AIBU: Mchekeshaji Said Said aaibika baada ya kuzuiwa na walinzi wa Rais, kisa zawadi ya Cheni

Kutwa yuko kwenye shuguli za wasanii

Ova
 
Nchi hii hovyo sana. Wenye taaluma hawaitwi wakasikilizwa changamoto zao eti wanaitwa watu wamchekeshe rais. Aibu kubwa
 
Kwanza nitoe shukurani zangu za dhati kwa aliye juu, aibu hii iwapate machawa wote ili tuisome namba kwa umoja na wao wakiwemo.

Pili, niseme tu kwamba Tanzania ili uwe maarufu na influencer unatakiwa ufanye kitu hata kimoja tu, wanaume ndio wana kazi kubwa ila wanawake hata kutikisa matako tu tayari anakuwa msanii maarufu (naiona hadhi ya usanii unavyoshuka). Huyo Said Said ni mtu anayepanick (hawezi fanya kazi under pressure) akiwa maeneo mengi yenye watu mashuhuri (sijasema maarufu) hana content. Japo mimi sio chawa, lakini kumu_adress Rais wa nchi kwa ex wako, mara sijui kumuumiza kisa picha na Rais hiyo sio comedy bali ni kumfanya Rais aonekane kama mshangazi wako. Japo kuna sehemu alisema maamuzi ya kusamehewa (ex) yako kwa mama, lakini haimaanishi kwamba "mama" peke yake inaweza kuwa ishara ya mzazi kwasababu siku hizi hata malaya wa instagram na facebook wakiwa kwa mahawara zao wanaitwa mama.

Iko haja ya watu wa itifaki na serikali kupitia wizara ya elimu kwa ujumla ione namna wasanii wetu ni empty headed. Sio mbaya sasa wakajikita katika kujenga sanaa kama taasisi na sio hiki kinachofanyika. Angalau mtu ili awe msanii, basi apite vyo vya sanaa walau hata diploma. Na huko vyuoni wakufunzi wawe serious na kazi watakayopewa. Fikiria kama hawa ndio wasanii wetu wanaoalikwa kwenye hafla zenye hadhi ya nyota tatu kwendelea, si wanalitia aibu Taifa?
 
Ndio gharama ya kuwakumbatia chawa. Wanajificha hadi kwenye mavuzi... sasa wakati wa kujikuna miwasho mbele ya hadhara fedheha inaambatana nawe.🥸🥸😎
 
Nchi hii hovyo sana. Wenye taaluma hawaitwi wakasikilizwa changamoto zao eti wanaitwa watu wamchekeshe rais. Aibu kubwa
Bongo watu wanafosi uchekeshaji... waende wakajifunze kwa mR.Bean
 
Huyo mchekeshaji ni mpuuzi na hajifunzi mambo kwa kuangalia matukio. Siku hizi ni ngumu kupeana mkono na rais. Juzi kati kwenye mei mosi wali aliokuwa anawapa zawadi za ufanyakazi bora hawakumpa mkono kabisa. Ni masuala ya usalama hayo, utampaje rais kitu wakati huaminiki?
 
Tatizo linaanza n chura mwenyewe TU.hana nyota y simba.kua kiongozi.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Huyu dogo tangu alivyochekesha mbele ya Rais kwenye ile tuzo aliyoandaa ommy dimples nilikuwa na mashaka nae ila thanx God alimaliza salama,waandaji walitakiwa walitambue hilo,dogo alibahatisha mara ya kwanza kumweka mara ya pili ilikuwa ni kutake risk.Nachoelewa kiongozi mkuu wa nchi anapohudhuria event yoyote performance zote ziwe za kijeshi au za kiraia wahusika hufanya rehersal ya mda mrefu,na hakuna surprise pale.Kuruhusu upuuzi kama ule shows kuna watu hawafanyi kazi yao.
 
Mnamuonea tu watu wapo kwenye industry yao
 
Shida nini watz mbona wivu sana?
 
Yaah watu walikua wanamsubirickwa hamuu sana, alipiga picha akajisifu mno, akatudisi sana, mpaka akaweka bango aloo.

Watu waliweka kitu rohoni wakisubiri dogo ajae, hiyo juzi dogo kajaa watu wamemjaza.
 
Upo sahihi kabisa mkuu.

Mimi nilianza kukiona kinazingua kilivyoyatupa maneno baada ya kupiga picha na JK.

Lakini wao ndiyo wanaowaendekeza, wacha waendelee kuwadhalilisha.

Hao uliowataja wanaalikika kwasababu wanajua kuchekesha na wanajua kipi cha kuongea kwa hadhira ipi.
 
Dogo bado hajakomaa kiakili Raisi ni Kiongozi mkuu wa Nchi huwezi mletea mzaha kama ule lazma uweke Mpaka na kumtofautisha na mtu mwengine wa kawaida
Kwanini Rais aende ktk mediocre events ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…