Ahmed Ally bado ana Utoto, Usemaji wa Kipuuzi ambao si Level ya Simba

Ahmed Ally bado ana Utoto, Usemaji wa Kipuuzi ambao si Level ya Simba

Binafsi naona msemaji aliyekuwa smart alikuwa Ezekiel Kamwaga. Huyu alikuwa professional hasa. Anajielewa na anaelewa Taaluma yake na hadhi ya Club aliyokuwa anaisemea..

Ahmed Ally nlitegemea angekuwa na cha kujifunza katika hilo. Kuwa msemaji wa kisasa mwenye weledi. Ameeenda kuangukia kwenye kundi lile lile la msemaji wa ovyo ovyo kama Manara ambaye sisi wengine tulikuwa tunamkataa toka akiwa Simba.

Tabia za kuinanga Yanga ni za Kipuuzi. Zinachochea Uadui na hazikuzi mpira wetu Kimataifa. Ndo maana unaona team ya Taifa ipo Hoi. Sababu tunapoteza sana katika Usimba na Uyanga.

Ali Kamwe alikuwa na akili alipoenda kuwa msemaji wa Yanga akili akazitoa na kubaki alivyo sasa. Mi nadhani Simba ilipaswa iache kujilinganisha na Yanga. Simba ilipaswa ijiangalie yenye na Clubs nyingine kubwa za Afrika.

Iachane na kushindana na Yanga. Ibaki kushindana na teams kubwa. Yanga ni team kama teams nyingine katika Ligi. Kujilinganisha na Yanga ni kuonesha bado Simba haijakua. Ina utoto ule ule wa miaka na miaka. Haitasaidia Club.

Yanga ikigundua kuwa nayo inapaswa i move toka hapo ilipo iangalie mbali...itabadilika. na teams nyingine pia zitaacha kukamia Simba na Yanga tu. Zitakamia Ligi nzima. Ili zikacheze mashindano Makubwa. Hivyo mpira wetu utakuwa. Team ya Taifa itakuwa imara.

Ahmed Ally. Ana Elimu bila shaka tofauti na Haji Manara ambaye hana Elimu. Afanye kwa namna ambayo tutaona tofauti ya watu hawa wawili. Simba hawana haja ya kuwa na mtu wa Kuinanga Yanga. Wa nini?Simba inahitaji mtu ambaye atakuwa daraja la Wapenzi na Uongozi na Wachezaji.

Maisha ya kunangana ni utoto na uswahili. Inawezekana kuna wanaopenda lakini pia tupo sisi hatuoni faida zaidi ya upuuzi na kujenga chuki kwa hizi teams mbili.
Hopeless kwa Tanzania na Culture yake huwezi kuwa Msemaji mwenye Ushawishi kwa Mashabiki wa hivi Vilabu Vikubwa Viwili kama huinangi Klabu mojawapo.

Punguza Chuki zako Binafsi kwa Ahmed Ally ( Msemaji wa Simba SC ) kama uliitaka hiyo Kazi na subiri muda wake ukimalizika nawe utaomba ili ukiipata tuone kama utaweza kuyafanya haya Unayojimwambafai nayo hapa.
 
Stupid culture and perception for hopeless people. Waswahili wengi wanaamini unapomkosoa mtu unamchukia. Ndo maana wanasiasa walio kwenye vyeo wakikosolewa huwadhuru wengine sababu ya perception kama hii yako ya chuki binafsi. "Ukupigao ndio ukufunzao" wewe ukiamua kusifu na kuabudu acha wengine watimize matakwa ya kikatiba kuongea what they feel.

Ni suala la kuamua kutumia akili au kutumia tumbo/makalio. Wenye kutumia akili hukosoa na kupendekeza. Wale wengine huona ni chuki au wivu.
 
Hopeless kwa Tanzania na Culture yake huwezi kuwa Msemaji mwenye Ushawishi kwa Mashabiki wa hivi Vilabu Vikubwa Viwili kama huinangi Klabu mojawapo.

Punguza Chuki zako Binafsi kwa Ahmed Ally ( Msemaji wa Simba SC ) kama uliitaka hiyo Kazi na subiri muda wake ukimalizika nawe utaomba ili ukiipata tuone kama utaweza kuyafanya haya Unayojimwambafai nayo hapa.
Stupid culture and perception for hopeless people.
 
Back
Top Bottom