Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Katika moja ya Interview ya Haji Manara wakati akiwa ni msemaji wa Simba, alishawahi kusema "Mimi sitadumu Simba milele ipo siku nitaondoka na atakuja mtu mwingine. Haji amefanya mengi sana na sidhani kama itakua fair kumjudge msemaji ajae kwa kumfananisha na Haji viatu vyangu ni vikubwa ila tukimpa support atafanya atakapo weza". Kipindi hicho Haji alikua kipenzi cha Wanasimba na alikua na confidence ya kutosha sana. Katu hakua na shaka na ukubwa wake.
"Mimi hapa mmoja ni sawa na wale wote kule Utopolo (Bumbuli na Nugaz), Haji mtu mkubwa bwana" Hayo yalikua maneno ya Haji kudhihirisha ukubwa wake. Siku zikapita Haji akang'atuka Simba kwa style iliyofanya kila Mwanasimba kusahau yote aliyoyatenda, mwamba akawa mkosoaji mkuu wa Simba.
Baadae Simba wakamtambulisha Ahmed Ally kama Manager wa mawasiliano na habari. Katika Interview akiwa Clouds Fm aliulizwa unahizi unaweza kuvaa viatu vya mtangulizi wako ambae alifanya makubwa sana ndani ya Simba na alikua kipenzi cha mashabiki. "Kuhusu mtangulizi alifanya makubwa sana ndani ya Simba ingawa kwa namna alivyoondoka ameifanya kazi yangu iwe nyepesi zaidi. Wanasimba walikua wanahitaji mtu wa kuwasemea baada ya kuachwa na mtangulizi wangu, hivyo hakuna uzito wowote".
Kitu alichotegemea Haji kingekua mlima kwa mrithi wake imekuja kua tambalale sababu ya namna alivyoondoka. Na uzuri ni kua mtu aliyekuja ameingia na kuanza kufanya kazi yake na ikaonekana kwa namna tofauti na ile ya mtangulizi wake. Ingawa ni ukweli usiopingika Ahmed bado sana kumfikia HAJI ila jamaa kashaingiwa na wasiwasi kuona ile legacy aliyodhani itakua mlima ishaanza kufutika ndani ya miezi mitatu. Hata zile kauli zake za kusema yeye ni mkubwa huliko wote sasa hivi ameacha na ameanza kuona mbali ya makubwa mtu anayoweza kufanya, ukishawapatia watu sababu ya kukusahau wanafanya hivyo.