Just...
Udogoni ukiingia chumbani kwangu utakuta vitu viwili huvikuti kwa mtoto yeyote wa Kariakoo.
Kwanza utakuta ukutani kuna ubao (blackboard).
Hii nikitumia kwa kusoma.
Nilikuwa nahifadhi ninayosoma kisha kuyaandika ubaoni.
Kitu kingine utakachokiona ni Hoffner Electric Guitar.
Nikipiga guitar.
Nikipenda kumuiga Hank Marvin.
Baadae nilipokwenda Uingereza nikajifunza keybaord na haikuwa kazi kubwa kuijua kwa kuwa tayari nilikuwa najua kupiga guitar.
Nimefurahi kusikia kuwa na wewe unapenda muziki.
Kitu kingine utakiona chumbani kwangu ni ''daluga'' yaani viatu vya mpira.
Nikipenda kuvaa Adidas.
Nilikuwa na ndoto iko siku nitavaa jezi ya Sunderland kisha timu ya taifa.
Niliishia kucheza Mnazi Mmoja na Kidongo Chekundu na kwengineko michangani sikugusa Karume Stadium.
Kiwango changu kilikuwa chini.
Mama kila siku akiulani mpira wangu na kuniombea dua niwe mwalimu kama baba yake Sheikh Muhammad Mvamila.
Bibi yangu Bi. Mwantum bint Mgeni akimwita mumewe, ''Hayati Bwana.''
Yeye dua yake nimechukua jina na nichukue yake yote.
Labda ndiyo maana leo niko hapa JF nasomesha.
Alhamdulilah.
Nyumba nyingi nilizofika nje hukuta watoto wa ndugu zangu wanasoma muziki shule basi hujikumbusha.