View attachment 2952641
Baadhi ya Mashabiki wa Simba waliojilipia nauli zao kusafiri kwenda kuipa support timu yao Nchini Misri
Kila shabiki amejilipia Dola 1200 sawa na Milioni 3,126,000.
Hili swala la Serikali kusafirisha Mashabiki nitatoa maoni yangu nikimalizana na Al Ahly, Sasa hivi akili inawaza namna ya kufuzu Nusu Fainali, Ila msimamo wangu ni kwamba si jambo jema hata kidogo.
Kwa Mashabiki mpira ni starehe hivyo Serikali haiwezi kugharamia watu kwenda kustarehe.
Tena bora ingekua imetoa usafiri tu. Lakini wametoa Posho Dola 500 kila kichwa sawa na Milioni 1,200,000 kwa ufupi hawa Mashabiki wamenuniliwa na wanalipwa kuishangilia timu yao.
Na hao sio Mashabiki wa kawaida ni Machawa wanaotetea maslahi ya viongozi wao yaani Serikali imelipia Machawa wa watu.
Kuwalipia nauli sio kuwapenda ni kufuga tatizo ambalo baadae hatutaweza kulitatua.
Leo unalipia mashabiki wa klabu, kesho Ali Kiba ataiomba Serikali iwagharamie mashabiki wake kwenda Marekani kufanya show utamnyima?
Twaha Kiduku ataomba aende kupigana Uingereza na mashabiki wake utamnyima??