Mangungo,
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza juhudi alizofanya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir katika kumuunga mkono Julius Nyerere kuijenga TANU kuwa "a nationalist-securalist party."
Na hii ni baada ya Hamza Mwapachu kumsisitizia Abdul Sykes kuwa uongozi wa TAA 1953 apewe Nyerere na 1954 waunde chama cha TANU na Nyerere aongoze harakati za kudai uhuru.
Mwapachu akasisitiza kuwa Nyerere ni Mkristo na kwa TANU kuongozwa na yeye kutasaidia kujenga umoja kwani haitaonekana kuwa harakati za siasa na kudai uhuru ni za Waislam.
Mazungumzo haya yaifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Ukerewe kati ya Mwapachu Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Hii ni moja ya "great moments," katika kitabu cha Abdul Sykes.
Yako mengi siwezi kueleza yote hapa.
Ndiyo maana kitabu hiki kinamshtua kila anaekisoma.
Waislam wamejitolea sana katika suala la kupiga vita udini.
Ndiyo nasisitiza mumsome Bergen na Sivalon mtambue nini kilifanywa baada ya uhuru kupatikana.
Historia uliyosoma wewe umemsoma Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Ali Mwinyi Tambwe na Sheikh Hassan bin Ameir?
Jiulize.
Kwa nini?
Ikiwa unawathamini wazalendo chembelecho "patriots" TANU ilijaa masheikh "patriots" wakiuza kadi za TANU ndani ya misikiti.
Huna sababu ya kuandika maneno ya kufikiria.
Jifunze historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Julius Nyerere.
Tusimame hapa kwa sasa.
Nahitimisha kwa kukupa tahadhari.
Maalim Faiza si wa kawaida.
She is above average intellect yake ni kubwa sana.
Kakaa vizuri darasani na ni bingwa wa lugha zote unazoandika wewe hapa na zaidi.
Tunafaidika sana hapa na elimu yake.
View attachment 2780832
Daily News halijui majina ya wazalendo hawa waliopigania uhuru wamepewa jina la mkururo, yaani jumla jamala mimi nawajua kwa kuwa ni babu zaungu: Kulia ni Mshume Kiyate, Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi.
Mshume Kiyate na Max Mbwana wamepewa mitaa kama kumbukumbu ya mchango wao katika ukombozi wa Tanganyika lakini miaka mingi imepita wahusika wamekataa kutekeleza.
Nini sababu?