Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Kuna mwanamke mmoja alitishia sana mtaa kutokana na uzuri wa sura na rangi ya mwili aliyonayo. Kati ya Predators waliovizia vizia nami nilikuwa mmoja wao
Nilipoona binti mwenyewe ni aina ya staki nataka nikamuweka chini na kumuomba anipatie jibu moja, akasema hanipendi. Nilipomuuliza sababu, akadai sina gari, sina nyumba, sina pesa, sina mvuto. Nilijilaumu tu kwa kuwa nilikuwa mjinga kipindi hicho. Nililia lia na mapenzi ilihali mapenzi ya siku hizi ni pesa mbele
Baada ya wiki kupita nilikuja kushangaa Mzee Madevu kashabutua, Mr Ugwadu kapiga, Mzabzab keshalima, Kettie Mashombe Shombe kaburuza. ie majina tajwa hapo juu si halisi, ni mfano ulio hai. Basi bhana, na mimi nikalengesha ki elfu thelathini changu, kikaliwa pasi na kupatiwa huduma, nikaombwa kuongeza dau yakanishinda. Hiyo ilikuwa Juni 2023
Ilivyofika mwezi Desemba 2023 uvumilivu ukanishinda tena, ile siku nilimuona na Shombe Shombe mmoja somewhere, niliishia kuumia moyo kwa kuwa nilimpenda sana, niliishia kumpandia Mnazi Mmoja usiku ule huku nikibubujukea na machozi makali sana yaliyoambatana na masabuni kutoka viganjani maake kwa namna alivyokuwa amevalia, duh! Na huo mtrako gejegeje😥. Binadamu tumeumbiwa kusahau, nikasahau
Mwezi uliopita (Juni) nikapata taarifa kuwa ameonekana mtaani, nikatamani nimuone kwa kuwa alikuwa bado ana nafasi ndani ya moyo wangu, awamu hii nikajisemea hata kama kila goti litapigwa mbele yake, mimi nitainamisha hata bichwa huku nikilamba unyayo wake, akisema ndio, naoa hapo hapo. Tena nilipanga niende nikiwa na Ostadhi na mkewe Ostadhati akiwa amebebelea mkeka na ubani
Ile nimefika tu nilishangaa kitu nilichokiona, nisingekiangalia sura ningeishia kukataa kuwa hakuwa yeye, kesho na hata kesho yake. Ee Mola, kiufupi ashakuwa moja, ngozi ya kuvutia ishachora ramani za rangi ya kuungua, dada hayo maacho😂. Nilijikuta nakimbia ovyo ovyo huku nikipepesuka almanusra niangukie sinia la mihogo la Mama Kalebo, machozi yalikuwa yakipaa huku na huko mithili ya mvua ya kisukuma, uso wote ulijaa mabonde mabonde ya mionekano, kama ungelinitizama ukiwa una njaa, ungeliona ni kama nauzunika sana. Kama ungeniona ukiwa umeshiba, ungeona kama nachekelea chekelea tu. Nilivyofika magetoni, nilivuta shuka nikalala kabisa usingizi
Juzi usiku kanitafuta kwa namba nyingine, baada ya salamu za hapa na pale kanieleza eti kati ya wanaume ambao walimtongoza, aliniona mie niko serious na yeye, hivyo anataka nimuoe. Niliishia kumuuliza kuwa anataka nimuoe au anaomba nimuoe, nikijiangalia mimi ni mkrishtu, kamoyo kangu kana chumba kimoja tu, naanzaje kukateketeza kachumba kangu ka makuti kwa mwanamke asiye sahihi. Nikachekelea sana hasa sauti ya mahaba aliyokuwa akiniongelesha, nikaona wacha niuwashe moto, ukawa ni mwendo wa vijembe na minyembe. Ndugu msomaji, hakuna mtu mwenye kisasi kikali cha maneno hapa dunia kama Melki Wamatukio. Baada ya kupretend kumkubalia, akaishia kunambia eti yuko na ujauzito anataka tushirikiane atoe nusu na mimi nitoe nusu (70,000) tukaangamize kiumbe cha Bwana cha mwanaume aliyekitupia ndani akiwa amemkaba mtoto wa watu shingo na kumkunja miguu yake mithili ya kiko bovu, muda huo mauno feni yaliyochanganyikana na nyonga radi yakilisukuma bao lililotengenezwa kwa mchanganyiko wa karanga na energy likitaradadi
Muda huu mnavyoniona hapa nilikuwa naye somewhere, nimeagiza bia la Kilimanjaro baridi halafu nikamwambia mhudumu alete fuko la kandoro la mia mbili amuwekee kwenye sahani la bati ashushie huku nikicheka sana cheko la kibosi, nimemshauri hiyo hela ya kuangamiza kiumbe kisicho na hatia, ni bora aitumie kama nauli ampeleke bibi ya mtoto mzigo ili alee
Nimalizie kwa kuwajulisha jambo, kuna kipindi (ni kama miezi mitatu imepita) nilipiga namba yake kwa bahati mbaya akapokea na kuniuliza nikusaidie nini hata bila salamu. Kumbe alipata mwanaume bhana, huyo mwanaume alionekana kufanya kazi TRA na alikuwa na kijigari fulani hivi kidogodogo, kumbe jamaa alimchezea mchezo. Jamaa aliingia TRA akatandika picha za kushanta akiwa na wahudumu wa mle ndani kisha kuazima kijigari gereji kwa rafiki yake, hii ilikuwa ni kwa lengo la kummotivate binti kwa kuwa binti alitaka mwanaume TRA mwenye gari, na huyu ndiye aliyeusukumia ndani mpaka kusababisha uhai ndani ya binti. Binti kuja kusanuka, kumbe mshikaji ni mishen town tu wakashindwana ndipo alipochukua uamuzi wa kupekenyua mafaili na kunidaka mimi akijua tutafaana
Nihitimishe:
Usiache mbachao kwa msala upitao
Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha
Mwisho wa ubaya ni aibu
Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani
Baniani mbaya kiatu chake ni dawa
Zimwi likujualo halikuli likakwisha
Mjini ukija bila gadi, utagawiwa wastani kwa idadi