusika waone hilo jambo litapokelewa kivipi na wananchi. Hii ndiyo maanakuna baadhi ya wabunge walisema hata kama hataki watamlazimasha kisangoma
 
Sio watu wote ni wajinga!

Ujumbe ni kwamba mipango ya kuongeza haitofanikiwa kamwe. Watu hawamtaki hata hii mitano mingine hawataki.

Hata huko Sisiemu na Sirikalini wameshamchoka.
 
yaani hii ndiyo gia ya kutaka kuwatia upofu Watanzania wasing'amue njama zenu?
mwezi January 2019, Magufuli kwa kinywa chake mwenyewe alitoa kauli tata hii hapa chini - alikuwa ana maana gani?

1600153264413.png

nini kitakachomzuia 2025 (kama atapita 2020) kusema "aah, nimegundua sijamaliza kutatua changamoto nyingi - kwa hiyo nakubaliana na ombi la kuongeza vipindi vya urais"? ni nini kitamzuia?
 
MATAGA bana, yaani hii ndiyo gia ya kutaka kuwatia upofu Watanzania wasing'amue njama zenu?

mwezi January 2019, Magufuli kwa kinywa chake mwenyewe alitoa kauli tata hii hapa chini - alikuwa ana maana gani?

View attachment 1570276

nini kitakachomzuia 2025 (kama atapita 2020) kusema "aah, nimegundua sijamaliza kutatua changamoto nyingi - kwa hiyo nakubaliana na ombi la kuongeza vipindi vya urais"? ni nini kitamzuia?
Ni kauli ya kawaida sana, tatizo lipo kwenye mapokeo na tafsiri ya wenye "hofu ya kisiasa" Kauli ipo sawa kimantiki.
 
Sio watu wote ni wajinga!

Ujumbe ni kwamba mipango ya kuongeza haitofanikiwa kamwe. Watu hawamtaki hata hii mitano mingine hawataki.

Hata huko Sisiemu na Sirikalini wameshamchoka.
Sio kweli Mkuu, mbona rais anakubalika kuliko wakati wote, upo nchini au nje? kama upo nje nitakutumia mchanganuo wa takwimu za uchumi wa vitu na watu.
 
Mtu mwenye nia ovu hawezi sema anafanya jambo fulani hadarani. Mengi yanafanywa kwa siri, ila kuna baadhi ya watu watatumika kuyasema kwa mifano au kutoa mawazo ili wale wahusika waone hilo jambo litapokelewa kivipi na wananchi. Hii ndiyo maanakuna baadhi ya wabunge walisema hata kama hataki watamlazimasha kisangoma
Thanks, Wabunge ni Watanzania kama wewe hayo ni mawazo yao na sio kusudio la Mkuu wa nchi, usijali puuzia uvumi huo.
 
Mwenye hii mada,kwa heshima na taadhima nikuombe uithamini elimu walionayo watanzania pamoja na kwamba inatolewa BURE na serikali.
Nikisema hivyo nadhani utakuwa umenielewa.
Mh.Spika alisema ktk bunge lililokwisha kwamba hiyo hoja iletwe ktk bunge lijalo na ana uhakika woote watarudi na wataipitisha apende asipende....Waheshimiwa wakashangilia.
Hapo hakuna aliyesema Inshaallah au Mwenyezimungu akitujaalia uzima.........wao wanayo guarantee ya kuishi...Subuhannallah
 
Back
Top Bottom