Aibu kubwa Rais kutembea na 'chawa' wake na kuwalipa kutetea anapokosolewa anapofanya makosa

Aibu kubwa Rais kutembea na 'chawa' wake na kuwalipa kutetea anapokosolewa anapofanya makosa

Nashukuru mimi sio maskini napambana kila siku watoto wanasoma vizuri wana bima kubwa!wanadeka maisha matamu.
Wanaolalamika ni walalahoi
 
Baada ya chawa wa mama hatua inafutia itakuwa kunguni wa mama.
 
Kama kuna msamiati mpya umeibuliwa na awamu ya sita si mwingine bali ule wa chawa, yaani mijitu mizima na akili yake inayoishi na kusifika kwa kujipendekeza na kusifiana hata upuuzi.

Ajabu ya maajabu, mingi ya mijitu hii ambayo mingi ni CCM au chawa wake, inajisifia uchafu hadharani ili kumfurahisha rais. Rais naye anaonyesha wazi kupenda chawa jambo ambalo ni ushahidi tosha kuwa si msafi.

Mtu gani safi anaweza kuwakubali chawa hata kama ni chawa watu. Yaani mijitu imefilisika kiakili hadi inakubali kuitwa au kujiita chawa ilmradi itupiwe makombo na nafasi za upendeleo. Je, namna hii nchi yetu itafika wapi?

Samia aambwe ukweli kuwa chawa si viumbe wa kuvumiliwa wala kushangiliwa hata kama wanamuimbia mapambio uchwara na ya kinafiki.

Political hypocrisy of the highest level.
 
Nawakumbusheni tu kwamba chawa hunyonya damu na kueneza magonjwa. Chawa asipodhibitiwa mapema, humsababishia kifo hasini (host) wake. Chawa ni ngurukia/parasite.
Na mtu mwenye chawa hafai kwenye jamii ya watu waliostaarabika
 
Nawakumbusheni tu kwamba chawa hunyonya damu na kueneza magonjwa. Chawa asipodhibitiwa mapema, humsababishia kifo hasini (host) wake. Chawa ni ngurukia/parasite.
Ngurukia na hasini. Nimejifunza maneno mapya leo.

Mangurukia ya hasini (mama) yatamfyonza mpaka wamuache mtupu🤣.

Rasmi nabadili ID yangu, kuanzia sasa najiita Ngurukia.
 
Nawakumbusheni tu kwamba chawa hunyonya damu na kueneza magonjwa. Chawa asipodhibitiwa mapema, humsababishia kifo hasini (host) wake. Chawa ni ngurukia/parasite.
Na Chawa huwa hawakwambii kwamba unaelekea shimoni, wao hutumbukia na wewe shimoni.

Ukishafia huko shimoni Chawa hukuacha na kwenda kutafuta mtu aliye hai.

Mungu Ibariki Tanzania,
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Mwenyekiti wa hao chawa ni huyu anayejiita Lucas Mwashambwa? au kuna mwingine.
 
Back
Top Bottom