Aibu/shida gani ulikutana nayo stendi au kwenye basi

Aibu/shida gani ulikutana nayo stendi au kwenye basi

Jamaa yangu alikuwa mtu wa Pombe sana,na safari zake zote alikuwa anaamkia Bar,basi siku hiyo tumesafiri wote ilikuwa ndani ya Scandinavia Songea to Dar
Ile basi ameanza kuchanganya tu,jamaa kaomba akachimbe dawa.haijafika hata nusa saa,jamaa kasimama tena anataka akachimbe dawa,si konda akaanza kumzingua anamwambia dereva hakuna kusimama Dar tutaingia saa ngapi
Huwezi amini yule jamaa alitoa dudu akakojoa pale kwa dereva, kwenye kitanda,ukitegemea alikuwa miraba minne halafu mbabe.
Ilibidi akisimama tu akitaka kwenda kukojoa dereva yeye mwenyewe anasimamisha gari bila kuombwa
Watu wamedata[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Nakumbuka mwaka jana 2020 , mwanzoni

Nlikuwa nmeenda kwenye project moja songea sasa wakati narudi sister akinipa kazi nirudi na beki tatu mmoja ambaye tayari sister alishamalizana na wazazi wake ilikuwa ni mimi tu kumchukua na kumfikisha mahali husika (DSM)

Sasa kufika Njombe pale saa 4 asubuhi , na ile winter tukashuka, kuchimba dawa nikampatia maelekezo namna ya kufanya na namna ya kurudi kwenye gari , akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa.

Ilitakiwa niwe makini mno maana alikuwa ni village girl.

Wakati tunarudi garini nikashaanga binti bado hajarejea na dakika zilikuwa zimeshaisha ikabidi nimface dereva kumuelekeza hali halisi uzuri akaelewa hivyo akavuta muda kidogo

Wakati huo mimi nmeshuka kumtafuta nikiwa na papara zangu , za kumtafuta yule binti.

Bwana bwana si nikakatiza kwenye ule ukoka wa maua pale Stendi mpya waliopita njombe watakuwa wanaelewa ,
Nikamsikia yule (mhudumu) dada wa pale stendi akiropoka kwa sauti kubwa.

Nanukuu

"Wewe kaka , nikutonze faini au??? Unapita kwenye Ukoka .. halafu mtu wa Mjini kabisaa " akamalizia na Msonyo

Daaah sasa wasafiri wote macho kwangu aibu iliyooje , kuepusha shari nikachepuka pembeni.

Nikiri tu akili yangu haikuwa sawa kwasababu ya yule binti...

Na kuhusu yule binti ,kumbe alichanganya magari badala ya kupanda basi namba 1 yeye akapanda namba 2

Maana yale mabasi ya Superfeo yanafanana fanana yakamchanganya binti wa watu😅😅

Tukawasiliana na uongozi na mambo yakawa sawa





ULIWAHI KUKUTANA NA DHAHAMA GANI STEND AU KWENYE BASI
ILIKUWAJE
Niliwahi kukuta nduguze Le Mutuz (wagogo) wakilana stendi ya basi pale Kisutu....yaani tuliwashangaa sana, walishikwa na nyege mpaka wakashindwa kujizuia.
 
Mwaka huu mwanzoni nikiwa maguful terminal alfajiri nasubiri kusafiri kwa basi linaloondoka 12. Nilipata shida ya tumbo la kuendesha acid tumboni imechachamaa kutokana na vidonda vya tumbo, nikalipia huduma ya msalani, nilipoingia, lahaula nilikuta kuna vyumba vinne tu na kuna watu karibu hamsini wako foleni....nashukuru tu jamaa waliponiona hali niliyokuwa nayo maana nilikuwa nimeshalowa kwa jasho, waliniruhusu nikaingia haraka vinginevyo sijui nini kingetokea.
 
Huu mkasa ulinipata Nairobi mwaka ule Mkapa alipoidhinishwa kumrithi Mwinyi. Nimeshuka Nai kwenye saa kumi jioni nikitokea Kitale. Sikutaka kulala Nairobi siku hiyo, lengo ilikuwa niunganishe siku hiyo hiyo hadi Namanga.
Kuuliza machalii wa Nai wakanijuza kuwa niende stendi ya Lang'ata pale nitapata ufumbuzi. Nikaenda stendi, nikaona Guest house moja pale nikaingia kuuliza vyumba kama sitaweza kuondoka siku hiyo, angalau nipige kambi hapo hadi kesho yake. Hapo Guest, nikataka nifanye booking tu, jamaa wakagoma. Basi nikalipia chumba kisha nikaenda kufanya upelekezi.
Nikapata taarifa kuwa kuna basi moja la Taqwa linaondoka Nai kila siku jioni kuelekea Dar es salaam, ingawa hakukuwa na uhakika. Nikampata wakala akaniambia nilipie nauri, saa 12 jioni niodoke na Taqwa.
Baada ya kulipia nikarudi kugombana na wakikuyu wa Guest wanirudishie pesa hata nusu maana sitalala Nai. Wakagoma!. Nikachukua mzigo wangu nikaenda kumkabidhi wakala wa Taqwa. Muda wa kuondoka ukiwa zaidi ya saa moja, nikaona niende kupata nyama choma nakumwagilia moyo kabla ya safari.
Huko baa kulichangamka balaa, nikajuta kwa nini nisingelala Nai siku hiyo ya ijumaa. Nilitoka baa dakika kumi kabla ya safari, nikafanya hima niwahi kupanda basi langu kwani muda ni muafaka....Sasa bwana, ile nafika tu stendi nikakutana na basi la Taqwa linatoka, konda kumuuliza akaniambia wanaenda kujaza mafuta kisha safari ianze. Akaniambia kama nimeishakata tiketi nipande tu. Nikapanda nikakaa kwenye siti yangu, Basi lile kumbe lilikuwa la kwenda Mombasa na lilikuwa linaondoka saa 12 jioni pia. Du!! nikamtonya konda kuwa mimi naelekea Dar....Akasema tunarudi stendi ila hana hakika kama tutalikuta tena basi la Dar maana anajua wanavyojali muda na mwendo wao ni hatari.
Kurudi stendi Taqwa ya Dar liliishaondoka kitambo. Ikabidi usukwe mpango wa kulifukuza basi hadi tulikute, taxi za Nai haziruhisiwi kuruka viunga vya Nai hadi uwe na kibali, ikatafutwa taxi bubu binafsi wakataka kuifanya kazi hiyo kwa Dollar mia, nikawalipa tukaanza kulifukuza basi.... Hatukuweza kulipata hadi tulipolikuta Namanga Border post.
 
Back
Top Bottom