Aibu kubwa ambayo inatia kinyaa kwa Watanzania

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Hapo awali CHADEMA kilionekana Chama ambacho sasa kimekuja kuwakwamua Watanzania toka katika tatizo kubwa lilikuwa linaiharibu nchi ya Tanzania.

Maana kilikuwa ndio mwiba kwa serikali ya CCM ambayo ilikuwa imechafuka na kuruhusu mianya ya ufisadi katika kila sekta. Palipotokea ufisadi wowote wao ndio walikuwa kidedea kuifichua na kuibana serikali. Na ilifikia kipindi wananchi wengi walihisi CCM inaenda kufa.

Mfano ni mikataba mibovu ya kuanzishwa mgodi wa Buzwagi ilipofichuliwa CHADEMA walipata umaarufu.

Dk Slaa kabla hajawa katibu mkuu alifichua madudu mengi kama Meremeta, EPA n.k na hii illikijengea CHADEMA heshima kubwa.

Mwaka 2015 baada ya kuondoka Dk. Slaa wamegeuka wao ndio wamekuwa mafisadi. Yaani hata bado kukanidhiwa dola wanakula na kufisadi michango ya wanachama na ruzuku bila aibu.

Kumbe hawa ni mafisadi hatari maana imeandikwa kama mtu hana uaminifu kwa kidogo; je, kikubwa atapata wapi uaminifu?

Kwa aibu hii iliyowakumba sijui Oktoba itakuwaje mbele za wananchi wakati wakiomba kura.
 
Ni kama inavyoaibika serikali ya Magufuli kwa kutafuna pesa za wastaafu.
Kipindi cha JK, wastaafu walilipwa mafao yao si zaidi ya miezi mitatu baada ya kustaafu. Ila tangu Magufuli aingie madarakani, wastaafu hulipwa mafao yao baada ya kuwa wamesota kwa kipindi cha miaka miwili na nusu hadi mitatu.
Wastaafu wanakufa kabla ya kupata mafao. Mwambieni Magufuli, hii in aibu kubwa kwake binafsi na serikali yake.
 
Nafikiri ipo wazi nje ya mada hapo.
 
Hivi unahabari upigaji mpya wa IpTL, diwans na ununuzi wa ndege?
 
Hii ndio akili ya kitanzania. Kulaumu udhaifu wa mlango katika tukio la wizi badala ya mwizi mwenyewe!!

Kashfa za wizi wa fedha za umma sasa analaumiwa CHADEMA kwa kushindwa kuzipigia kelele badala ya kuchukua hatua dhidi ya wezi wenyewe!!
Kwani ruzuku inayotafunwa na michango inayotafunwa sio mali ya umma?
 
Ni kama inavyoaibika serikali ya Magufuli kwa kutafuna pesa za wastaafu.
Kipindi cha JK, wastaafu walilipwa mafao yao si zaidi ya miezi mitatu baada ya kustaafu. Ila tangu Magufuli aingie madarakani, wastaafu hulipwa mafao yao baada ya kuwa wamesota kwa kipindi cha miaka miwili na nusu hadi mitatu.
Wastaafu wanakufa kabla ya kupata mafao. Mwambieni Magufuli, hii in aibu kubwa kwake binafsi na serikali yake.
Muda wa kufa unakuwa umewadia au unapingana na Mungu!
 
Mkubwa naheshimu mawazo yako.
Lakini nadhani njia Bora ya kuwahakikishia CHADEMA kuwa hawafai tena, tuweke mazingira sawa ya kampeini kwa vyama vyote, tume ya uchaguzi itende haki mshindi wa ndani ya box la kura ndio atangazwe sio yule wa maelekezo kutoka juu kwenye utukufu mshirika wa Mungu!
Huo ndio utakuwa msumari wa mwisho ktk jeneza la CHADEMA.
 
Kwani kuna mshindi nje ya box la kura huwa anatangazwa?
 
Mada yako nyingine kuihusu cdm, hapa NCCR na Ccm umezipotezea maana unajua hazina mvuto.
 
Wewe mbona unataka kunipangia mada za kuandika? Kama hazina mvuto achana nazo. Usiingilie uhuru wangu.
 
Sikupangii maana sina uwezo huo, ila nakuonyesha kuwa upo sehemu zisizo na mvuto, na wenye mvuto una nongwa nao.
Yaani Chadema wanamvuto? Na nina nongwa nao? Mimi wakati Dk Slaa katibu niliuza ng'ombe kwa ajili ya Chadema. Leo hii mmekuwa mafisadi.
 
Back
Top Bottom