Ahsante Rais Samia, hatimaye HESLB wafuta VRF kwenye system yao

Sory me nataka kuapply mkopo ila naofia juu ya makato swali langu ni kwamba je kuna uwezekano wa kuilipa hela yote ya mkopo papo kwa papo???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuendelee kupeana update. Tupe ushuhuda kwako ikoje. Me nimetoka statement inasema it seems you have liquidate your loan.. cjui ndo nimemaliza?? Ila salary slip inasoma 1.6m
Hongera umemaliza deni lako, nenda Bodi wakupe Liquidation letter, alafu uipeleke kwa Afisa Utumishi wako asitishe makato hayo wasiendelee kukukata kwa msaada piga namba hii, 0225507910
 
Unamshukuru Samia badala ya kushukuru mifumo na taasisi zinazohusika?WTF!!!Tatizo la Watanzania wengi kuwa na akili fupi namna hii ni nini?Ni elimu hamna?Ni elimu duni?Ni syllabus zetu?
 
Wakuu misaada hapo salary inaonesha deni limebaki m 1 point 4 na mkopo alianza kupata mwaka wa pili semister ya pili mkopo kaanza kukatwa mwezi wa nne mwaka huu, kifupi salary slip na hapa bodi kuna tofauti kubwa
 
Wakuu misaada hapo salary inaonesha deni limebaki m 1 point 4 na mkopo alianza kupata mwaka wa pili semister ya pili mkopo kaanza kukatwa mwezi wa nne mwaka huu, kifupi salary slip na hapa bodi kuna tofauti kubwa View attachment 1845082
Alipoanza kukatwa mkopo mwezi wa NNE deni lilikuwa kiasi gani?
 
Alipoanza kukatwa mkopo mwezi wa NNE deni lilikuwa kiasi gani?
Deni alilotakiwa kulipa ni 7800000 lkn customer statement alopewa chuoni wakati anaondoka 2015 ilisoma m 11 akagundua kuwa mwaka 2010 aliaply chuo na akapata mkopo lkn hakwenda chuo hivyo akaenda chuo rasmi 2012 mwaka wa kwanza hakuwa na mkopo mwaka wa pili akaomba akapata tena asilimia kama 96 hivi
Akaenda bodi ili wamtolee deni la 2010 lisisome kwenye statement yake maana hiyo hela hakuchukua wala chuo hakwenda sijui ilikuwa inapigwa na nani.... Sasa mwezi wa nne mwaka huu bodi wamemdaka lkn salary slip deni limeonekana dogo anaona soo kwenda tena bodi kuogopa kuwatingisha...
 
Akachukue bank statement kuanzia semister ya pili mwaka wa pili hadi alipomaliza mwaka wa tatu kisha awafuate bodi. Hiyo hela ya nyuma 2010 kama waliingiza waliingiza kwenye account gani?
 
Akachukue bank statement kuanzia semister ya pili mwaka wa pili hadi alipomaliza mwaka wa tatu kisha awafuate bodi. Hiyo hela ya nyuma 2010 kama waliingiza waliingiza kwenye account gani?
Hiyo ya 2010 hakuwahi kukutana nayo kwenye account yake ila siku kamaliza chuo alipopewa statement ya deni la helsb chuoni ndio akaona habari hizo za 2010 yaani imeoneshwa 2010 alikua SJUT tawi la dar wakati ye kasoma saut mtwara 2012-2015

Statement alopewa chuoni Inaonesha hivi
SJUIT 2010/2011 SH......
SAUT 2014/2015 SH......

Alipoenda bodi wakasema hiyo ya SJUIT watatoa lakini hadi leo tunamwangalizia inawezekana limeungana na kufika m 10 badala ya m7 alizozitumia SAUT
 
Naomba kueleweshwa hii VAR ya 6% inaanzia mwaka huu wa fedha tu au inaondolewa kuanzia kipindi cha nyuma?
 
Hii website ya HESLB nayo imepumzishwa kutoa huduma?
Naambiwa "This site isn't working".
Na bado waombaji wapya hawajaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…