darubin ya mbao
JF-Expert Member
- Aug 3, 2016
- 1,899
- 4,055
Siku za maza kuanguka hazipo mbali, maumivu ya kichwa huanza kidogo kidogo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaongelea mtu specific, nimeongelea aina ya watu, nimetaja watu.Hata wewe unaamini watekaji wanafanya hivyo kama stori hii ilivyo??
Labda mtekwaji bado ana wenge!!Kwamba wamemteka halafu wakamwacha aendeshe gari mwenyewe wao wakimfata Kwa nyuma!! Acheni utani nyiee
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Hakuna anayetaka kuuza sehemu yoyote ya JMT, umepotoshwa na wewe umeingia mazima kwenye kuamini habari za uzushi.Tusipokuwa makini hata mlima Kilimanjaro siku moja atauziwa mwarabu. Tuna viongozi washamba sana
Tunataka BANDARI zetu tulipigania Uhuru Kwa kutaka Mali zetu Leo Samia MANGUNGO anagawa Kwa waarabu , DPWORLD waondoke
Kuna mambo mengi umepishana kwa hoja ila ktk hili suala hoja zako nyingi zimekuwa hazina mashiko. Mara useme wanaoidai Tanganyika ni warundi, mara watalipua makanisa, mara kuna suala la udini ktk bandari yaani umekuwa kiroja. Waache watanganyika wadai mali zao.Msilipue makanisa please..
Tunataka Amani...tupishane Kwa hoja
Amani ni faida kwetu sote
RUBBISH.hata hawajui kwamba wakiendeleza huo ujinga, wananchi nao wataamua kuchukua sheria mkononi, na hapo ndio unakuwaga mwanzo wa vita, mmarekani amekaa paleee anasuburi tugombane ili achague wa kumpa silaha watu wauane yeye auze silaha au achote dhahabu na gesi. hawa waarabu wana faida gani Tanzania hata kuja kutuondolea amani namna hii? angekuwepo magufuli wangekuja namna hii kweli ? kwamba wanagombanisha serikali na wananchi, si waondoke tuishi kwa amani kama tulivyozoea?
Watanzania kwa ujumla wetu tunazo mali zetu leo, kesho na kesho kutwa. Hizi hulka za kishenzi za kibaguzi zitashindwa milele, tupo wengi tunaiombea mema Tanzania.Kuna mambo mengi umepishana kwa hoja ila ktk hili suala hoja zako nyingi zimekuwa hazina mashiko. Mara useme wanaoidai Tanganyika ni warundi, mara watalipua makanisa, mara kuna suala la udini ktk bandari yaani umekuwa kiroja. Waache watanganyika wadai mali zao.
😃😃Huyo ni nani na kwa umaarufu gani? asitafutwe slaa wala lissu hatutaki drama kama aliiba mke wa mtu amrudishe!
Wabongo washenzi sana Kwa uongoWatekaji wakamlazimisha kuingia Kwa gari akawa mateka..
Halafu akaendesha gari peke yake huku wanamfata??
Bring back TanganyikaTusipokuwa makini hata mlima Kilimanjaro siku moja atauziwa mwarabu. Tuna viongozi washamba sana
Tunataka BANDARI zetu tulipigania Uhuru Kwa kutaka Mali zetu Leo Samia MANGUNGO anagawa Kwa waarabu , DPWORLD waondoke
14. Umoja wa Waarabu TanganyikaNdugu Watanzania!
Tumeongea Ahobokile Mwaitenda ikiwa ni siku moja baada ya kunusurika kuuawa au kutekwa na watu wasiojulikana. Mwaitenda ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa CHADEMA na alikuwa ni Mgombea Ubunge Jimbo la Rungwe, Mbeya Uchaguzi wa Oktoba 2020 kupitia CHEDEMA.
Usiku wa 7 Julai 2023 akiwa anatokea uelekeo wa Mwenge kuelekea Goba, alivamiwa na watu 4 (wanaume 3 na mwanamke 1). Walimkimbiza na gari wakimpigia kelele asimame. Akifikiri huenda amegonga gari bila kujua, akakimbilia na karibu na Shule ya Makongo na kusimama.
Aliposimama wakashuka watu hao wakaanza kumpiga ngumi na mateke huku wakimfokea wakisema anajifanya anajua kusema sana juu ya Mkataba wa Bandari. Walinzi wa Shule ile waliokuwa mbali walipoanza kusongelea pale, watekaji wakamlazimisha Mwaitenda aingie kwenye gari. Muda huo tayari alikuwa mateka.
Aliendelea kuendesha gari huku wakimfuata na ndipo akakimbilia katika Kituo cha Polisi Kawe na kugonga Geti kwa gari. Alishuka haraka na kujisalimisha huku akiwa amenyoosha mikono juu. Wale watu wakegeuza gari na kukimbia.
Ndugu Watanzania! Jana tuliandika pia juu ya vitisho walivyopata wanasheria wanakosoa pia Mkataba wa Bandari ambao ni Dkt. Nshala na Boniface Mwabukusi! Mhe. Balozi Dkt. Willbrod Slaa alitishwa hadharani na kiongozi mmoja wa serikali baada ya Dkt. Slaa kuukosoa mkataba! Vitisho ni vingi sana na hatuwezi kuelezwa kila mtu anayetishiwa uhai wake.
Sisi Askofu Mwamakula tumesikitishwa sana na vitendo hivi vya kutaka kuteka, kuua na hata kunyamazisha watu waoikosoa serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Ufalme wa Dubai na Serikali ya Tanzania. Sisi tunatoa wito kwa Serikali kutoa kauli kuhusu vitendo hivi kwani wafanyao vitendo hivyo wanajinasibisha moja kwa moja na serikali. Kukaa kimya kwa Serikali katika matukio yaliyojitokeza sasa itachukuliwa kuwa ni Serikali inayoratibu na kufadhili vitendo vya kutisha na kuteka na kutaka kuua watu.
Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito pia kwa viongozi wote wa dini ili wakemea kwa nguvu vitendo hivyo kwani vinalenga katika kufinya haki na kuendelea kuondoa amani na utulivu katika taifa letu. Uhuru wa kutoa maoni ni haki ya kila raia wa nchi hii. Hakuna mtu au taasisi ye yote ikiwemo serikali aliye na haki ya kuzuia wengine wasitoe maoni yao katika nchi yao.
Tunaendelea kuonya na kutahadharisha kuwa ikiwa yeyote anayeikosoa Serikali ya Tanzania juu ya Mkataba wa Bandari atadhurika au hata kuuawa, basi watu wote waliowahi kutoa kauli hadharani kuwatisha wakosaoji, basi watu hao watawajibika sambamba na serikali endapo pia yenyewe haitajitenga na vitendo hivyo.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Uamsho Duniani.
Dar es Salaam, 8 Julai 2023; 21:11 pm.
Waione na kuisoma:
1. Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)
2. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
3. Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)
4. Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
5. Tanganyika Law Society (TLS)
6. Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania
7. Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania
8. Umoja wa Ulaya
9. Umoja wa Mataifa (UN)
10. Kituo cha Haki za Binadamu (LCHR)
11. Vyombo vyote vya Habari vya ndani na Nje
12. Sheikh Ponda Issa Ponda
13. Askofu William Mwamalanga
Kimeumanaa...😔😔duh aiseee