Aibu/shida gani ulikutana nayo stendi au kwenye basi

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Nakumbuka mwaka jana 2020 , mwanzoni

Nlikuwa nmeenda kwenye project moja songea sasa wakati narudi sister akinipa kazi nirudi na beki tatu mmoja ambaye tayari sister alishamalizana na wazazi wake ilikuwa ni mimi tu kumchukua na kumfikisha mahali husika (DSM)

Sasa kufika Njombe pale saa 4 asubuhi , na ile winter tukashuka, kuchimba dawa nikampatia maelekezo namna ya kufanya na namna ya kurudi kwenye gari , akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa.

Ilitakiwa niwe makini mno maana alikuwa ni village girl.

Wakati tunarudi garini nikashaanga binti bado hajarejea na dakika zilikuwa zimeshaisha ikabidi nimface dereva kumuelekeza hali halisi uzuri akaelewa hivyo akavuta muda kidogo

Wakati huo mimi nmeshuka kumtafuta nikiwa na papara zangu , za kumtafuta yule binti.

Bwana bwana si nikakatiza kwenye ule ukoka wa maua pale Stendi mpya waliopita njombe watakuwa wanaelewa ,
Nikamsikia yule (mhudumu) dada wa pale stendi akiropoka kwa sauti kubwa.

Nanukuu

"Wewe kaka , nikutonze faini au??? Unapita kwenye Ukoka .. halafu mtu wa Mjini kabisaa " akamalizia na Msonyo

Daaah sasa wasafiri wote macho kwangu aibu iliyooje , kuepusha shari nikachepuka pembeni.

Nikiri tu akili yangu haikuwa sawa kwasababu ya yule binti...

Na kuhusu yule binti ,kumbe alichanganya magari badala ya kupanda basi namba 1 yeye akapanda namba 2

Maana yale mabasi ya Superfeo yanafanana fanana yakamchanganya binti wa watu😅😅

Tukawasiliana na uongozi na mambo yakawa sawa

ULIWAHI KUKUTANA NA DHAHAMA GANI STEND AU KWENYE BASI
ILIKUWAJE
 
...bonge la msonyo kwa nguvu kabisa, nikashuka kituo kinachofuata namba 11 mgongoni mpaka home
 
kuachwa na gari wakati wa kuchimba dawa sitasahau halafu mbaya zaidi umeenda mkoa ambao sio mwenyeji
 
Nimetoka hukohuko Songea-Mbeya. Jana yake usiku nilikuwa nimekula mbuzi na chachandu pale Serengeti. Bila shaka ni food poisoning ya ile chachandu. Tumbo la kuhara linakuja kwa spidi zote. Kufika sehemu mapoti wakasimamisha, nikashuka kuwaomba uelekeo wa msalani. Dele anapiga honi nachelewa, mi najisemea, "hawezi niacha kwa mapoti." Karatasi na majani. Siku ile niliwaheshimu sana wale mapoti.

Kurudi kwenye gari, siti ya nyuma! Uzuri watu nao wanakuwa na aibu, hawawezi kukukazia mimacho. Kufika makambako tena ni mbio msalani. Siku ile sikula kitu njia nzima.

BTW Flagyl haifungi choo. Ukipatwa na hali hiyo tumia loperamide, ndiyo inakata kuharisha.
 
ungepiga PEPSI baridi kali sana unagigida yote ndio kiboko ya tumbo la kuhara ghafra
 
Rry to be a GENTLEMAN sasa hapo kuna shida/aibu gani?!
 
Nilipanda daladala ilikua ipo level seat ikabidi nisimame kituo kilicho fata akapanda dada mmoja , yule dada akawa anajibada kwangu anaiwekea tak* nikirudi nyuma nae anakuja kila nikirudi nae anarud ikabidi nisimame nikiwa naangalia upande wa dirisha lakn bad ananigusa, Sasa sijui alidhamiria au na yeye alikua na stress zake tu hakujua anacho kfanya , daah mi ni rijal bana mwsho kichwa Cha chin kikaamka ikabidi niingize mkono mfukon kuibana .
ililibidi nipitilize kituo ninachotakiwa kushuka ili kichwa cha chini kipunguze hasira kwanza nikashukia kituo kinachofata,,,
 
Nimetoka hukohuko Songea-Mbeya. Jana yake usiku nilikuwa nimekula mbuzi na chachandu pale Serengeti. Bila shaka ni food poisoning ya ile chachandu. Tumbo la kuhara linakuja kwa spidi zote. Kufika sehemu mapoti wakasimamisha, nikashuka kuwaomba uelekeo wa msalani. Dele anapiga honi nachelewa, mi najisemea, "hawezi niacha kwa mapoti." Karatasi na majani. Siku ile niliwaheshimu sana wale mapoti.

Kurudi kwenye gari, siti ya nyuma! Uzuri watu nao wanakuwa na aibu, hawawezi kukukazia mimacho. Kufika makambako tena ni mbio msalani. Siku ile sikula kitu njia nzima.

BTW Flagyl haifungi choo. Ukipatwa na hali hiyo tumia loperamide, ndiyo inakata kuharisha.
Aiseee mkuu ulitumia hizo metro nini??
 
Aibu ya kwenye daladala stand halafu pembeni kuna watoto wakalii
ushajipa imani konda kakusahau mana ushatoka mlqngoni ushampita ile unapiga hatua 2 konda anabwatuka yowe
"hoya brother hujanipa nauri yangu"
😅😅😅
 
Nilipanda daladala ilikua ipo level seat ikabidi nisimame kituo kilicho fata akapanda dada mmoja , yule dada akawa anajibada kwangu anaiwekea tak* nikirudi nyuma nae anakuja kila nikirudi nae anarud ikabidi nisimame nikiwa naangalia upande wa dirisha lakn bad ananigusa, Sasa sijui alidhamiria au na yeye alikua na stress zake tu hakujua anacho kfanya , daah mi ni rijal bana mwsho kichwa Cha chin kikaamka ikabidi niingize mkono mfukon kuibana .
ililibidi nipitilize kituo ninachotakiwa kushuka ili kichwa cha chini kipunguze hasira kwanza nikashukia kituo kinachofata,,,
😅😅😅😅😅 ungemwomba na namb kabisaa
 
Kuomba namba kwa pis jiran kwa kuinongoneza, lakn yenyewe ikaropoka kwa sauti ''NIMESEMA SIKUPI NAMBA WE VIPI MBONA KINGANGANIZI''

Aloo abiria wote wakageuza macho kunitzama msumbufu mie naelazmisha namba
😅😅😅hatari mkuu
 
Back
Top Bottom