Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Agizo: Wasafiri watakaoingia nchini watakaa karantini siku 14 kwa gharama zao

Kuna kitu nyuma ya Pazia kimeanza kutokota

Ili kikiwaka vizuri waseme hatua zilichukuliwa

Lakini mambo bado hayajaharibika sana

Kwa jinsi India kilivyoumana na Hawa wenzetu lazima Itakuwa kuna ndugu zao huko wanasepa kuja Bongo kujificha

India wana hali tete sana sana

All in all, Sijajua kwanini hawa virusi wanawavamia sana ngozi nyeupe

Au wanakula sana Burger, Pizza na vile vitu laini laini kama biscuits na choklate
Kwani wahindi ni ngozi nyeupe?

Embu jaribu kuangalia picha ama video zao za majanga ya Covid ili kuthibitisha kauli yako ama kujibu swali langu.
 
Ni jambo jema lakini wakumbuke nchi za Dunia ya Kwanza Raia wao wamepata chanjo kwa hivi swala la kuwalazimisha hizo siku 14 ni zoezi lisilowahusu zaidi iwe ni kwa wenyeji kuliko wageni.
Wenyeji ndio hawana chanjo hao ndio walipaswa kupewa hizo siku 14
Nchi za wenye kujitambua wapo mbali huku kwetu ndio kumekucha...
 
Hiyo haiingii akilini hata kidogo.

--Wenye chanjo hawaruhusiwi kuwekwa karanteen.

-- wageni kukaa karanteen siku 14 na wenyeji kukaa karanteen kwenye nyumba zao.

Kweli serikali mpo serious?

Fungeni mipaka ya inchi,,,,Eboo!!
 
Si wawawekee mashine ya nyungu wakifika wajifushe kwa ile garama waliyoiweka kisha wawaachie
 
Uko sawa kabisa Mkuu Watanzania na wageni wote ni kupiga marufuku kuingia nchini au iwe ni mandatory kuwekwa karantini kwa gharama zao kwa siku 14, vinginevyo hizi hatua ni sawa na kutwanga maji. Ukweli ni lazima uanikwe hadharani bila kupindisha maneno.
Ni hatua nzuri lakini haitoshi kwa wasafiri wale watokao nchi zilizopigika kwelikweli mfano India.
Nchi za hivyo kuna haja ya kuzuia wasafiri watokao huko kuingia nchini!
 
Mwingine aliyefanya PROMO huyu hapa na ugonjwa haukufanya ajizi.
Huu UGONJWA wa promo.

kadri unavyoupa air time ndivyo unavyozidi kukua..dawa NI kuupotezea na kumuomba MUNGU
 
Wakitufungia tu,tunamuamusha Magufuli kokote aliko aje arekebishe,alafu arudi zake akapumzike salama!!
Lile liuaji hata uliamsheje haliwezi kuamka. Mungu kaliweka sehemu isiyojulikana.

Mungu wetu ni mwema sana, ametutendea mambo makuu... Sisi ni nani hata tusimshukuru?
 
bila Shaka.
ILA kaa ukijua . MISIMAMO MIKALI YA MAGUFULI JUU YA CORONA.
Ndo imetufanya tuwe salama dhidi ya Corona.
usidhani hyo barakoa na chanjo na sanitizer vinaweza kukulinda na Corona.
basi wangepona ulaya na marekani na Asia.
NI MUNGU TU.
kwa akili Kama zako,Kama taifa tuna safari ndefu aiseee daaaaa
Usikute na wewe unaitwa mume,baba,mjomba mkubwa
Daaaaa kazi ipo wazeee![emoji849][emoji849][emoji849]
 
Kufa ni ahadi na wenye akili timamu hujilinda ili kuepuka maambukizi ya aina yoyote ili kwa kuvaa ndom, kuchemsha maji, kuweka vyandarua etc. Huo ni ufinyu mkubwa wa akili kuona ugonjwa uliowaua binadamu zaidi ya milioni 3 in less than 18 months na hivyo kuua watu wengi duniani kuliko ugonjwa wowote ule kwa zaidi ya miaka Mia unafanyiwa promo.
Kufa NI AHADI.ila hip UGONJWA bila promo hauendi.
 
Back
Top Bottom