Ahmed Ally amtetea Chasambi baada ya kujifunga bao lililoigharimu timu yake

Ahmed Ally amtetea Chasambi baada ya kujifunga bao lililoigharimu timu yake

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Rasmi leo ndio umekua mtu mzima wa kimpira, ingekua kimaumbile tungesema umebaleghe hii leo

Matusi, kejeli, na dhihaka zote utakazopokea leo ni ukaribisho kwenye ukubwa wako, yasikutishe tamaa na wala yasikuvunje moyo, KARIBU UKUBWANI

Umeumiza mioyoo ya Wana Simba, lakini wewe sio wa kwanza kwenye mpira, wapo wenzio makosa yao yaliwanyima Kombe la Dunia

Kosa hili linakuongezea ukomavu

Ndugu zangu Wana Simba najua tunahisira na kijana wetu lakini kila mtu kazini kwake anakosea

Na tukumbuke kabla ya kujifunga alishaisaidia timu kupata goli hivyo sukari na chumvi vimechanganyikana hii leo na bahati mbaya chumvi imezidi

Tukasirike lakini tusimchukie, na kama haitoshi tumsamehe na tuanze kumtia moyo

Kipindi hiki anatuhitaji zaidi sisi familia yake kumtetea na kumpigania ili arejee kwenye utulivu wake wa kiakali na aendelee kuipigania Simba yetu

Tunapatia pamoja, tunakosea pamoja, tunajisahihisha pamoja tunasonga mbele
IMG_2975.jpeg
 
Kaongea vema kabisa, ila hawa madogo ndio wawe wanachagua maneno ya kuzungumza, kwa soka letu la afrika kuongea vile ni changamoto, na sio afrika hata huko ulaya mchezaji wa tottenham, umsifie wa arsenal, ama wa Liverpool uwakane wenzio kisha ukampambe wa man u.. Kazi ipo
 
Sema huyo dogo hajui kupambanua mambo, akili imelala, ni aina ya wachezaji kama akina Ngasa ambae akiwa Azam Fc alivaa jezi ya Uto ndani na nje ya Azam Fc na akaivua ya Azam ili kuonyesha mahaba Kwa Uto, akili kisoda!
Hajui kama anapokuwa mchezaji wa timu Fulani anatakiwa awe na ushabiki wa hiyo timu Kwa wakati huo, ndio maana kuna kubusu jezi n.k hata kama hakuwahi kuipenda hiyo timu kabla. Sasa Kutokana na ufala wake kajitengenezea chuki kutoka Kwa mashabiki.
 
Kaongea vema kabisa, ila hawa madogo ndio wawe wanachagua maneno ya kuzungumza, kwa soka letu la afrika kuongea vile ni changamoto, na sio afrika hata huko ulaya mchezaji wa tottenham, umsifie wa arsenal, ama wa Liverpool uwakane wenzio kisha ukampambe wa man u.. Kazi ipo
Yule dogo usikute ni yanga, au alibeti both team to score
 
Mimi sio mtabiri lakini naona career ya huyu dogo pale msimbazi imeishia hapa, na alivyosema role model wake ni Nzengeli hapo ndo mchezo ulipoishia.... Yaani upo ccm unasema unampenda Tundu Lissu utabakije salama...
 
Kwenye hilo la kuonyesha appreciation kwa mtu sina shida nae, sababu sio wa kwanza. Hata Nzengeli anaonyesha kumkubali Awesu sana tu. Pia ligi kubwa ni kawaida tu.

Huenda ni kweli ana mahaba ya dhati kule ila hili la leo limeharibu kabisa atmosphere, watu wataunganisha na kauli yake kisha watapata conclusion
 
Mashabiki wote wanaomtukana huyo dogo, ndiyo wale walioitwa mbumbumbu na Rage. Kwa shabiki mwenye akili timamu atagundua makosa kama hayo yamekuwa yakifanyika kila siku duniani kote, kwenye mpira wa miguu.
Kwa wachezaji wenye uwezo mdogo kama huyu. Kwanza nyuma kuna mpinzani, kipa hayupo kwenye nafasi sahihi.

Bado unamchezaji mwenzako jirani unapigaje mpira mrefu kama ule. Tena basi mlenge golikipa alipo. Unatafuta post ya mbali.

Dogo amezingua sana, kwanza yeye si beki anahangaikaje kupiga pasi ya kipa tena hakuwa na presha kubwa.
 
Aisee nyie wakina Amedy pamoja na huyu dogo chasambi msituzengue.

Mnajua machungu ya kukosa ibimgwa x3 mfululizo?

Alafu tunapata mafasi ya kuchukua ubingwa tunaichezea?

Sisi mashabiki hatuwaelewi kabisa na hatuta waelewa tena tukiukosa ubingwa msimu huu kwa ujinga huu wa kuchezesha wachezaji wasiojielewa

Hata yule jean Awa awekwe bechi nafasi nyingi Amepata ameishia kufanya mizaatu.
 
Sema bora dogo chasambi kuliko mutale, kibu angekuwa ndani asinge Fanya ule upuuzi
 
Back
Top Bottom