Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Mimi niliwauliza VRF imefutwa hii VRF ya laki 5 mliyoniwekea before 1st May ni ya nini?
Wakanijibu nanukuu " Hiyo sio kwamba tumekuwekea bali umeilipa hadi kufikia 30th April. Kwahiyo kwenye marejesho yako tumetoa laki 5 ya VRF na laki 1 ya Administration fee jumla laki 6"
Kwenye slip yangu ilibaki 1.5 mill. Sasa walipopunguza ile laki 6, deni likapanda hadi 2.1 mill.
Nakaribisha maswali kama yapo.
 
Aisee waliweka mambo kinyume

Sent from my Nokia 2.4 using JamiiForums mobile app
 
Sasa mkuu kwangu nimekuta deni limepungua kutoka 6milioni Hadi 28500. Kwa maana ya kwamba salary slip inasoma loan helsb ni 28500. Inabidi niende niwatimbie bodi au nikaushee.
 
Sasa mkuu kwangu nimekuta deni limepungua kutoka 6milioni Hadi 28500. Kwa maana ya kwamba salary slip inasoma loan helsb ni 28500. Inabidi niende niwatimbie bodi au nikaushee.
Hiyo ya kwenye slip hawaitambui wao wana deni lao kule
 
Na mimi Nimejaribu mara tatu lakini najibiwa hivyohivyo. Kuhusu password na username pia sijaelewa naweka neno lolote au?
Username ni namba yako ya form 4 kwa format waliyoiweka kwenye mfano wao. Mf. S0144.0099.2005.

Password unaitengeneza wewe wakati unafanya registration kwa mara ya kwanza kwenye mfumo. Isipungue tarakimu au herufi sita.
 
Hiyo ya kwenye slip hawaitambui wao wana deni lao kule
Sasa mkuu Kama hawaitambui . Mfano mwezi huu mkopo ukiisha . Ntaendelea kukatwa ? Maana kwenye salary slip itakuwa mkopo umeisha.
 
Username ni namba yako ya form 4 kwa format waliyoiweka kwenye mfano wao. Mf. S0144.0099.2005.

Password unaitengeneza wewe wakati unafanya registration kwa mara ya kwanza kwenye mfumo. Isipungue tarakimu au herufi sita.
Asante sana kiongozi
 

Yaani mkuu wewe ndiyo umenivuruga kabisaa au labda bichwa langu chenga sasa kama walifanya hivi si deni lako lingepungua?!
 
Hapo hakun kulipa kizembe mpk watuajir wenyew watukate kwny mishahara yetu
 
Huyu mama aendelee hadi achoke mwenyewe. Yaan kufumba na kufumbua deni langu leo limebaki 1m!! Asante Mungu. Maana lilikua liende hadi 2024!!
Mkuu kwenye salary slip ndoo umekuta mabadiliko au umeenda ofisi za bodi
 
Na ukiandikiwa provisional balance ina maana gani mkuu
 
Wadau naomba mnijuze mana sijaelewa deni ninalodaiwa ni sh ngapi
 
Kuna bado ka wizi ambako watu hawajakaelewa kamefanyika kihuni sana na Bodi (HESLB) ukijaribu kuangalia Total charges amount hazifanani na je wametumia formula gani kuipata watueleze kwa mfano mm deni langu Disbursed Amount sio kubwa sana ila ile Total charges amount ni kubwa ukilinganisha na wengine wenye Disbursed Amount kubwa zaidi yangu. Pili nikiangalia statement ya zamani niliyoichukua 2016 VRF na Penalty ambazo ndizo tozo zilizokua zinatakiwa kuondolewa hazijapungua kwa kiasi kilichotakiwa ni sehemu tu. HESLB watolee ufafanuzi katika hili na tusikurupuke sana mpk watueleze hiyo total amount charges inachajiwa kwa percent gani kwa kila mnufaika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…