Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Serikali ya Tanzania hii leo imetoa mwongozo mpya kuhusu ugonjwa wa corona ambapo wasafiri watakaokuwa wanatoka katika nchi zenye maambukizo ya virusi vipya vya corona watatakiwa kukaa karantini kwa siku 14.
Mwongozo huo uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Profesa Abel Makubi utaanza kufanyiwa kazi rasmi kesho Mei 4 2021, unaeleza kuwa karantini hiyo itawahusu wasafiri ambao ni wakaazi na wageni.
Kabla ya kwenda karantini kwanza watafanyiwa vipimo vya lazima vya corona.
Kwa wageni watatakiwa kukaa karantini kwa gharama zao "watachagua eneo moja katika orodha itakayotolewa na serikali."
Wasafiri ambao ni wakaazi wa Tanzania wataruhiswa kujitenga kwa siku 14 katika nyumba zao wenyewe.
Hatua hizo zitawahusu pia wasafiri ambao safari zao zilipitia katika nchi hizo walau katika siku 14 zilizopita.
Mwezi mei mwaka jana Tanzania iliondoa karantini ya lazima kwa wasafiri kutaka nje ya nchi hiyo na badala yake wakatangaza kuwa kutafanyika vipimo vya ugonjwa huo.
Wizara ya Afya ya Tanzania imeeleza kuwa nchi hizo zenye virusi vipya vya corona zitatambuliwa kupitia taarifa zinazotolewa kila siku na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kwa sasa virusi vipya vinavyogonga vichwa vya habari zaidi ni vya India na Brazili.
Nchini India hali ni mbaya zaidi ambapo zaidi ya watu 300,000 kila siku hukutwa na maambukizi ya corona.
Wataalamu wanatahadharisha kuwa idadi ya maambukizi inaweza ikawa kubwa zaidi ya hiyo.