Ahmed Ally bado ana Utoto, Usemaji wa Kipuuzi ambao si Level ya Simba

Ahmed Ally bado ana Utoto, Usemaji wa Kipuuzi ambao si Level ya Simba

Hapa kuna wanaoangalia tv nyumbani huku wameshika remote watoto wasijeweka katuni VS Tunaoangalia kwenye mkusanyiko na vibe kubwa.
Hapa hatufiki mwisho, mimi mwenyewe napenda usemaji wa Ahmed ila tu asivuke mipaka kama ya yule wa kwanza kuwa na mabifu na waandishi na kuwadhalilisha.
 
Hapo umeongea sawa. Wewe shabiki wa Ahmed Ally. Kama ambavyo ulikuwa Shabiki wa Manara. Mimi nahitaji kujadiliana hili na Wapenzi wa Mpira wanaoipenda Simba. level ya mashabiki wa watu hiyo ni ya wasio na elimu au watoto.
Unachokosea ni kuhisi kuwa wewe una elimu kuzidi wengine au ni mkubwa kuliko wengine. Basi umeshinda tunaompenda ahmed ni sisi darasa la saba B na tumezaliwa 2004.

Aina ya watu kama wewe ni wale ambao sababu anawajua kina zamoyoni mogella,Hussein Marsha, Mwameja Mohammed basi unahisi wewe ndo unamapenzi na simba kuliko yeyote.
 
Mpira wetu umetengenezwa kwenye utani fulani hasa kwa Simba na Yanga......kama ndiyo unaanza leo kufuatilia lazima upate shida sana.....ila hata aje Malaika awe Simba or Yanga, hawezi kuisemea timu moja bila kuitaja nyingine ni ngumu
Umemjibu vema sana na uzi umeishia hapa
 
Mpira wetu umetengenezwa kwenye utani fulani hasa kwa Simba na Yanga......kama ndiyo unaanza leo kufuatilia lazima upate shida sana.....ila hata aje Malaika awe Simba or Yanga, hawezi kuisemea timu moja bila kuitaja nyingine ni ngumu
Tunaelewa utani,, lakini tunatarajia kuona mipanga mikakati ya kuzifanya timu zetu ziende mbele zaidi ! Sio kila siku unawaza mtani tuu yaani msemaji anatumia nguvu nyingi kuliko akili na weledi wa kazi wakati mwingine msemaji anaropoka ya kwake tu
 
Pole sana mkuu umeandika kwa Huzuni nyingi.

Mimi ni Simba Lia Lia.

Huyu kijana anatafuta Tension, umaarufu, usimba kindaki ndaki, unazi nk.

Sishangai kufanya Hivi ndio utamaduni wa vilabu vya Simba na. Yanga, Lazima umcharule mpinzani, umseme, umkomoe nk.

Hawawezi KUSIMAMA kwenye mosingi ya weledi wamejaa kunangana.

Mashabiki wa vilabu Hivi masikini ndio Huwa wanapenda sana kunangana kuliko weledi.
Kamwaga alikuwa mtu sahihi sana sana.
Kwa muda mfupi niliona akileta hamasa na sio mpenda vijembe wala mropokaji
 
Ahmed hatukani mtu,hadhalilishi mtu, ila utani wake unakera. Mbaya zaidi mkimuundia kitu anakutumia kama fursa. Mlete mzungu, kispika nk.....ametumia kama fursa mkajikuta weupe
 
Hapa kuna wanaoangalia tv nyumbani huku wameshika remote watoto wasijeweka katuni VS Tunaoangalia kwenye mkusanyiko na vibe kubwa.
Hapa hatufiki mwisho, mimi mwenyewe napenda usemaji wa Ahmed ila tu asivuke mipaka kama ya yule wa kwanza kuwa na mabifu na waandishi na kuwadhalilisha.
Ni hivyo tu mkuu. Safi sana
 
Mshkaj anatakiwa abadlike
Watu hawawezi kuelewa. Watakwambia wao ni Mashabiki wa Ahmed Ally. Tuna kazi sana kutoka huku tuliko kwenda level za wenzetu. Simba inatakiwa kuwa level za juu zaidi ila kuna ukale bado unaisumbua club.haujatoka wote. CEO Aendeshe club kisomi.
 
Mbona humsifii kajaza uwanja juzi kutokana na kuhamasisha mashabiki waingie uwanjani
Hili wazo mlianza kumpa na haji kuwa ndo anajaza uwanja. Hii ni akili ya wapi? Anajaza uwanja anatoa wapi hao watu? Team ikifanya vizuri watu wataenda tu uwanjani. mimi naenda uwanjani toka.early 90s hakuwepo yeyote kati ya hao. Achaneni na hii dhana please.
 
Kamwaga alikuwa mtu sahihi sana sana.
Kwa muda mfupi niliona akileta hamasa na sio mpenda vijembe wala mropokaji
Kamwaga ni smart. Anajielewa. Na yule ni mwanasimba hasa. Ana mapenzi na Simba na ana mapenzi na mpira. MIMI BINAFSI SIONI FAIDA YA VIJEMBE NA KUROPOKA. mbona walioendelea hawapo hivyo na tunaiga mifumo yao?
 
Ila jamaa ana ongea kishamba shamba sana, itakua muda mwingi kautumia akiwa vijijini yani kila nikimuangalia amekaa ki kijijini kijijini tu
 
Ahmed hatukani mtu,hadhalilishi mtu, ila utani wake unakera. Mbaya zaidi mkimuundia kitu anakutumia kama fursa. Mlete mzungu, kispika nk.....ametumia kama fursa mkajikuta weupe
Kutumia fursa za kejeli za wengine ni jambo jema. Kwa nini asijikite katika kuizungumzia simba pekee mpaka aitaje yanga au aikejeli? Hapo sioni faida. Kwa nini asijikite kuifananisha Simba na Clubs kubwa za level yake? Kuna level inabidi kutoka kuachana nazo. Simba wangeachana na kujifananisha na Yanga kuonesha Simba ni level ya juu.

Simba inapaswa ishindane na Orlando, Al Hilal, Al Ahly n.k huko ndiko inapaswa iwe. Kuhangaika na yanga ni wendawazimu. Ninyi wengije mnapenda mipasho n.k mimi sioni faida yake zaidi ya Uhasama wa kipuuzi ambao hausaidiii soka letu. Yanga kupoteza liwe somo la Simba. Kuangalia yanga wamepotezaje. Then simba i move on. Haina haja ya kuzungumzia Yanga.
 
Ila jamaa ana ongea kishamba shamba sana, itakua muda mwingi kautumia akiwa vijijini yani kila nikimuangalia amekaa ki kijijini kijijini tu
Anataka kuita ushamba wa Haji. Haji naye ana ushamba mwingi sana. Na Ushamba ni tabia si mtu alikokaa. Haji amekaa kariakoo na bado ni mshamba sana. Ni usemaji wa kiswahili wa kishamba usio na akili.
 
Yani mbona anaongea kawaida sana hana matusi hana lugha mbaya na matusi japo maneno yake kama ni mpizani lazima yakukere lakini hajavuka mipaka kama Bi Ashura
 
Mzee wa kispika [emoji350] awaamini macho yaooo[emoji41]
 
Huu ujinga ulianza kipindi cha Haji Manara na Jerry Muro sasa hivi umeambukiza wengine
 
Soka letu kivyetu vyetu ahmed ally piga kazi baba usitishwe na kibwengo yoyote
 
Binafsi naona msemaji aliyekuwa smart alikuwa Ezekiel Kamwaga. Huyu alikuwa professional hasa. Anajielewa na anaelewa Taaluma yake na hadhi ya Club aliyokuwa anaisemea..

Ahmed Ally nlitegemea angekuwa na cha kujifunza katika hilo. Kuwa msemaji wa kisasa mwenye weledi. Ameeenda kuangukia kwenye kundi lile lile la msemaji wa ovyo ovyo kama Manara ambaye sisi wengine tulikuwa tunamkataa toka akiwa Simba.

Tabia za kuinanga Yanga ni za Kipuuzi. Zinachochea Uadui na hazikuzi mpira wetu Kimataifa. Ndo maana unaona team ya Taifa ipo Hoi. Sababu tunapoteza sana katika Usimba na Uyanga.

Ali Kamwe alikuwa na akili alipoenda kuwa msemaji wa Yanga akili akazitoa na kubaki alivyo sasa. Mi nadhani Simba ilipaswa iache kujilinganisha na Yanga. Simba ilipaswa ijiangalie yenye na Clubs nyingine kubwa za Afrika.

Iachane na kushindana na Yanga. Ibaki kushindana na teams kubwa. Yanga ni team kama teams nyingine katika Ligi. Kujilinganisha na Yanga ni kuonesha bado Simba haijakua. Ina utoto ule ule wa miaka na miaka. Haitasaidia Club.

Yanga ikigundua kuwa nayo inapaswa i move toka hapo ilipo iangalie mbali...itabadilika. na teams nyingine pia zitaacha kukamia Simba na Yanga tu. Zitakamia Ligi nzima. Ili zikacheze mashindano Makubwa. Hivyo mpira wetu utakuwa. Team ya Taifa itakuwa imara.

Ahmed Ally. Ana Elimu bila shaka tofauti na Haji Manara ambaye hana Elimu. Afanye kwa namna ambayo tutaona tofauti ya watu hawa wawili. Simba hawana haja ya kuwa na mtu wa Kuinanga Yanga. Wa nini?Simba inahitaji mtu ambaye atakuwa daraja la Wapenzi na Uongozi na Wachezaji.

Maisha ya kunangana ni utoto na uswahili. Inawezekana kuna wanaopenda lakini pia tupo sisi hatuoni faida zaidi ya upuuzi na kujenga chuki kwa hizi teams mbili.

Tofautisha Kati ya Afisa Habari na Msemaji
 
Back
Top Bottom