AIBU CHUO KIKUU DAR ES SALAAM KUAJIRI WAHITIMU KISIWALIPE NA KUTOWAPA MIKATABA YA KAZI

AIBU CHUO KIKUU DAR ES SALAAM KUAJIRI WAHITIMU KISIWALIPE NA KUTOWAPA MIKATABA YA KAZI

gcmmedia

Member
Joined
Jul 19, 2024
Posts
34
Reaction score
75
Katika miaka ya hivi karibuni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikichukua wanafunzi wanaofanya vizuri kitaaluma wahitimu kubaki kusaidia shughuli za kitaaluma (TAs).

Cha kusikitisha vijana Hawa Chuo huwatekeza bila mikataba wala malipo. Kwa mfano, vijana wengi waliohitimu mwaka 2024 na kubakishwa kwa madhumuni hayo wanaendelea na kazi kwa miezi mitatu (3) sasa bila kupewa mikataba ya kazi wala kulipwa chochote.

Hivi, UDSM inafikiri wanaishije vijana Hawa? Mnawaingiza katika matatizo makubwa ya maisha na pia kutowalipa wala kuwapa mikataba ni ukiukwaji wa sheria ya Kazi na Mahusiano kazini.

UDSM Angalieni hili muwasaidie Hawa vijana
 
Dhuluma ya hali ya juu,vijana wana njaa kali na hawana pa kwenda inabidi wavumilie manyanyaso wakisubiri bahati nasibu ya ajira chini ya serikali ya kitapeli ya CCM
 
Kama hawajalipwa wanafanya nini huko??? Wamefungwa miguu?????,tuache uchonganishi!
Kuna ile ya kujipa imani kwamba 🥶🤨hapa ni uhakika wacha nivumilie Niombee pocket home! Maybe after six or one year naajiriwa ajira ya moja kwa moja

Kwahyo wanafanya kazi kwa bidii na utii, Ata bila malipo 🤔wakiamini fungu ni lao

Kuna sisi wengine hatukupata GPA kubwa 😅Kila kazi inayotoka inataka higher GPA tupo mtaani na hatukosi hela ya kula namshukuru Mungu kwa hilo
 
Halafu unategemea huyu TA asitoe desa kwa wanafunzi wake baada ya kutanguliziwa pesa.

Tunaipeleka wapi elimu yetu?

Hii sio sawa kama ni kweli,haiwezekani aliyefaulu vizuri na akaaminiwa kutufundishia watoto wetu afanywe kibarua.
 
Elimu barani Afrika ilishafeli kitambo sana.

Kilichobaki ni biashara tu.
 
Back
Top Bottom