Ahadi ya kujenga nyumba yangu ya kuishi kabla ya miaka 35 imetimia

Ahadi ya kujenga nyumba yangu ya kuishi kabla ya miaka 35 imetimia

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Niliweka nadhiri kwamba kabla ya kufikisha miaka 35 hapa duniani lazima niwe nimejenga nyumba yangu na nimehamia kwangu, ndoto hii imetimia tarehe 23/2 nimehamia kwangu na kila nikiamka asubuhi nazunguka na taulo kiunoni nyumba nzima huku nikipiga mswaki na kufokafoka.

Wale mnaosema kujenga ni kuzika pesa endeleeni kubanana na wahindi kwenye kota za chumba na sebule na joto hili kali la Dar ni shida tu.

Kwa heri upangaji na sasa karibu mashambulizi ya kwenye biashara.
 
Ulichelewa mno Kuna dogo langu alihamia kwake akiwa na 19yrs old na aliishia la tano Ila ana hela chafu. Hapo unasemaje
Mkuu mkianza kushindana au kulinganisha vitu, basi mtakuwa mnakosea Sana.
👉Kila mtu Ana jikuna ana poweza
👉Vipato vya watu havilingani
👉Kila mmoja ana malengo na vipaumbele vyake
 
Inategemea umejenga nyumba ya aina gani, gharama gani na eneo gani. Sio kwamba wengi wanashindwa kujenga au hawana hela ila hawataki kujenga vibanda vya kujikinga na mvua, kujenga eneo mvua ikija utafute ngalawa na nyumba paa limenyanyuka kama mnara wa babeli!
 
Back
Top Bottom