Ahadi za Rais Magufuli kuhusu uchaguzi huru na haki hazitekelezeki, ni ahadi hewa kimazingira

Ahadi za Rais Magufuli kuhusu uchaguzi huru na haki hazitekelezeki, ni ahadi hewa kimazingira

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Hivi karibuni Rais Magufuli alipozungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na mambo mengine alitoa ahadi ya kufanyika uchaguzi huru na haki mwaka huu wa 2020 jambo lililoleta mjadala sana kwenye jamii.

Hii kauli haitekelezeki kwa sasa. Hakuna mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na haki.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kwamba muundo wa Tume ya UCHAGUZI SIO HURU, mfumo wetu ambapo mwenyekiti wa Chama Tawala ( CCM ) ambae ni Rais ndio huchagua Mwenyekiti na Mkurugenzi wake, na Maofisa kuwajibika moja kwa Serikalini ndio tatizo la kwanza. Hali hio tu basi inatosha kuufanya uchaguzi usiwe huru na haki. Mwenyekiti na Mkurugenzi wanapokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM. Hakuna HATUA YOYOTE YA KUUNDWA tume huru hadi sasa.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya kuondolewa wakurugenzi wa Halmashauri na manispaa kuwa wasimamiaji wa chaguzi kwenye ngazi ya Jimbo na wqilaya kutokana na kuwa ni wakereketwa wa chama Tawala. Imefika mahali hadi mahakama ikataka wazuiwe lakini chama TAWALA NA TUME WAMEENDELEA KUWATUMIA KWA MASLAHI YAO. Huu ni ushahidi mwengine kwamba hakuwezekani kukawa na Uchaguzi huru na Haki kwa sasa. Vitimbi vya karibuni vya Wakurugenzi hawa kujificha na kufanya figisu kwa wapinzani ni dhahiri hakuwezekani kufanyika uchaguzi huru na haki.

Serikali ya Rais Magufuli kulea uhuni wa watendaji waliovuruga chaguzi tena wazi wazi kuanzia zile za marejeo na za serikali za mitaa ni ishara nyengine kwamba hakuna utashi na hakuna uwezekano wa kufanyika uchaguzi huru na haki.

Kwa ufupi wa maneno instrumentally, hakuna mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na haki na vile vile kiutashi na kimadaraka kwa utawala uliopo hilo haliwezekani.

Hali hio haiko kwa Bara wala Zanzibar. Wakati Zanzibar kuna Malalamikoi ya uandikishaji tayari na hakuna hatua yoyote iliyo wazi ya kutatua tatizo basi tayari ni ushahidi kwamba hiyo ahadi ya Uchaguzi huru na Haki imeshafeli.

WATANZANIA WANASUBIRI AHADI ZA RAIS MAGUFULI.
Watu wanasubiri viashiria walau, Rais Magufuli atathubutu kupeleka mswaada wa kuundwa Tume Huru wakati huu?

Je, wadau watashirikishwa muundo wa Tume unaotakiwa na kuridhiwa na wote?

Je, wakurugenzi wa Halmashauri na tarafa wataondolewa kuwa wasimamiaji wa chaguzi.

Muda ndio utaongea lakini ni wazi mazingira ya SASA HAYARUHUSU KUFANYIKA UCHAGUZI HURU NA HAKI.

Kishada.
 
The best thing he did, ameadmit in a way kwamba huko nyuma Tanzania hatukuwa na Chaguzi za Huru na Haki .............!!
 
The best thing he did, ameadmit in a way kwamba huko nyuma Tanzania hatukuwa na Chaguzi za Huru na Haki .............!!
Mkuu wewe unaamini kutakuwa na uchaguzi huru na haki kwa mazingira yaliyopo?
 
Mbona vyama vya siasa havionekani " kuitamani" hiyo Tume huru bwashee?

Hapo chini ni kauli ya nani na alikuwa anajibu kuhusu nini?

Johnthebaptist
JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
rep.png
25,355
point.png
2,000

Khaligraph Jordan said:
@johnthebaptist Yuda njoo huku
Hahahaaaa....... Tume huru haishuki kutoka mawinguni bwashee!

Mtajuta kulikimbia bunge la katiba.
 
Hermanone,
Kumbe anakusudiwa mtu fulani ajute, sio Tanzania isije ikajuta? By the way jee kuna uwezekano wa uchaguzi huru na Haki kwa mazingira ya sasa?
 
Hermanone,
Wapinzani " wangetamani" Tume huru ya uchaguzi wasingesusia bunge la katiba kwani ilikuwa ndio fursa ya pekee kuweza kuipata zaidi ya hapo ni kupiga makelele tu!
 
Wapinzani " wangetamani" Tume huru ya uchaguzi wasingesusia bunge la katiba kwani ilikuwa ndio fursa ya pekee kuweza kuipata...........zaidi ya hapo ni kupiga makelele tu!
Wapinzani walisusia bunge la katiba baada ya wajumbe wa ccm kutupilia mbali maoni ya wananchi yaliyokusanywa na kamati ya jaji warioba na kuja na maoni ya chama chao. Hata hilo nalo unataka upelekwe shule ili uelewe?
 
Wapinzani walisusia bunge la katiba baada ya wajumbe wa ccm kutupilia mbali maoni ya wananchi yaliyokusanywa na kamati ya jaji warioba na kuja na maoni ya chama chao. Hata hilo nalo unataka upelekwe shule ili uelewe?
Kwahiyo suluhu ilikuwa ni Kukimbia badala ya kupambana?!
 
Mazingira hayaruhusu mpaka kufanyike mbadiliko kwanza. Na hilo la Mabadiliko ndicho kipimo cha kwanza lakini tayari kuna tatizo limeanza la uandikishaji kule Zanzibar ambalo linalalamikiwa kwa dosari lukuki. Mpaka hapa ahadi haitekelezeki.
 
Back
Top Bottom