Aibu ya pombe

Aibu ya pombe

Heri ya krismasi na mwaka mpya,nilikua mnywaji mkubwa wa pombe ila baada ya kushauriwa na kuona inaniletea matatizo nikaamua niiache.

Juzi siku ya boxing day nikatoka na washkaji hadi mtaa wa mbali kidogo ila nafahamika nikasema nikumbushie kidogo pombe.

Matokeo yake nilikunywa kupitiliza nikagombana na kila mtu hata wale wakubwa nnaowaheshimu mbaya zaidi hata kurudi nyumbani nilishindwa nikalala kwenye pagala.Naona aibu kutoka hata nje kwa nilichokifanya.MSAADA Nijinsi gani naweza rejesha heshima yangu na kuiacha pombe kabisa?
Kunywa kistaarabu
 
Ende
Mkuu mimi ni mdau mzuri wa tungi. Kuna muda naicontrol kuna muda inanicontrol. Ila nishajua udhaifu wangu nikipiga pombe kali ndio shida ila hizi laini bia nakua poa kabsa.
Na nilichofanya siku hizi ni kuepuka kwenda bar kubwa. Napiga kijiweni kwangu au home basi. Imesaidia kiasi.

Karibu mkuu nimeamka nayo new year...

View attachment 1664602
Mimi hapana
 
Ukishindwa kupunguza ukaribu na marafiki zako walevi ni ngumu kuacha pombe.
 
Kawaida hiyo, hao watu uliowatukana watajua ni pombe tu
 
Asante juzi ndo nilikunywa,baada ya kukaa miaka 2,shida ni namna ya kuacha jumla
Hakuna kuacha, jifunze kunywa kistaarabu tu, basi. Km ni bia kunywa lkn si zadi ya 4,km ni nyagi au k vant piga kasichana alafu sepa kabisa, kwenye pombe hua hatuagi,ukitosheka unatoroka unawahi home, mengine yatajulikana kesho. Sasa ww unakunywa weeeeeeee hadi unasahau jina lako unaanza kuongea kingereza cha ugokoni na matusi juu hadi unagombana na mabosi wako iko siku utakunya kitandani ndiyo utajua pombe si chai.
 
Mkuu mimi ni mdau mzuri wa tungi. Kuna muda naicontrol kuna muda inanicontrol. Ila nishajua udhaifu wangu nikipiga pombe kali ndio shida ila hizi laini bia nakua poa kabsa.
Na nilichofanya siku hizi ni kuepuka kwenda bar kubwa. Napiga kijiweni kwangu au home basi. Imesaidia kiasi.

Karibu mkuu nimeamka nayo new year...

View attachment 1664602
Shukrani Sana mkuu [emoji16]
 
Tatizo Lililokukuta Limenikuta Pia Mimi Jumatutu,Nilikunywa Kwa Starehe Mapema Tu Nkarejea Home,Ila Home Wife Hayupo So Nkaona Nipo Bored,Nkatoka Nkakutana na Washkaji,Nikabwia-nikabwia Nikaamua Kurudi Home Mapema Tu,Kimbembe Kikaanzia Hapa,Ili Nifike Magetoni Kuna Ngazi Za Kupanda,Ndugu Yako Ngazi Nkawa Nazipanda Nakushuka,Yani Nkikaribia Ya Mwisho Nateleza Naanza Upya,Na Ni Hatua 5 Tu Nabakiza Kufikia Mlango Wangu,Basi Nkapanda Shuka Nkaona Isiwe Tabu,Nkauchapa Happy Happy,Sasa Kumbe Yupo Mtu Alikuwa Ananisoma na Ni Wa Hapa Hapa Nyumbani ya Pili Toka Kwangu,Akampigia Simu Mzee Mwenye Nyumba,Me Nimepanga Gorofani Ye Anaishi Kwa Chini Ndo Mzee Kuja Kunipa Msaada.
Nakuja Kushtuka Ni Asubuhi,Nimechafuka Sina Hali.

Nini Nimeamua Kufanya,Nimeamua Kumkabidhi Yesu Maisha Yangu Na Nizaliwe Upya.
Kudhalilika Huku Imetosha.

Hivyo Nikushauri Nawewe Mwenzangu,Pia Tuwe Na Mawasiliano Kuulizana Tulipofikia.
Vipi hadi leo hujagonga tungi
 
Heri ya krismasi na mwaka mpya,nilikua mnywaji mkubwa wa pombe ila baada ya kushauriwa na kuona inaniletea matatizo nikaamua niiache.

Juzi siku ya boxing day nikatoka na washkaji hadi mtaa wa mbali kidogo ila nafahamika nikasema nikumbushie kidogo pombe.

Matokeo yake nilikunywa kupitiliza nikagombana na kila mtu hata wale wakubwa nnaowaheshimu mbaya zaidi hata kurudi nyumbani nilishindwa nikalala kwenye pagala.Naona aibu kutoka hata nje kwa nilichokifanya.MSAADA Nijinsi gani naweza rejesha heshima yangu na kuiacha pombe kabisa?
Nyoa kipara
 
Back
Top Bottom