TANZIA Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar

TANZIA Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar

vijana wa leo mjiulize na mjifunze,Agnes amefariki je ameacha Legacy gan au jambo gan la mfano na kukumbukwa zaid ya watu ku refer makalio yake makubwa
Mkuu wewe una legacy gani ?.., duniani ishi kwa faida yako na furaha yako sio utakumbukwa vipi ukifa.., yeye anakumbukwa na wasiomjua kuna watu wakifa hata ndugu zao hawawakumbuki..., kuna watu kama Tesla they did a lot for humanity but died alone with nothing and unhappiness..., the point being live for yourself and do things your heart desires.., do them for their impacts not for the sake of being remembered..,
 
Wadau nilipita Mama Ngoma Health Centre Mwenge na kukuta watu wakilia kuuliza naambiwa Video Queen Masogange amefariki muda mfupi uliopita.


=========
UPDATES:
=========

Video queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyoko Mwenge, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alikuwa anasumbuliwa na Homa ya matumbo pamoja na tatizo la kupungukiwa na damu.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Habari zaidi....

Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia jioni ya leo April 20 alipokuwa amelazwa katika hospital ya Mama Ngoma akipatiwa matibabu

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.
Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.

Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.

Je ugonjwa wa pnemuonia (Nimonia) ni nini?

Pneumonia ni maambukizi katika viriba ya hewa katika pafu moja au mapafu yote. Viriba hivi vya hewa huweza kujaa maji au usaha na kusababisha mgonjwa kukohoa, homa kali na kupumua kwa shida. Pneumonia hubebwa na bakteria, virusi au fangasi.

Habari zaidi, soma=>Ufahamu undani wa ugonjwa wa pneumonia (Nimonia)
"
Je ugonjwa wa pnemuonia (Nimonia) ni nini?

Pneumonia ni maambukizi katika viriba ya hewa katika pafu moja au mapafu yote. Viriba hivi vya hewa huweza kujaa maji au usaha na kusababisha mgonjwa kukohoa, homa kali na kupumua kwa shida. Pneumonia hubebwa na bakteria, virusi au fangasi."

Nimesoma hii paragraph nikakumbuka ingekuwa ni miaka ile ya Decembwr 2019 kuelekea March 2020 wangesema ni yenyewe ilimtoa duniani"

Nilikuwa naipitia hii Paragraph hapa nikiwaza Nimonia ya sasa watu wanaifananisha na Covid_19.
 
Nimesoma hii paragraph nikakumbuka ingekuwa ni miaka ile ya Decembwr 2019 kuelekea March 2020 wangesema ni yenyewe ilimtoa duniani"

Nilikuwa naipitia hii Paragraph hapa nikiwaza Nimonia ya sasa watu wanaifananisha na Covid_19.
Ni kweli

Hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo nguvu kubwa inapaswa kuwa katika ELIMU ,ELIMU , ELIMU kwa jaamii nzima kuhusu maswala mbali mbali ya kiafya izidi kutolewa kwa kina.
 
Back
Top Bottom