Ahsante kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Jamii 2024/24

Ahsante kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Jamii 2024/24

Wasaalam.

Nawashukuru watanzania wote kwa ufuatiliaji wa wasilisho la bajeti ya wizara ya jamii 2024/25.

Namshukuru Mungu kwamba, mjadala mkubwa wakati wa uwasilishaji, ni ishara ya elimu kuifikia jamii kwa kina kuhusu kupambana na kutokomeza ukatili wa kijinsia na kudhibiti mmomonyoko wa maadili unaosababisha vitendo mbalimbali viovu.

Kuzinduliwa kwa mpango wa pili wa kutokomeza ukatili huu na mmomonyoko wa maadili kwa ujumla, utaipeleka ajenda hii hadi ngazi ya mtaa, kijiji, kata, halmashauri, vikao vya mabaraza ya madiwani, baraza la madiwani, baraza la maendeleo la wilaya na mkoa kwa kina zaidi. Na hapo ndiyo tutakuwa tumeungana wote kama taifa kwenye vita hivi kupitia ugatuaji madaraka na kuyasogeza karibu na jamii (DxD).

Tuendelee kushirikiana kwa upya kabisa, inawezekana kutunza maadili.

Elimu zaidi kuhusu bajeti yetu, Sera mpya ya jinsia na maendeleo ya wanawake na mpango mkakati wa pili wa MTAKUWWA tuliozindua 15 Mei, 2024: tukutane wiki ijayo Jamii Forums online na Twitter space pia na space zingine. Ratiba inakuja. Kisha kutoka online kwenda halmashauri kwa halmashauri.

Asubuhi njema🙏🏽

View attachment 2992948

Unaweza kuisoma yote hapa: Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka 2024/25
Mungu atusaidie tuimarike na kujikita zaidi kwenye msingi wa jamii au taifa bora ambao ni malezi bora katika familia. Tukiwa na malezi bora katika ngazi ya familia, hakika tutakuwa tumetatua matatizo mengi au yote yanayotukabili kwa sasa.

Ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla, hujengwa na familia zilizostawi kimalezi. Hongera kwa uwasilishaji mzuri Mhe Dorothy.
 
Hongera, Maendeleo ya jamii ni moja ya issue nyeti sana kwa Taifa linaloendelea kama Tanzania, kwa hiyo inahitaji mipango na mikakati ya hali ya juu sana, pia usisahau sera nzuri zinazolenga jamii moja kwa moja, Dawati la jinsia linafanya Kazi kubwa sana, ila kuna wachache ambao uelewa bado ni mdogo ambao wanaweka urasimu kwenye baadhi ya Mambo ya msingi. Mimi pia ni mdau na mtaalamu wa Social protection, nashauri pia kwenye wizara yako kungekua na kitengo hiki kwa ajili ya Training, Consultant na Research kwa ajili ya kua karibu na jamii yenyewe zaidi. Mungu akusimamie kwenye majukumu yako. 0743664260
 
Wizara inaandaa Sera, Miongozo, kanuni, nzuri zilizojitosheleza. Vikao vinanakaliwa na posho nzito wanalipana kwenye kuandaa miongozo. Changamoto inakuja kwenye utekelezaji ambapo ni watendaji wa ngazi ya chini (maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata).

Pongezi kwa kuajiri maafisa Maendeleo ya jamii ngazi ya kata. Lakini hawa watumishi hawana vitendea kazi vya kuwawezesha kwenda field (usafiri wa pikipiki). Kamati mbalimbali kama MTAKUWWA wajumbe hawapewi hata ya hela ya maji, hivyo kamati zinakosa uhai kwa sababu wajumbe muhimu hawezi kufika bila kuwezeshwa.

Rai yangu kamati zote za ngazi ya kata na kijiji ziwezeshwe ili kuleta matokeo tarajiwa
 
Back
Top Bottom