Watanzania tuna silka yetu ama ukipenda tabia yetu iliyozoeleka ya kutokupigana hasa tunapokuwa kwenye mtanziko ama mkwamo wa Jambo lolote lile.
Huu siyo uzumbukuku, uzoba ama uzwazwa kama wengi wasemavyo bali ni karama toka kwa mola waliopewa watu wa taifa hili. Nchi hii ni Kisiwa cha baraka na jicho la mwenyezi Mungu.
Ndiyo maana hata uhuru wa taifa letu ulipatikana kwa maneno tu.
Pia tumeepushwa na mkono wa chuma wa awamu ya tano kwa sala tu.
Hivi sasa tupo kwenye mateso ya tozo, lkn tusimwache Mungu wetu. Tumlilie tena Mungu wetu atufanyie njia pasipo njia. Kila mtu kwa Imani yake na mahala pake pa kazi ama makazi amuombe Mungu atuepushe na mzigo huu wa tozo. (YUPO MUNGU MBINGUNI ASIKIAYE KILIO CHETU).
NB: Tozo ni wizi wa kimabavu. Kilicho halali kwa serikali ni kodi. Kila mtu anapaswa kulipa kodi lkn siiyo tozo.