Ahadi za Viongozi kuhusu kuanza kwa Huduma za Usafiri wa Treni ya SGR zimedumu kwa miaka 5 na bado haijaanza kazi

Ahadi za Viongozi kuhusu kuanza kwa Huduma za Usafiri wa Treni ya SGR zimedumu kwa miaka 5 na bado haijaanza kazi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa takriban miaka 5 kumekuwa na ahadi kutoka kwa Mamlaka mbalimbali juu ya kuanza kwa huduma za usafiri wa Treni yenye Kasi zaidi (SGR) lakini utekelezaji wake umekuwa na mabadiliko ya muda mara kwa mara yanayotajwa kusababishwa na kutokamilika kwa baadhi ya Miundombinu.

Hapa kuna mtiririko wa ahadi zilizowahi kutolewa na Viongozi kuhusu kuanza kwa huduma hizo tangu Februari 2019 mpaka ahadi ya hivi karibuni ya Desemba 2023 kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa.
1701669895974.png

Mdau wa Huduma za Usafiri una maoni gani kuhusu Mradi huu?
 
Bora Mbarawa akae kimya ,wakikamilisha Kila kitu ndio watoe taarifa ya uzinduzi
 
Unapoongoza Ng'ombe always unakuwa Comfortable kuwafanya lolote unalotaka.

Ng'ombe hawana jeuri ya kuchukua hatua kwa Mchungaji wake.

Note,. Siongelei Ngombe
 
Binafsi huu mradi hata siuelewi jinsi unavyoenda na huko watajua wenyewe.
Kubwa ningeonba tu mamlaka husika watufungukie njia za Majumba Sita na Njia panda ya Airport kama walivyofanya Vingunguti kwani kero imekuwa kubwa sana ya watumiaji wa barabara kwa kufunga haya maeneo halafu hatuoni mtu/harakati zozote ktk maeneo husika ya ujenzi/site.
 
Unaweza kukuta mkopo wa SGR umeshaanza kulipwa alafu mradi haujulikani utakamilika lini
 
Abood na shabib wanaangalia tu mnavyopapatika.
 
Back
Top Bottom