Ahadi ya billioni moja kwa wachezaji Yanga yawatisha Al Hilal, ya Vipers yawapa wazimu

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Ingawa ilifanywa siri kutokana na hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo wanuka jasho wa Tanzania, fununu mchomoko ni kwamba yule tajiri wa kiukweliukweli asiye na ubahili hata kidogo, yaani yeye kumwaga mapesa hafikirii mara mbili wala hachungulii daftari, KATENGA BILLION MOJA Al Hilal apasuke kwao.

Piga mwenyewe mahesabu kila mchezaji na wa benchi la ufundi wataondoka na ngapi, siyo chini ya milioni 25-30. Wapo watakaobisha ila ndiyo muelewe kwamba Yanga kwa sasa wanaogelea pesa, yaani hata mchezaji akimtembelea ofisini akikohoa shida tu jamaa anazama kwenye droo anatoka na kibuunda.

Ahadi hii ni siri sababu wachezaji wametaka iwe hivyo wasije wakasumbuliwa na ndugu na jamaa na marafiki, ila taarifa za kintelejensia za njaa kali hatari imezinasa.

Kingine kinachoendelea hapo Khartoum ni ubaridi uliowapata mashabiki, wachezaji na viongozi wa Al Hilal hapo jana baada ya Vipers kuwatoa Mazembe, wakajiuliza sasa kama Vipers waliwafunga Yanga 2-0 wakiwa na Bobosi wamewatoa Mazembe ambao tulifungwa 3-0 na wadogo zao Don Bosco, je, sisi itakuwaje? Ina maana Yanga ni kubwa na imara sana?

Hadi sasa kwa hayo yanayoendelea, Yanga anaenda kushinda 4-1, Mayele anapiga hat trick!
 
Hatua wanayogombania kufika watapata kiasi gani?

Hata kama watapata hela hiyo, je inaweza kurudisha faida kwa timu, hasa ukizingatia pesa ya usajili iliyotumika msimu huu?

Billion moja si mchezo,je kwa klabu yangu ya Yanga inaweza kutoa pesa zote hizo kama motisha?
 
ushaambiwa imetoka kwa tajiri asiye chuplichupli , hachungulii pesa yeye anazimwaga tu
 
Utoe 1B kwa wachezaji endapo wataweza kuvuka

Wakati huo makundi unapewa hiyo hiyo 1B

Mbona hesabu kama zinagoma?

Anyway hiyo 1B naiona kama picha ya samaki tu
Unamjua Gharib unamsikia weeee, hajali kuhusu pesa ndogondogo kama MO, jamaa siyo bahili , kajitolea tu ili kuwapa furaha wanayanga
 
kawai sana,wenzie kina Mo huwa wanaanzia kugawa izo bonus quatal final huko.huku hatua za awali kama unatimu makini ni pakutoboa kwa speed ya risasi.
 
Kwani gharama unazotumia kutafuta ubingwa zinalingana na zawadi unayopata ukiwa bingwa?
 
WALIKUWA WAPI WANGEHAIDI KWA MKAPA NA KUHONGA YULE REFA MSAIDIZI TUSINGEEBDA NA PRESSURE

MNANIKUMBUSHA SIMBA WALIHAIDIWS ENZI HIZO NA A.DEWJI GARI KILA MCHEZA KILA MCHEZAJI..MABEKI WALICHOFANYA N SIRI YAO NA BOLIZOZO

.USIAMINI SANA HIZI PESA KUBWA WAKATI MWININGNE TUNALISHWA...
 
Inabidi Bolizozo ajengewe mnara pale Msimbazi. Sijui kama katika historia yake kama itapotea kwenye kumbukumbu za Simba.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]saa tatu sio mbali
 
Again again Pdidy nguli wa uandishi jf
 
Shule ulisomea ujinga 🤣🤣🤣
 
Alietoa hiyo billion 1 kashajua kabisa Yanga hata akipewa trillion 3 bado kichapo hawawezi kukikwepa ndo maana Hana mashaka na hela yake iko salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…