Ahirisho la 'press conference' ya Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka

Ahirisho la 'press conference' ya Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Bwana Shaka msemaji wa CCM Taifa ilitarajiwa angekuwa na kikao na wanahabari, lakini kwa mshangao wa wengi press conference imesogezwa mbele.

Ni dhahiri mada kuu ni mustakabali wa Spika wa Bunge Mh Ndugai.

Najaribu kufikiri sababu za kuhairisha press conference najikuta nawaza tofauti na waTanzania wengi.

Kwamba Ndugai ni mkosaji saaaana. Kwamba Ndugai lazima kichwa chake kiliwe. Kwamba kukopa mabilioni kwaajili ya ujenzi wa madarasa kusihojiwe. Kwamba tozo tuliyoambiwa ni kwaajili ya kujenga vyumba vya madarasa haitoshi.

Akili inaniambia hicho kikao cha Halmashauri kuu kuna watu wachache wenye akili za kuhoji kulikoni.Mbona kasi ya kukopa imekuwa kubwa ndani ya miezi michache.

Nahisi hicho kikao kimekumbana na mpasuko mkubwa kuliko ilivyotarajiwa.

Nahisi Ndugai sasa anabembelezwa amsaidie Rais kwa kujiuzulu kwakuwa asipofanya itakuwa ni kumfedhehesha Rais.

Ni hayo tu kwa leo

Ngongo kwasasa Kongwa.
 
Nadhani watu wenye hekima na saburi wamewashauri wasifanye mambo kwa pupa,bali kwa tuo, tafakuri na hadhari

Wale raia kutoka nchi jirani ambao pia ni raia halali kabisa wa nchi hii walishaiteka Serekali,nadhani wenye chama wamewakatalia.

Inatafutwa njia namna bora ya kuokoa jahazi.

Kama ulifuatilia mkutano wa Mh Sana,wale wote waliokuwa wakimnanga Mh wa Kongwa ni wateule wake.
 
Ndungai asiwanyenyekee hao maboya , alaf kuomba msamaha lilikuwa kosa la Karne , kama vip awasikilizie wanachotaka wafanye na wafanye na hakuna kujiuzulu , tozo lazima zihojiwe na ukopaji wa pupa lazima uhojiwe ,
 
Tusimwangalie Ndugai,tutazame hoja zake.Wazungu wana Msemo wao “even a broken clock is right twice a day”
Screenshot_20220106-050627.jpg
 
Tusimwangalie Ndugai,tutazame hoja zake.Wazungu wana Msemo wao “even a broken clock is right twice a day”
Nitamsamehe yote Ndugai lakini si ukatili aliyomfanyia Tundu Lisu, kumnyima matibabu na kumvuwa ubunge.

Kama ningekuwa na mamlaka huyu ni mtu wa kupigwa risasi hadharani ili iwe fundisho kwa wengine.

KARMA ndio inamtafuna sasa, malipo ni hapahapa duniani.
 
Back
Top Bottom