Ahsante kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Jamii 2024/24

Mambo ni mengi sana naona kuna vitu umefumbia macho kukemea mnaufyata kwa wafadhili, maisha ni kimya kimya tusubiri kizazi cha mashangazi siku za usoni
 
wanaona kama vile wao siyo watu wa kukutwa na msongo wa mawazo kwa kuwa hiyo ni dalili ya udhaifu na udhaifu ni ishara ya wanawake. SAIKOLOJIA. Hii ndiyo shida.....
Wanaume wabishi wameongezeka sana, wanapigwa vitasa na wake zao Ila hawatafuti msaada kwa sababu ni wabishi.

Fanya maarifa hao wanaume wasaidiwe
 
Hongera sana Dr Gwajima, watoto wa kiume nao ni muhimu sana kuwaweka katika mipango ya serikali, Kwa maana tunaona mmeegemea sana Kwa mtoto wa kike pekee.
 
Mambo ni mengi sana naona kuna vitu umefumbia macho kukemea mnaufyata kwa wafadhili, maisha ni kimya kimya tusubiri kizazi cha mashangazi siku za usoni
Naweza kusema tu kuwa, ufuatiliaji wako kuhusu kazi nafanya nadhani siyo wa Kila siku kwa Kila content. Ndiyo maana kuna kazi zangu zingine hukuzipata. Ingia google andika Dorothy Gwajima Shinyanga, kisha chagua video halafu tafuta video moja ina dakika 3.19 ya tarehe 5 Disemba 2022 kisha uje utoe maoni tafadhali. Shukrani kwa muda wako. Ukiona tatizo kinyume na sheria ukawa huna msaada nitumie sms tuunganishe nguvu kwenye 0765345777 nakala 0734124191, mpe na mwingine, kazi iendelee
 
Hongera sana Dr Gwajima, watoto wa kiume nao ni muhimu sana kuwaweka katika mipango ya serikali, Kwa maana tunaona mmeegemea sana Kwa mtoto wa kike pekee.
Ahsante Sana kwa maoni. Nami niruhusu nielimishe kwamba; ni uelewa tu, kwa kuwa, idara ya watoto inashughulika na watoto wote wa kike na kiume kupitia program ya malezi na makuzi, lakini madawati ya ulinzi wa watoto shule za msingi na Sekondari ni wote, kwenye madawati ya Jinsia na watoto Polisi ni wote, kwenye mabaraza ya watoto ni wote, mabaraza ya Wazee ni jinsia zote, kwenye program ya vijana balehe ni wote. Changamoto Iko kwa watu wazima wanaume ambao wakiwa kwenye migogoro ya mahusiano hawaji kwa aibu zao tu na siyo kwamba hawapokelewi. Mbona mimi nawapokea na nawaunganisha na mifumo? Na wanapata huduma?
 
Hivi kuna bunge linaendelea hapa dodoma? Npo hapahapa dodoma na sjui kama kuna mjadala wa bunge la budget....maana humo kila ktu tunamshukuru rais as if mpo mle kwa lengo kuwa wasemaji wa rais na kutetea ccm ndo maana watz weng hatuna muda wa kupoteza kuwaskiliza.
 
Hongera
 
Hongera Mhe. Gwajima.

Ila mbunge wa Iringa mjini Msambatavangu ana hoja ya msingi, asikilizwe..


View: https://youtu.be/AyJYIuH8O9Q?si=hfjntscyOLeFAW_O
 
Hongera Dkt. Gwajima D , sikujua kama wewe ni mdau hapa, nimefurahi kuona uzi wako hapa.

Kuna wimbi kubwa sana la watoto kulawitiana wenyewe kwa wenyewe na wengine na ndugu wa familia kwenye shule za msingi serekali, naomba iundwe tume ya kupita kwenye shule zote utashangaa.

Natolea mfano shule za Bagamoyo, kwa uchunguzi wangu mwaka huu pekee kumekuwa na visa zaidi ya vitano kwa shule tatu tofauti za hapa mjini.

Mbaya zaidi mambo haya yamekuwa yalimalizwa juu kwa juu lakini bado watoto wanabaki na adhari za kisaikolojia.
 
Hongera sana mama kwa uchapaji wako kazi mimi ni moja kati ya mashabiki wako wakubwa sana na ninakukubali sana mama kwa utendaji wako uliotukuka.kazi iendelee

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza nikupongeze mama kwa kazi nzuri unayoifanya kwenye hii wizara. Kiukweli hii wizara ina mtu.

Kuna huu mpango wa marekebisho ya tabia kwa watoto waliokinzana na sheria. Ni moja ya mipango mizuri sana inayosimamiwa na ofisi za ustawi wa jamii. Nikuombe mama ukae na wataalamu wako uone ni namna gani ya kuendeleza mpango huu uendelee kuwa na ufanisi kama ilivyokuwa huko nyuma. Mpango umewasaidia sana watoto ambao wanajihusisha na vitendo vya uhalifu, ni matumaini yangu ukiboreshwa, utaendelea kuwasaidia sasa wahalifu watoto ili wasiendelee na vitendo vya uhalifu.
 
You are the best da Dr Dorice
 
Mhe. Waziri, hauko sahihi katika jambo hili.

Lazima ujaribu kupunguza kuamini unayoyaamini ili uitendee haki nafasi yako. Nafasi yako kumbuka ni (Managerial Post siyo technical post). Kusikiliza na kusoma kuwe kwingi ili baadaye utoe majumuisho jumuishi.

Kiuhalisia, mwanaume ana hatua muhimu tatu katika kuishi kwake duniani:-
1. Ni hatua ambayo anakuwa ni Mkuu wa Kaya na neno lake ni Amri. Katika hatua hii, akinamama, hujitahidi kuvumilia na kukubali kuwa chini ya mwanaume. Hapa ndipo Wanawake hunyanyasika (Wizara yako kwa wakati huu Wanawake wanaitegemea sana). Ukweli wa mambo ni hapa mwanaume anakuwa ni hodari kitandani. Lakini kadri miaka inavyokwenda na kusema za ukweli mwanaume akawa goigoi kitandani, mwanamke huanza kuchukua hatamu kidogo kidogo kwa kuhakikisha anamrudisha chini mwanaume. Katika hatua hii, watoto bado ni wadogo.
2. Ni hatua ambayo mwanamke anakuwa ni Mkuu wa Kaya, mwanaume anapokea amri kutoka kwa mke wake. Hii hali huanza hasa baada ya Tezi dume kuchachamaa na mwanaume kutoweza kitandani. Hapa ndipo Mbunge wa Iringa jana (
View: https://www.youtube.com/watch?v=fcKfgmE-zkc) alikuwa anakueleza kuwa umewasahau wanaume katika budget yako. Hapa Mwanamke huwa analipiza kwa yale ya hatua ya kwanza. Jinsi inavyoanza, ni mwanamke anakuwa na commands nyingi kiasi mwanaume anakubali ili yaishe ili kupunguza kero. Watoto wanakuwa wamemaliza vyuo na wanaanza kujitegemea. Mzazi anakuwa amestaafu, pension imekata.
3. Ni hatua ambapo wote wawili (Mwanaume na Mwanamke) wanatawaliwa na watoto. Watoto ndiyo wanatoa amri na pengine wazazi wanaishi nao. Baada ya hapo ni kusubiri wakati wao.

Ukizijua hatua hizi tatu muhimu, utagundua kuwa Mwanaume ana uhitaji wa huduma za Wizara yako nyeti. Wengi huangalia

Nawasilisha
 
Mama wewe Wakutengee hata bilioni 100.Wizara yako Ndio inabeba afya ya jamii na sura yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…