AnyWayZ
JF-Expert Member
- May 30, 2022
- 4,880
- 8,424
Hapo ndo nimecheka sana,Watekaji wakamlazimisha kuingia Kwa gari akawa mateka..
Halafu akaendesha gari peke yake huku wanamfata??
Anyway Chadema Idumu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo ndo nimecheka sana,Watekaji wakamlazimisha kuingia Kwa gari akawa mateka..
Halafu akaendesha gari peke yake huku wanamfata??
Ukimwangalia Kwa mwonekano wa nje ameweka pause, anaonekana mtu makini, bright Kweli Kweli.Nimecheka sana mh waziri mkuu kuna clip nimeona anasema watanzania tuwamini , kwamba serikali ya tz imewatega DP WORLD, Ila Majaliwa kiboko, unamtegaje Dp WORLD kwa mkataba ule?
Yale yale mambo ya Mchungaji Christopher Mtikila, Dkt. Sengondo Mvungi, Prof.Juan Mwaikusa, Prof Luvigha, Prof.Nicas Mahinda, n.k yamerudi tena kwa kasi ya tsunami hapa nxhini.
Ya Mchungaji Christopher Mtikila, Dkt. Sengondo Mvungi, Prof.Juan Mwaikusa, Prof.Nicas Mahinda yamerudi tena kwa kasi ya unami hapa nxhini.
Kuua wakosoaji kamwe haijawahi kuwa suluhisho la matatizo. Endapo kama wangefanikiwa kumuua mtu huyu kama walivyodhamiria, Je, mapungufu yaliyopo kwenye huo Mkataba wa Bandari ndio yangeondoka???????Ndugu Watanzania!
Tumeongea Ahobokile Mwaitenda ikiwa ni siku moja baada ya kunusurika kuuawa au kutekwa na watu wasiojulikana. Mwaitenda ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa CHADEMA na alikuwa ni Mgombea Ubunge Jimbo la Rungwe, Mbeya Uchaguzi wa Oktoba 2020 kupitia CHEDEMA.
Usiku wa 7 Julai 2023 akiwa anatokea uelekeo wa Mwenge kuelekea Goba, alivamiwa na watu 4 (wanaume 3 na mwanamke 1). Walimkimbiza na gari wakimpigia kelele asimame. Akifikiri huenda amegonga gari bila kujua, akakimbilia na karibu na Shule ya Makongo na kusimama.
Aliposimama wakashuka watu hao wakaanza kumpiga ngumi na mateke huku wakimfokea wakisema anajifanya anajua kusema sana juu ya Mkataba wa Bandari. Walinzi wa Shule ile waliokuwa mbali walipoanza kusongelea pale, watekaji wakamlazimisha Mwaitenda aingie kwenye gari. Muda huo tayari alikuwa mateka.
Aliendelea kuendesha gari huku wakimfuata na ndipo akakimbilia katika Kituo cha Polisi Kawe na kugonga Geti kwa gari. Alishuka haraka na kujisalimisha huku akiwa amenyoosha mikono juu. Wale watu wakegeuza gari na kukimbia.
Ndugu Watanzania! Jana tuliandika pia juu ya vitisho walivyopata wanasheria wanakosoa pia Mkataba wa Bandari ambao ni Dkt. Nshala na Boniface Mwabukusi! Mhe. Balozi Dkt. Willbrod Slaa alitishwa hadharani na kiongozi mmoja wa serikali baada ya Dkt. Slaa kuukosoa mkataba! Vitisho ni vingi sana na hatuwezi kuelezwa kila mtu anayetishiwa uhai wake.
Sisi Askofu Mwamakula tumesikitishwa sana na vitendo hivi vya kutaka kuteka, kuua na hata kunyamazisha watu waoikosoa serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Ufalme wa Dubai na Serikali ya Tanzania. Sisi tunatoa wito kwa Serikali kutoa kauli kuhusu vitendo hivi kwani wafanyao vitendo hivyo wanajinasibisha moja kwa moja na serikali. Kukaa kimya kwa Serikali katika matukio yaliyojitokeza sasa itachukuliwa kuwa ni Serikali inayoratibu na kufadhili vitendo vya kutisha na kuteka na kutaka kuua watu.
Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito pia kwa viongozi wote wa dini ili wakemea kwa nguvu vitendo hivyo kwani vinalenga katika kufinya haki na kuendelea kuondoa amani na utulivu katika taifa letu. Uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kila raia wa nchi hii. Hakuna mtu au taasisi ye yote ikiwemo serikali aliye na haki ya kuzuia wengine wasitoe maoni yao katika nchi yao.
Tunaendelea kuonya na kutahadharisha kuwa ikiwa yeyote anayeikosoa Serikali ya Tanzania juu ya Mkataba wa Bandari atadhurika au hata kuuawa, basi watu wote waliowahi kutoa kauli hadharani kuwatisha wakosaoji, basi watu hao watawajibika sambamba na serikali endapo pia yenyewe haitajitenga na vitendo hivyo.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Uamsho Duniani.
Dar es Salaam, 8 Julai 2023; 21:11 pm.
Waione na kuisoma:
1. Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)
2. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
3. Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)
4. Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
5. Tanganyika Law Society (TLS)
6. Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
7. Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania
8. Umoja wa Ulaya
9. Umoja wa Mataifa (UN)
10. Kituo cha Haki za Binadamu (LCHR)
11. Vyombo vyote vya Habari vya ndani na Nje
12. Sheikh Ponda Issa Ponda
13. Askofu William Mwamalanga
Hizi nondo hakuna wa kujibu, labda Kitenge na Zembwela au yule professor wa majalalaniHoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
😂😂😂😂😂Huyo ni nani na kwa umaarufu gani? asitafutwe slaa wala lissu hatutaki drama kama aliiba mke wa mtu amrudishe!