Ahmed Ally bado ana Utoto, Usemaji wa Kipuuzi ambao si Level ya Simba

Sisi Mashabiki ndio Waajiri Halali Wa Hawa Maafisa Habari.....kupitia Kamati Zetu Tendaji za hizi Timu.., tutawaeleza Afisa Habari tunayemtaka Aweje..!

Mtu kama Msukule aendelee tu Kupumzika... yaani Hatakiwi, hata akimaliza Kifungo chake Cha Miaka miwili aendelee tu Kuongeza 'Wake zake' baaaasi ndo anachokiweza...!

Kwenye Usemaji Wa Klabu Big NO..!
 

Mbona humsifii kajaza uwanja juzi kutokana na kuhamasisha mashabiki waingie uwanjani
 
Sasa kama wao mashabiki wa timu hizo ndio mnapenda aina hiyo ya usemaji wao wafanye nini?Huyo kamwaga wanasimba walikuwa wakimponda kuwa amepooza kama mkojo wa ngedele!!kutokana na u smart aliokuwa!!!Nyie si mnapenda ule usemaji wa ki propaganda,mala kwa simba hii hata BARCA,tena ile ya kina Niesta,hawatoki!! Kwani humuoni hata huyo wa YANGA mpya,alikuwa smart lakini ili kwenda na vibe la mashabiki wa timu yake,ameshakuwa pompoma!!!
 
Kumjibu yule msukule nafikiri ni kumuongezea umaarufu na attention

Mjinga hajibiwi, ni kama kupigana mweleka na nguruwe
 
Kiongozi mzuri hapelekeshwi na hisia za mashabiki ambao wengi mbumbumbu
Kutukana timu pinzani kama alivyokuwa akifanya Manara ni upuuzi mkubwa ambao hauna afya kwa soka

Mtu anasema kwenye club flani wenye akili ni watu wawili tu, sportsmanship iko wapi?
Kuna siku katukana wachezaji wa Yanga na kusema Yanga wanaokota takataka
Kawaita mashabiki wake nyani baada ya ile kauli ya Luc Eymail
Katukana na kudhalilisha waandishi wa habari mara kibao.

Hivi ndivyo mpira wetu unatakiwa kuwa?
Kuna kupigana vijembe vya hapa na pale lakini matusi kama haya ni too much
After all Simba na Yanga zimefanya vizuri kipindi cha nyuma bila kuwa na watukanaji kama hawa
 
Yanga wamechoka kweli kweli hadi wanatia huruma. Sasa hivi hawataki kuzodolewa.

Mleta mada ameleta ushauri mzuri ila kama baadhi walivyokujibu, wasemaji wanaendana na vibe la waswahili ambao ndiyo hasa mashabiki wa timu hizi mbili. Ukileta 'uzungu' sana utakwama.

Ila Simba na Ahmed Ally wanajitahidi kupunguza maneno ya kejeli. Leo nasikia amesema Simba wanaihofia mechi inayokuja na Yanga. Hauwezi kumsikia mtu wa Yanga akisema kitu kama hicho.
 
Club Africain ameanza kuwachanganya
Huyu Sasa ndo shabiki halisi wa mpira wa Tanzania. Kuna wakati hawezi hata kukupangia line up ya Simba lakini ni msema chochote.
 
Kijna yule anaongelea kwenye pua nletee nzu guuu ngoja aje apigwe nnje ndani lzm sauti iitoke tu
 
Mimi ni shabiki wa ahmed ally, jamaa anaupiga mwingi sana. Zile spana zinawapata vilivyo utopolo.

Mpira wetu ukileta uzungu hatukuelewi kabisa yani. Ili ujue hili soka kuna content za kikwetukwetu ni hili suala la wasemaji wa team sina uhakika kama kuna sehemu nyingine wa utaratibu huu.

Halafu huwa inashangaza sana, unawezaje kudharau watu kutokana na elimu yao? Wakati hao ndo wakiambiwa njooni uwanjani wanakuja? Wakiona jezi mpya wananunua? Unapata wapi nguvu ya kusema "uswahili".

Spana muhimu sana zile zinaleta amani sana.
 
Ahmed yupo vizur nakubaliana nawe
 
Shida ya Ahmed ni mswahili, kwangu wasemaji walikuwa dis 10 na kamwaga hawa wengine mi naona ni takataka tu
Kabisa. Nlipenda watu smart kama hao.
 
Declare interest, wewe ni Yanga?
Nlikuwa nadhani wewe ni mtu mzima unayejielewa. Ila kwa hii comment kama pamoja na kusoma nlichoandika hujaelewa. Napata mashaka sana na umri wako. Kuna age ambayo wengine tulishavuka na ngazi ya ushabiki ambayo hatupo tunahitaji tu kuwa na discussion na wanasimba wenye uelewa na si ushabiki maandazi.

Simba ilianzishwa ikiwa ni team yenye mashabiki wenye Elimu na kwa miaka mingi imekuwa na ustaarabu wake ukiacha hapo katikati walipokuja mashabiki wa haji manara ambao mostly ni watoto wadogo wasioifahamu Simba. Hawa huwa sioni kama ni sahihi kwangu kubishana nao.
 
Hapo umeongea sawa. Wewe shabiki wa Ahmed Ally. Kama ambavyo ulikuwa Shabiki wa Manara. Mimi nahitaji kujadiliana hili na Wapenzi wa Mpira wanaoipenda Simba. level ya mashabiki wa watu hiyo ni ya wasio na elimu au watoto.
 
Mwanasimba kama mwanasimba hahitaji mtu wa kumwambia njoo uwanjani au nunua jersey. Anafahamu wajibu wake. Nyie ndo mlikuwa mnapa kichwa hata yule bwatubwatu manara akadhani yeye ndo anajaza uwanja wa mkapa.

Sisi tunaenda kuiangalia Simba inafungwa na Stella ya Abjan Taifa hatukuhamasishwa na mtu. Miaka yote Simba inacheza nikiwa Taifa inamfunga Club Sports Villa ya Uganda bao 3 enzi za akina Z. Mogella na Coach Mchezaji H. Afif hakuna ambaye alituita Uwanjani. Simba ni club inayojitegemea haihitaji kuwa kama Yanga au kwa sasa kushindana na Yanga.

You need to have certain intelligence to understand this.
 
Mshkaj anatakiwa abadlike
Watu hawawezi kuelewa. Watakwambia wao ni Mashabiki wa Ahmed Ally. Tuna kazi sana kutoka huku tuliko kwenda level za wenzetu. Simba inatakiwa kuwa level za juu zaidi ila kuna ukale bado unasumbua.
 
Kila mtu anataka msemaji wake, huyu anataka uzungu mwingi, yule anataka uswahi mwingi, sasa kwa vile msemaji ni mmoja tu hawezi kuwa navyo vyote mia kwa mia bila shaka Ila kwangu Mimi Ahmed Ally anajitahidi kubalance, huwezi kumridhisha kila mtu, kijana songa mbele...Simba wengi tuko nyuma yako, wachache sana wasio kukubali na hilo ni kawaida, huwezi kupendwa na watu wote wewe sio hela.
 
Ezekiel Kamwaga yupo Uingereza anasoma, huyu Ahmed Ally na Manara ni chupa na mfuniko tu, wote wapumbavu watupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…