The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano, Machi 12, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Caroline Kiliwa baada ya mshtakiwa kukutwa na hatia.
Mshtakiwa huyo ambaye pia ni mganga wa kienyeji, alipewa adhabu hiyo katika kesi iliyokuwa inamkabili kwenye mahakama hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.
Awali akisoma kosa la mshtakiwa, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mashtaka Mkoa, Lupiana Mahenge alielezea mahakama kuwa Chifu alikutwa na nyara ya Serikali ambayo ni fisi akiwa hai akimfuga nyumbani kwake kinyume cha sheria.