Aibu ya Propaganda: Baada ya kushindwa kudanganya kifo cha Netanyahu, Iran wamekuja na nyingine ya Marekani kuwalipa Dola Bilioni 6.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Taarifa zinazosambaa kwamba Marekani imekubali kuilipa Iran dola bilioni 6 ni propaganda za zinazorejelea tukio la zamani lililotokea Septemba 2023 kipindi Biden akiwa Rais wa Marekani.

Dola Bilioni 6 zilikuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na wafungwa, ambapo Marekani ilitoa ruhusa maalum ya vikwazo (sanctions waiver) kuruhusu takribani dola bilioni 6 za mapato ya Iran kuhamishwa kutoka Korea Kusini kwenda akaunti maalum nchini Qatar.

Hata hivyo, baada ya matukio ya Oktoba 2023 na uhusiano wa Iran na makundi kama Hamas, fedha hizo zilisimamishwa tena na hadi sasa (Aprili 2026) bado hazijapatikana kwa matumizi ya Iran.

Jaribio hili la kuwasilisha tukio la zamani kama ushindi mpya linaonyesha namna propaganda inavyoweza kujaribu kupotosha ukweli, lakini pia linafichua udhaifu wake pale ukweli unapowekwa wazi. Kwa wafuasi wa Iran, hili linabaki kuwa somo muhimu la kuchuja taarifa kabla ya kuziamini.

Hadi sasa hakuna chombo chochote cha Marekani kilichotoa tamko rasmi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…