Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
AGENDA YA KUBADILI KATIBA SI YA RAIS MAGUFULI, NI AGENDA YA WAPAMBE.
Nawasalim wana JF
Nimeamua kuandika andiko hili ili kutoa ufafanuzi wa maneno na taarifa zinazosambaa mitaani, mitandaoni na viunga mbalimbali vya taifa letu kuwa Rais Magufuli ana mpango wa kubadilisha “ Katiba ili aweze kutawala milele” Hoja hii ni ya uongo, upotoshaji na iliyojaa chuki na uzandiki wa hali ya juu sana, na ni hoja ya kipambe zaidi kuliko ukweli mwenyewe, aidha huu ni uvumi wa kisiasa usio kuwa na tija kwa taifa letu na unastahili kupuuzwa kwa nguvu zote.
Rais Magufuli kila mara amekuwa akikanusha taarifa hizi kwa kusema na hapa namunukuu “ Baada ya muda wangu kuisha sitaongeza hata dakika” Je taarifa hizi za kuongeza muda zinatoka wapi au ni agenda ya nani? Bila shaka ni agenda ya wapuuzi wanaotaka kumchonganisha Mkuu wa nchi na watu wake. Rais Magufuli ni kiongozi mwema mwenye haiba ya usikivu na “Kiongozi mwenye kuheshimu Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ Aidha ni mwenye busara anayetambua umuhimu wa kuilinda na kuiheshimu katiba ya nchi.
Wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati tuache kutoa taarifa za uongo zenye uchonganishi wa rais na watu wake, Hakuna taarifa rasmi au hotuba yoyote ambayo mkuu wa nchi aliwai kusikika akisema ana mpango wa kuongeza muda wa madaraka au kubadili katiba ya nchi hakuna kabisa, lakini kwa sababu ya ukosefu wa agenda kisiasa kumekuwepo na uvumi wa kiudaku udaku juu ya dhana hiyo isiyo na mashiko ya aina yoyote.
Aidha wote wanaozusha jambo hilo hawana ushahidi wa aina yoyote isipokuwa tu wanaongozwa na mihemko, chuki na propaganda za kishamba katika kuchonganisha mtu na mtu, tujenge hoja na kuendesha siasa safi tunapokuwa majukwaani na si kuzusha wala kukashifu rais na kumsemea mambo ambayo hajawai kuyasema.
Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli amefanya makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano bila shaka wana JF wanakubaliana na mimi kuwa uchumi wa vitu na watu uliofanywa na serikali ya JPM umenoga na pengine ndio sababu ya kuanza kuzusha mambo ambayo hayana tija katika ustawi wa maendeleo ya Mtanzania wa kawaida, Nashauri wana JF tupingane na wazushi wanaomzushia rais wetu kipenzi na tushikamane kutangaza mema ya John Pombe Magufuli.
Nawatakieni Jnne njema.
Deogratias Mutungi
0717-718619