Hakuna anayemhukumu mtu ila kasome biblia yako vizuri kama ni mkristo,kama biblia imesema "waliomkataa Yesu wamekwisha kuhukumia" sasa mimi nikisema kama hujampokea Yesu umekwisha kuhukumiwa kwani mimi nakuhukumu?Neno limeshakuhukumu muda mrefu mimi natumia neno(nakukumbusha tu) sasa liondoe kwanza neno kisha uje kwa anayelitumia neno.
Hakuna sala za marehemu,kila mtu Mungu atamuweka alikochagua wakati yuko hai(tusidanganyane),otherwise hakuna Jehanamu kwa sababu kila anayekufa wanasema "alazwe mahali pema peponi" ina maana Kuzimu hakuna watu?Wote wamelazwa pema peponi,mimi nikifa msiseme hivyo kwani sitaki kulala muda wote kuna muda nitahitaji kutembea tembea.
Hayo ndiyo Yesu aliita mapokeao ya wanadamu,watu hawafuati Mungu anasema nini wanafuata mapokea ya wanadamu,wanadamu hawana mbingu ya kukupeleka ukifa,Mungu pekee anayo mbingu kama utaishi katika njia zake.
Wewe ambaye uko hai je umechagua Mungu akuweke wapi siku ukifa?Moyoni mwako unashuhudiwa wewe ni wa wapi.Neema ipo leo kama utampokea Yesu hata ukifa lipo tumaini.Saa ya wokovu ni sasa ,endelea kucheza tu zamu yako inakujua hapo nafsi na roho zikiuacha mwili utakumbuka haya tunayoyasema.
Naunga mkono kuombeana mema kwa mtu akiwa hai tu,akishakufa hizo ni mbwembwe za wanaobaki.Mungu anamhukumu mtu baada tu ya kufa,kama unampenda mtu mwombee akiwa hai.Ni bora utoe pesa kumhudumia mgonjwa kuliko usimsaidie mgonjwa akiwa hai,kisha kifa unanunua jeneza la gharama na kuchukua video.You are wasting your resources.Tubadilikeni si muda wa kuchanganya wema na uovu.