Mimi niliwauliza VRF imefutwa hii VRF ya laki 5 mliyoniwekea before 1st May ni ya nini?Unajua hao jamaa ni waajabu,wadau hapo juu walioenda Bod wanasema VRF kabla ya tamko la mama bado ipo,Sasa jiulize mbona wao walituingizia 15% hata sisi ambao tulikuwa tushaanza kulipa na sheria ikatukuta tena kwa mkataba wa zamani?Nionavyo mimi HESLB pale bila Raisi kuwapiga chini baadhi ya watendaji akili zao hazitawakaa sawa.Walishaambiwa waondoe VRF kwakuwa ni mzigo mzito hawaelewi.
Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
Wakanijibu nanukuu " Hiyo sio kwamba tumekuwekea bali umeilipa hadi kufikia 30th April. Kwahiyo kwenye marejesho yako tumetoa laki 5 ya VRF na laki 1 ya Administration fee jumla laki 6"
Kwenye slip yangu ilibaki 1.5 mill. Sasa walipopunguza ile laki 6, deni likapanda hadi 2.1 mill.
Nakaribisha maswali kama yapo.