Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Uchaguzi 2020 Aida Khenani (CHADEMA): Siwezi kuwasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini, mimi ni mbunge halali, ninasubiri kuapishwa tu

Mmewasikia wenyewe wanatamka kwa midomo yao, na sauti zao.

Majuzi walituwekea bandiko la uongo linalomuhusu huyo mdada.

Sasa ndio tumesikia maneno yake, sio ubabaishaji wa kutuwekea maneno ya uongo
 
Sasa huyo mmoja ndio atabadilisha picha halisi ya hilo Bunge?

Kumbe nafsi zinawsuta kuona mmebaki peke yenu!!
Ni bora kubaki peke yetu kuliko kuwa na genge la watukanaji. Mngependa huyu mbunge asusie kama kawaida yenu kawaaibisha vibaya. Huyu pamoja na wale viti maalum watakao teuliwa hakuna kupeleka 1M wala 500K kwa Mwenyekiti wa saccos..
 
Mmewasikia wenyewe wanatamka kwa midomo yao, na sauti zao.

Majuzi walituwekea bandiko la uongo linalomuhusu huyo mdada.

Sasa ndio tumesikia maneno yake, sio ubabaishaji wa kutuwekea maneno ya uongo
Wengi kwenye hilo genge la wahuni wanawivu balaa. Wanatamani hata kumyang'anya hiyo nafasi aisee. Kumbe ruzuku za Serikali mwapenda ee ha ha ha mmekula wa chuya.
 
Hana sehemu ya kuponea zaidi ya ubunge na CCM wamemchagua huyu wakijua hata elimu yake ni haba sana mwaka jana alikuwa form four resetter kwahiyo wanajua hatawasumbua.
Huyu dada hana CV hata ya mistari sita.
Yet chama makini kama Chadema wakampitisha kuwa mgombea wao
 
Wamfutie uanachama fasta asituletee ngonjera wakati huu wa maombolezo
Wala hafutiwi uanachama hata akifutiwa ataendelea kuwa mbunge sababu chama sio mliompigia kura amepigiwa kura na wananchi wenye vyama na wasio na vyama

Mumesahau mlifukuza wabunge kibao uanachama na waliendelea kuwa wabunge

Mumejaa roho mbaya mkishindwa nyie mnataka kila mtu awe kama nyie.

Kila mtu alikuwa akipambana na hali yake aliyeshinda kashinda aliyeshindwa kashindwa

Mama usiwe na hofu wala shaka umeshinda kihalali na tume imekutangaza hakutoi mtu kwenye ubunge wako.Uwe na amani kabisa .Hata ukiletewa barua ya kujitoa usihangaike kuijibu na hata wakikwambia umefukuzwa uanachama usiwajibu

Wewe sasa kazi yako ubunge full stop
 
Hana sehemu ya kuponea zaidi ya ubunge na CCM wamemchagua huyu wakijua hata elimu yake ni haba sana mwaka jana alikuwa form four resetter kwahiyo wanajua hatawasumbua.
Huyu dada hana CV hata ya mistari sita.
Mbowe ni form six division zero mbona humsemi umemkomalia mama wa watu
 
Kwa hiyo unaamini kuwa ataweza kuwakilisha kikamilifu kambi ya upinzani? Yeye na yule dada wa Mtwara? Na kama hataweza, hatakuwa na tofauti na wabunge wa Chama tawala ambao kazi yao kubwa ni kuwakilisha majimbo yao na sio kuisimamia serikali. Binafsi, sioni namna ambayo Chadema watakubali awawakilishe
Kwa nini waliwateua kugombea ubunge kama waliona hawafai na hawana uwezo? Wana uwezo mkubwa ndio maana hao akina mama wameshinda acheni wivu

Kinawauma mkiona pesa watakazopata bungeni roho zinawauma hadi basi
 
Aidah amechaguliwa na wananchi na Aidah ataenda na John Pombe Magufuli
😉😉😉😉😉
 
mbowe alika kumzibia ridhiki dada wawatu sasa naye kachaluka sijui itakuwaje,maana kina mbowe hawatambui matokeo yoyote!! Labda wamfute uanachama!! Cdm buana😂😂😂😂😂😂
Wakishinda wao matokeo hali wakishinda wengine sio halali
Nakumbuka 2015 UCHAGUZI wa Zazibar CUF wengi walishinda kura za ubunge na baraqza la wawakilishi.Lakini Maalim SEIF akashindwa.Aliposhindwa ikatangazwa kuwa uchaguzi wote batili na seif akagomesha asiweko mtu kupigiwa kura uchaguzi wa marudio.Wabunge wale na wawakilishi wote wakapoteza nafasi zao!!!! Kisa yeye kashindwa

Uchaguzi kila mtu anapigana kivyake haya mambo ya mtu kushindwa na kutaka wengine nao waachie ngazi sio sahihi

Huyo mama abaki na msimamo huo huo
 
Ivi Mbowe angeshinda Hai angejiuzulu kwa sababu ya wenzake!!.

Ama angesema ngoja akapambanie tumehuru bungeni.
 
Hana sehemu ya kuponea zaidi ya ubunge na CCM wamemchagua huyu wakijua hata elimu yake ni haba sana mwaka jana alikuwa form four resetter kwahiyo wanajua hatawasumbua.
Huyu dada hana CV hata ya mistari sita.

Tutakapoweza kutofautisha Kati ya elimu ya mkoloni ya kupata makaratasi tunayoyaita vyeti na elimu yetu isiyo rasmi, elimu ya mazingira, ujuzi na uzoefu; na tutakapoweza kuacha kuwadharau wasio na makaratasi na kutumia elimu ya makaratasi kuboresha ujuzi wa asili ya mtanzania na matumizi sahihi ya rasilimali na desturi zilizo bora tutaweza kuleta maendeleo makubwa zaidi kwenye jamii zetu na kupiga hatua kubwa sana katika kuleta maendeleo ya nchi yetu

Go go Aidah......Wachana na wale wenye madigrii kwenye vyeti bila uzalendo mioyoni wanaoishia kutumika kama vibaraka kwa nchi yetu
 
Huyo dada kwangu akienda bungeni ni sawa, na akiamua kusimamia msimamo wa chama ni sawa. Cha muhimu akiwa bungeni asigeuzwe kondoo wa kutii mambo ya ccm. Tena kuna uwezekano wa kuwashinda kwa hoja hao viazi wengi wa ccm.
Vipi hujaenda barabarani kama ambavyo mlikuwa mnaambiwa na kibaraka Lissu? Yaani wanasaccos ni wabaya sana yaani mmemwacha Lissu pekee yake kweli?
 
Tutakapoweza kutofautisha Kati ya elimu ya mkoloni ya kupata makaratasi tunayoyaita vyeti na elimu yetu isiyo rasmi, elimu ya mazingira, ujuzi na uzoefu; na tutakapoweza kuacha kuwadharau wasio na makaratasi na kutumia elimu ya makaratasi kuboresha ujuzi wa asili ya mtanzania na matumizi sahihi ya rasilimali na desturi zilizo bora tutaweza kuleta maendeleo makubwa zaidi kwenye jamii zetu na kupiga hatua kubwa sana katika kuleta maendeleo ya nchi yetu

Go go Aidah......Wachana na wale wenye madigrii kwenye vyeti bila uzalendo mioyoni wanaoishia kutumika kama vibaraka kwa nchi yetu
Good comment ever!. Asante sana dada kwa upeo mkubwa ulionao!
 
Chama kiliniamini kikarudisha mamlaka kwa wananchi na wananchi wamenipa mamlaka. Kama niliapa Chadema siwezi isaliti hali kadhalika siwezi wasaliti wananchi wa Nkasi Kaskazini.

Naomba nitoe msimamo wangu, mimi Aida nimechaguliwa kwa mujibu wa sheria na ni mbunge halali wa Nkasi Kaskazini, ninasubiri kuapishwa na hakuna jambo jingine, sina mabadiliko mengine.

Pia soma> Aida Khenan: Demokrasia ni muhimu kuliko ushindi wangu. Nipo tayari kuungana na wenzangu kwa maamuzi yoyote

Patamu apo............kama uchaguzi huu ni batili basi na huyu chama chake kisimtambue
 
Vipi hujaenda barabarani kama ambavyo mlikuwa mnaambiwa na kibaraka Lissu? Yaani wanasaccos ni wabaya sana yaani mmemwacha Lissu pekee yake kweli?

Barabarani tupo kila siku. Kwa taarifa yako sisi wengine tulioko mitandaoni tuna madhara kuliko hata kuingia barabarani. Kuingia barabarani Ni njia moja wapo kati ya njia nyingi za kukomesha uhuni wa kitoto.
 
Dada anajielewa sana kuliko yule mbunge wa zamani wa Kawe.
 
Back
Top Bottom