Ahadi za uongo za marafiki

Nashukuru sana,ila bado tunaishi ngoja tuone mbele,kukwama kupo tu,kuna mahesabu nilikosea ndio nikaingia uhitaji,sasa jamaa nimezoea hata yeye aliwahi kupata shida na nilimpa kiasi kikamuinua,kwangu yamenipata amepiga tukio,lakini najua atakuja kwa shida.
 
Asante mkuu,umeongea mema Sana🙏
 
siku ukipitia hali niliyopitia,haya uliyoandika hapa utarudi kusema yabatilishwe.

nashukuru kwa mchango wako,ila kukopa si laana,kumbuka sijaomba hivyo nitarudisha.
 
Binaadamu wengi Huwa wanadhani Wana marafiki wa karibu na ndugu wanaowapenda sana lakini Hilo hubainika kuwa wadhaniavyo ndivyo sivyo mpaka pale siku Moja watakapo fikwa na shida/matatizo
 
Kila mtu na maswaibu yake mwamba kuna wengine hawajui kukataa .Mi kuna Uncle wangu ukimwambie niazime elf 20 utasikia sawa badae kidogo uncle ,milioni 5 nayo ni hivyo hivyo utasikia nipe muda hii niweke kwenye account yako au.Lakini hatumi hata 100.
Nina hili tatizo [emoji848]
 
Na wewe mpotezee unafikiria kuendelea kumtafuta wa Nini kwani mzazi wako huyo?
Hebu endelea kutafuta Hela achana na hiyo mbuzi kwanza anakudharau anajua haumwongezei chochote hata akikupoteza.
 
Kujitegemea kunaleta heshima sana,sema TU bas Kuna muda mambo yanakaba[emoji26]

Huenda hajapata mkuu,sema inatakiwa akujulishe Ili uangalie njia nyingine
Umenikumbusha mbali Sana!!
 
Una macho lakin huoni ,ifike hatua muwe na akili basi ,ukiona hivo jiongeze maana yake kakwama hawezi kukusaidia ,na sio wote wenye uwezo wa kuja kukuambia kuwa kakwama hawezi kukusaidia ......

Huko shuleni mlienda kusomea ujinga ,vitu vingine vinaonekana ila unakuta mtu kakaza fuvu ,et mpaka aambiwe ....acha kulalama tafuta Hela ...
 
toka lini rafiki akawa msaada wako?
marafiki ni watu Wa kubadili stori na kuishi nao kuwepo kwa wakati wa raha zako
usitegemee rafiki sio business partner huyo wengine hawawez kusema siwez saidia ila matendo yataonyesha kuwa hawez kukusaidia
 
relax mkuu
mi kuna jamaa ni rafiki kichizi,nimemshika mkono sanaa

siku nikawa na shida ya laki moja nikamwomba msaada majibu yake ni nakutumia (najua ana fedha maana kuna mishe tunafanya na yake iliwahi kutiki kabla yangu) nikamwibukia kwake nakuta anakarabati nyumba akanihaidi atanipa siku iyo ila wapiii

baada ya wiki 2 inshu yangu ikatiki pia akaniomba laki 3 hahahaha akipiga simu huwa napokea kwa kiitikio cha `wewe wa kuninyima laki" alafu nauchuna

huyu bwana nimemuweka kwenye orodha ya jamaa zangu watakao kumbana na vikwazo vya kiuchumi miaka yote. pia nimemwondoa kwenye orodha ya watakao fahamu kipato changu
 
Kila mtu na maswaibu yake mwamba kuna wengine hawajui kukataa .Mi kuna Uncle wangu ukimwambie niazime elf 20 utasikia sawa badae kidogo uncle ,milioni 5 nayo ni hivyo hivyo utasikia nipe muda hii niweke kwenye account yako au.Lakini hatumi hata 100.
[emoji1787][emoji1787]Nina kaka angu nayeye hajui kukataa ila hutapata hata 100..Kuna siku nlimuuliza sababu akadai hapendi kumkatisha mtu tamaa!
 
Na hiyo ndio dawa ya rafiki mnafiki. Siku yakimkuta na ww unamkanyagia tu.
 
Meet nae face to face
 
siku ukipitia hali niliyopitia,haya uliyoandika hapa utarudi kusema yabatilishwe.

nashukuru kwa mchango wako,ila kukopa si laana,kumbuka sijaomba hivyo nitarudisha.
Hapana nimepitia mengi tu siwezi kukuambia hapa..Ninachotaka kukuambia kwamba usilaumu ndo washaamua hao marafiki
 
Akija msaidie itamuuma zaidi kuliko ukilipa kisasi cha kutokumsaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…