Agizo hili la Rais kwa vyombo vya Dola ni Amri, lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Agizo hili la Rais kwa vyombo vya Dola yaani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Majeshi, ni AMRI ya Kirais iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu.

Tunataraji angalau ndani ya saa 24 hadi siku 7, wote waliohusika kwa kupanga, kumteka na mauaji ya Mzee Ally Mohamed Kibao watakuwa wamekamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma, Hayati Rais Rais Magufuli alitoa AMRI ya kuhakikisha vyombo vya dola vinachunguza na kuchukua hatua kwa jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu siku ya 7/9/2017, Lakini hadi leo Magufuli amefariki hata jarada la uchunguzi tu halijawahi kufunguliwa na hakuna anayejua nani alihusika na jaribio lile baya kabisa.

Kwahiyo, Mh Rais taifa liko kwenye majaribu mazito, taifa linapimwa uvumilivu, Utawala wako unajaribiwa, Njia pekee muhimu, tunataka uwajibikaji kwa tukio hili na matukio mengine yote ya utekaji ya akina Soka, Mlay, Dioniz nk, Jambo jema umetoa amri hiyo wewe mwenyewe unataka vyombo vya dola vikuletee taarifa za matukio haya, Tunaamini hili na mengine hayatafunikwa!

Soma Pia:
Na katika hatua za mwanzo, Ninashauri uwajibikaji kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi huru na Haki.

Na Yericko Nyerere

IMG_3929.jpeg

IMG_3930.jpeg
 
Inasemekana Woodrow Wilson hakuwa raisi kuelekea ukingoni mwa muhula wake. MKe wake Bibie Edith Wilson ndiye alikuwa akisaini kila kitu akifoji sahihi ya mumewe. Bwana Woodrow Wilson alikuwa mgonjwa. Na mambo nchini yakawa yanaenda. Bibie Edith alipewa maelekezo machache na permanent 'Washington' mambo yakasonga mbele.

Naamini ile hulka ya kuwa tunachagua viongozi kwenda kuisimamia serikali imepitwa na wakati. Liserikali limeshakuwa likubwa na inaweza kujiongoza yenyewe. lina autonomous entities ambazo hazisikilizi mtu wala kitu

Civilian authority over the government has gone. Kauli ya wawakilishi wetu haina nguvu tena. Kila kiongozi anayechaguliwa anaweza akawa ana nia njema mwanzoni lakini akamezwa na mfumo baadae.
 
Inasemekana Woodrow Wilson hakuwa raisi kuelekea ukingoni mwa muhula wake. MKe wake Bibie Edith Wilson ndiye alikuwa akisaini kila kitu akifoji sahihi ya mumewe. Bwana Woodrow Wilson alikuwa mgonjwa. Na mambo nchini yakawa yanaenda. Bibie Edith alipewa maelekezo machache na permanent 'Washington' mambo yakasonga mbele.

Naamini ile hulka ya kuwa tunachagua viongozi kwenda kuisimamia serikali imepitwa na wakati. Liserikali limeshakuwa likubwa na inaweza kujiongoza yenyewe. lina autonomous entities ambazo hazikilizi mtu wala kitu

Civilian authority over the government has gone. Kauli ya wawakilishi wetu haina nguvu tena. Kila kiongozi anayechaguliwa anaweza akawa ana nia njema mwanzoni lakini akamezwa na mfumo baadae.
Civilian authority over the government has gone! This is exactly the reality! Civilian authority was vanished since day one of the nation's birth!
 
Matukio yote yametokea mwezi wa Tisa siku zile ni zile tu zinakaribiana baada ya miaka 7🤔
 
Ngoja tuone kama yule aliyewavunjavunja wakina Sungu na Mnyika kule Mbeya kama atashughulikiwa!
 
Agizo hili la Rais kwa vyombo vya Dola yaani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Majeshi, ni AMRI ya Kirais iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu.

Tunataraji angalau ndani ya saa 24 hadi siku 7, wote waliohusika kwa kupanga, kumteka na mauaji ya Mzee Ally Mohamed Kibao watakuwa wamekamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma, Hayati Rais Rais Magufuli alitoa AMRI ya kuhakikisha vyombo vya dola vinachunguza na kuchukua hatua kwa jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu siku ya 7/9/2017, Lakini hadi leo Magufuli amefariki hata jarada la uchunguzi tu halijawahi kufunguliwa na hakuna anayejua nani alihusika na jaribio lile baya kabisa.

Kwahiyo, Mh Rais taifa liko kwenye majaribu mazito, taifa linapimwa uvumilivu, Utawala wako unajaribiwa, Njia pekee muhimu, tunataka uwajibikaji kwa tukio hili na matukio mengine yote ya utekaji ya akina Soka, Mlay, Dioniz nk, Jambo jema umetoa amri hiyo wewe mwenyewe unataka vyombo vya dola vikuletee taarifa za matukio haya, Tunaamini hili na mengine hayatafunikwa!

Na katika hatua za mwanzo, Ninashauri uwajibikaji kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi huru na Haki.

Na Yericko Nyerere

View attachment 3091627
View attachment 3091628
Hao anaowapa amri ya kumpatia taarifa ndio hao hao wanaoshukiwa kutenda uovu huo. Sasa ni taarifa gani watakayotoa kwa huyo mtoa amri?

Watu wa CHADEMA wachukue nasaha kutoka kwa Mzee Oliver Tambo aliyesema kwamba:-
"We were forced to install the Paramilitary Wing of uMkhonto we Sizwe (MK) within ANC because the Government of White Minorities in South Africa was terrorising us ANC by using the State Security Forces."

Oliver Reginald Tambo, the former President of African National Congress (ANC) from 1967 to 1993.
 
Lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma, Hayati Rais Rais Magufuli alitoa AMRI ya kuhakikisha vyombo vya dola vinachunguza na kuchukua hatua kwa jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu siku ya 7/9/2017, Lakini hadi leo Magufuli amefariki hata jarada la uchunguzi tu halijawahi kufunguliwa na hakuna anayejua nani alihusika na jaribio lile baya kabisa.
Ni wimbo uleule tofauti ni waimbaji
 
Agizo hili la Rais kwa vyombo vya Dola yaani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Majeshi, ni AMRI ya Kirais iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu.

Tunataraji angalau ndani ya saa 24 hadi siku 7, wote waliohusika kwa kupanga, kumteka na mauaji ya Mzee Ally Mohamed Kibao watakuwa wamekamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma, Hayati Rais Rais Magufuli alitoa AMRI ya kuhakikisha vyombo vya dola vinachunguza na kuchukua hatua kwa jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu siku ya 7/9/2017, Lakini hadi leo Magufuli amefariki hata jarada la uchunguzi tu halijawahi kufunguliwa na hakuna anayejua nani alihusika na jaribio lile baya kabisa.

Kwahiyo, Mh Rais taifa liko kwenye majaribu mazito, taifa linapimwa uvumilivu, Utawala wako unajaribiwa, Njia pekee muhimu, tunataka uwajibikaji kwa tukio hili na matukio mengine yote ya utekaji ya akina Soka, Mlay, Dioniz nk, Jambo jema umetoa amri hiyo wewe mwenyewe unataka vyombo vya dola vikuletee taarifa za matukio haya, Tunaamini hili na mengine hayatafunikwa!

Na katika hatua za mwanzo, Ninashauri uwajibikaji kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi ili kupisha uchunguzi huru na Haki.

Na Yericko Nyerere

View attachment 3091627
View attachment 3091628
Hakuna lolote litafanyika maana hayo mauji ni maagizo ya rais kupitia ile sheria mpya ya usalama wa taifa. Usitegemee ripoti yoyoye ya maana kuandaliwa na polisi, maana wao polisi kazi yao ni kufuata maagizo ya viongozi.
 
Kibao sio wa kwanza, na wala hatokuwa wa mwisho kuuliwa.

R.I.E.P kamanda.
 
Vyombo vya dola vinamheshimu Amiri Jeshi Mkuu kweli!vinginevyo kwa matukio haya nina wasiwasi, yeye mwenyewe yuko mashakani, maana hata ndani ya chama kunafuka moshi.Abadilike 4 R kwa heri ya kuonana. Uchaguzi safari ni mbaya zaidi ya 2019/20. Mtajionea wenyewe. Hizi ni dalili mbaya.
 
Back
Top Bottom