Mkirua,
Ukitaka uwe mtu wa kuheshimiwa na uwe msomi makini chunga lugha yako.
Lugha, "kurukaruka," ni matusi, kejeli na kebehi.
Nitakufunza adabu ya mjadala.
Ingekuwa mie ni wewe swali hilo ningeliliuliza hivi:
"Mohamed Said nimeshanga namna mnavyoshindwa kujibu swali hili rahisi
mimi nakuomba utuoe jibu...ni halali au si halali?"[/QUOTE]
Aksante sana kwa darsa babu Mohammed Said. Sikujua kuruka ruka ni matusi. Leo nimeongeza hili neno katika "orodha ya Matusi" ninayoyafahamu. Kwakuwa umetunyooshea vizuri swali tungefarijika sasa ukatuwekea na jibu kwani mwalimu mzuri wa kurekebisha maswali lazima uwe na majibu.... Ni halali au si halali?
Mkirua,
Inawezekana kuwa hujui kumwambia mtu kuwa anarukaruka ni tusi.
Hata mie nimeingia katika mtego huo uliokunasa wewe.
Kuna neno
Maalim Faiza kalitumia katika jibu lake zuri sana ambalo
mimi nililiwekea "like."
Aliyejibiwa akaniambia kuwa mimi naunga mkono matusi na nilimjibu
kuwa kwetu hilo neno tunalitumia hata mbele ya wazee wetu kwani si
tusi.
Lakini nikizingatia kuwa lugha ya Kiswahili unasemwa na wengi na kila
jamii ina uelewa wake katika baadhi ya maneno nikamuomba radhi
anisamehe.
Mkirua,
Wewe nimefahamisha kuwa unenitukana jibu lako ndilo hilo ulolileta
hapa barzani...kiburi, kiburi, kiburi.
Haijakupitikia kuwa kweli umetukana kwa jinsi jamii nyingine inavyochukulia
hilo neno.
Lakini sikulaumu.
Huenda kwenu hukufunzwa.
Mimi nimefunzwa adabu kabla hata sijaanza chuo (madras) na nilipofika
madras baadhi ya adab niliyofunzwa ni adab ya majadiliano (mnakasha).
Ikiwa utanieleza mimi kama nimekutukana mathalan.
Kitakachofata kutoka kwangu si majibu ya kejeli bali ni kukutaka radhi.
Pitia maandiko yangu hapa
Majlis utaona tofauti kubwa sana.
Sasa narejea kwenye uhalili na uharamu swali ambalo linachoma nyoyo
zenu sana.
Nimejibu mara nyingi tu kuwa hilo si swali kwani kuna swali na swali na
nikatoa mfano wa jinsi
Sheikh Hassan bin Amir alipokuwa anadarsisha
alikuwa hajibu swali ambalo watu wanataka jibu lake kufa na kupona.
Sheikh Hassan alikuwa akiwaambia wasome hilo somo wao wenyewe
watapata jibu.
Nitakuwa mjinga sana mimi ikiwa baada ya kuwasoma wanazuoni wakubwa
kama hawa leo niwaghalif mimi mtu mdogo sana ambae hata viatu vyao
siwezi kuwabebea.
Nitakuwa nimetoka chuoni bila ya kujifunza kitu.