Ahukumiwa kuchapwa viboko 6 kwa kosa la ubakaji

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Mahakama ya mkoa Manyara imemhukumu John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ya kesi namba 73 ya mwaka 2021 imetolewa leo Septemba 26,2022 na Hakimu mkazi mkoa wa Manyara Mariam Rusewa.Hakimu Rusewa ameiambia mahakama hiyo kuwa Emmanuel alimbaka mwanafunzi wa darasa la nne (13) Septemba 10,2021 katika kijiji cha Malangi.

Kwa mujibu Kifungu cha 131 (2) cha sheria namba 16 kinaeleza kuwa, Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini; Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu ambapo hakimu ataamua ni viboko vingapi.

Chanzo: Mwanzo TV
 
Viboko 6 na miaka 30 jela wewe utachaguwa nini?
Kutoka na kosa la muhusika na umri aliotenda kosa, option ilikuwa na viboko. Naomba Mungu nisiingie katika haya majanga hapo sina cha kuchagua, kila siku naomba Mungu aniepushe na hayo machangamoto.
 
John Walter-Manyara
Mahakama ya mkoa Manyara imemhukumu John Emmanuel (18) mkazi wa kijiji cha Malangi wilayani Babati kuchapwa viboko sita (6) baada ya kukutwa na kosa la ubakaji.

Hukumu hiyo ya kesi namba 73 ya mwaka 2021 imetolewa leo Septemba 26,2022 na Hakimu mkazi mkoa wa Manyara Mariam Rusewa.

Hakimu Rusewa ameiambia mahakama hiyo kuwa Emmanuel alimbaka mwanafunzi wa darasa la nne (13) Septemba 10,2021 katika kijiji cha Malangi.

Kwa mujibu Kifungu cha 131 (2) cha sheria namba 16 kinaeleza kuwa, Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote, ubakaji unapofanywa na mvulana wa miaka kumi na nane au chini; Kama mvulana huyo amefanya ubakaji kwa mara ya kwanza, atapewa adhabu ya viboko tu ambapo hakimu ataamua ni viboko vingapi.
 
John Emmanuel (18) Mkazi wa Kijiji cha Malangi Babati Vijijini amekutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara imemhukumu kuchapwa viboko 6.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Mariam Lusewa ikibainishwa kuwa Sheria ya Hukumu hiyo inaeleza kama Mvulana mwenye umri wa miaka 18 au chini ya hapo ikiwa kosa lake ni la kwanza hukumu yake ni kuchapwa viboko.

Chanzo: Azam TV
 
Daah, kwahiyo angetimiza tu 19 ndio ingekuwa kwaheri, miaka 30 jela!
 
Kama alifanya kosa akiwa under age mbona hakupelekwa Juvenile court?

Sasa Panya road si ndio umri wao huo? Nao wawe treated under Juvenile?

Tunahitaji marekebisho ya sheria ziendane na wakati na uhalisia.
Ila vile viboko ukipigwa kimoja tu unaweza ukaomba ufungwe jela maisha, sasa fikiria 6 , acha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…