Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Wawaachie tuu waingie na virusi vyao tuvizoee na vyenyewe.
 
We are in the right track
1620068271989.png
 
Serikali ya Tanzania hii leo imetoa mwongozo mpya kuhusu ugonjwa wa corona ambapo wasafiri watakaokuwa wanatoka katika nchi zenye maambukizo ya virusi vipya vya corona watatakiwa kukaa karantini kwa siku 14.
Mwongozo huo uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Profesa Abel Makubi utaanza kufanyiwa kazi rasmi kesho Mei 4 2021, unaeleza kuwa karantini hiyo itawahusu wasafiri ambao ni wakaazi na wageni.
Kabla ya kwenda karantini kwanza watafanyiwa vipimo vya lazima vya corona.
Kwa wageni watatakiwa kukaa karantini kwa gharama zao "watachagua eneo moja katika orodha itakayotolewa na serikali.

Wasafiri ambao ni wakaazi wa Tanzania wataruhiswa kujitenga kwa siku 14 katika nyumba zao wenyewe.
Hatua hizo zitawahusu pia wasafiri ambao safari zao zilipitia katika nchi hizo walau katika siku 14 zilizopita.

Mwezi mei mwaka jana Tanzania iliondoa karantini ya lazima kwa wasafiri kutaka nje ya nchi hiyo na badala yake wakatangaza kuwa kutafanyika vipimo vya ugonjwa huo.
Wizara ya Afya ya Tanzania imeeleza kuwa nchi hizo zenye virusi vipya vya corona zitatambuliwa kupitia taarifa zinazotolewa kila siku na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kwa sasa virusi vipya vinavyogonga vichwa vya habari zaidi ni vya India na Brazili.
Nchini India hali ni mbaya zaidi ambapo zaidi ya watu 300,000 kila siku hukutwa na maambukizi ya corona.
Wataalamu wanatahadharisha kuwa idadi ya maambukizi inaweza ikawa kubwa zaidi ya hiyo.
Source: BBC Swahili
Huu ni ushauri au maagizo!? ile tume aliyounda Mama kumshauri ndiyo imetoa maagizo hayo!? Lakini kazi ya hiyo tume si kumshauri Mama au kutupa maelekezo!?
 
Jamani tukianza kufungiwa ndani mkae kiimyaaa maana mamb ndy yanaanza ivo
 
Leo wamekurupuka na kusema watu wanaotoka nchi zenye virus wakali wakae karantiini siku 14. Hili sidhani kama linatosha kwa wasafiri kutoka India. Wangesitisha safari kwanza. Virus wakienea Tanzania inaweza kuleta maafa.
Bado wanashangilia ujio WA Nyalandu Covid baadae.
 
Tanzania kwa wananchi waliopo ndani watangazieni watumie barakoa hali sio shwari na iwe lazima hiyo rapid test kazungura iliwachanganya mtu huyo huyo mmoja asubuhi akipima ana corona jioni hana tena ile wave two wakati imekomaa wakaacha kupima wakawa wanabaki kusoma majibu ya kipimo cha UTH Lusaka..inatakiwa kusitisha safari za ndege kutoka na kuingia India au Brazil kama zipo...
Matumizi ya sanitizer au kunawa na kupunguza misongamano isiyo ya lazima..
Kila ofisi au duka iwekwe sanitizer au maji ya kunawa na sabuni..
Kupunguza misongamano kwenye vyombo vya usafiri wa ndani..
Kupunguza misongamano huko polisi..
Watu waache kusalimiana kwa kushikana mikono...
Mechi ya Simba vs Yanga washabiki waruhusiwe wachache tuu..
Kuhamasisha matumizi ya barakoa kuwa ya lazima..
Wazee wa Corona naona mnakuja kwa kasi sana sasa! Pls tusitishane! Maisha ni ya Mungu!!
 
Wazee wa Corona naona mnakuja kwa kasi sana sasa! Pls tusitishane! Maisha ni ya Mungu!!
Hakuna Wazee wa corona,Corona ipo tunatoa angalizo sio kutishana mpaka kesho Cape Town usipovaa barakoa unakula bakora na polisi vitu vya kufata havina gharama kuliko corona yenyewe...
 
Back
Top Bottom