Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Agizo hili la Rais kwa vyombo vya Dola yaani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa na Mkuu wa Majeshi, ni AMRI ya Kirais iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu.
Tunataraji angalau ndani ya saa 24 hadi siku 7, wote waliohusika kwa kupanga, kumteka na mauaji ya Mzee Ally Mohamed Kibao watakuwa wamekamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.
Lakini binafsi natoa angalizo kwa kurejea uzoefu wa nyuma, Hayati Rais Rais Magufuli alitoa AMRI ya kuhakikisha vyombo vya dola vinachunguza na kuchukua hatua kwa jaribio la mauaji ya Mh Tundu Lissu siku ya 7/9/2017, Lakini hadi leo Magufuli amefariki hata jarada la uchunguzi tu halijawahi kufunguliwa na hakuna anayejua nani alihusika na jaribio lile baya kabisa.
Kwahiyo, Mh Rais taifa liko kwenye majaribu mazito, taifa linapimwa uvumilivu, Utawala wako unajaribiwa, Njia pekee muhimu, tunataka uwajibikaji kwa tukio hili na matukio mengine yote ya utekaji ya akina Soka, Mlay, Dioniz nk, Jambo jema umetoa amri hiyo wewe mwenyewe unataka vyombo vya dola vikuletee taarifa za matukio haya, Tunaamini hili na mengine hayatafunikwa!
Soma Pia:
Na Yericko Nyerere

- Rais Samia aagiza Vyombo vya Uchunguzi kumpa taarifa ya kina ya Kifo cha Ali Mohamed Kibao
- Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
Na Yericko Nyerere