Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Inawezekana na wapinzani wamempigia rais
Unaelewa kweli kilichoko hapa?
Kura za Ubunge CCM Ni 35,000+ na anaefuatia ni 11,000, jumla na wengine ni Kama 50,000+ hivi waliopiga kura za Ubunge.

Sasa kichekesho Magu ana kura 165,000+ za Urais, Ina maana Kuna watu 115,000+ wamepiga kura za Urais tu?
 
Kawe Rashidi amepewa kura 194,000 halafu Magufuli kura 305,000![emoji276]
FB_IMG_16040264088975506.jpg


Na huku je?
 
Hatimae chama pendwa cha CHADEMA kimepata mbunge mmoja mpaka sasa aitwae Aidah Kenani wa Nkasi kaskazini baada ya kumuangusha Bwana Ally Keissy, mbunge machachari kwa kutetea hata upuuzi wa chama. Hongera sana kwa mkurugenzi ambae hata amethubutu kumtamka mpinzani.

=====

Ally Mohamed Keissy(CCM) amepata kura 19,972, Aida Khenan wa CHADEMA kura 21,226 tofauti ni kura 1,254 mshindi ni Aida Khenan jimbo la Nkasi Kaskazini.

Missana Kwangula, msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa ndiye aliyetangaza matokeo haya usiku wa leo.
NASIKIA HUYU MKURUGENZI ALITAMKA WAZI KWAMBA LIWALO NA LIWE. INASEMEKANA HUYU NDUGU AMETOKEA KUWA MCHA MUNGU KWELI KWELI TOFAUTI NA KIPINDI ANACHAGULIWA NA KUAPISHWA. NA ALIKUWEPO WAKATI MZEE ALIWAAMBIA KWAMBA "NIKULIPE MSHAHARA, NIKUPE NYUMBA, GARI, DEREVA HALAFU ETI UMTANGAZE MPINZANI KASHINDA".
HUYU NI MKURUGENZI TOFAUTI NA YULE WA MTWARA VIJIJINI ALIYEPEWA AMRI TOKA JUU KWAMBA ASITHUBUTU KUMTANGAZA HAWA MAANA ALIMUUDHI MZEE KWENYE KOOSHO KIASI CHA MZEE KIJIAPIZA KUMCHARAZA BAKORA HAWA NA SHANGAZI ZAKE.
 
Unaelewa kweli kilichoko hapa?
Kura za Ubunge CCM Ni 35,000+ na anaefuatia ni 11,000, jumla na wengine ni Kama 50,000+ hivi waliopiga kura za Ubunge.

Sasa kichekesho Magu ana kura 165,000+ za Urais, Ina maana Kuna watu 115,000+ wamepiga kura za Urais tu?
Hawezi kuelewa lkn muda mchache ujao wataelewa maana dikteta hana rafiki.
 
Hivi kweli kesho, Jumamosi na Jumapili watu wataingia nyumba za Ibada kumsifu na kumshukuru Mungu kwa Baraka zake zakushinda uchaguzi uliojaa dhuluma, uvunjifu wa haki, ubabe wa kujipindishia sheria na ubatili wa matokeo ? Nasi tutashangilia kwa kusema Takbir au Bwana Asifiwe?
 
Mwenzao Aida khenan ameshinda ubunge kwenye wakati mgumu sana, si Mbowe wala Lissu aliyeenda kumuombea kura huko Nkasi , acha ale maisha tena bila makato ya kuchangia chama.

Ni aibu kubwa sana kwa Mbowe ,Msigwa ,Lema ,Mdee, Sugu kuzidiwa mbinu za medani katika kulinda kura na mtoto mdogo tena mwanamke Aida !
 
Mwenzao Aida khenan ameshinda ubunge kwenye wakati mgumu sana, si Mbowe wala Lissu aliyeenda kumuombea kura huko Nkasi , acha ale maisha tena bila makato ya kuchangia chama....
Tulisema hapa kwamba kufungiwa kwa mitandao ya kijamii kutaleta madhara hadi kwa wanachama watiifu huko Greenland.
Onasasa unekurupuka toka lumumba, unakuja na habari mbayo tayari muhusika amesha itolea tamko...😂😂
 
Malalamiko ya kura feki ni kawe tu mbona mbowe na Lema hawajalalamika
Kura feki NI nchi nzima. Ukiona Hadi kwenye ngome ya CCM Ruvuma Jimbo la mbinga Mjini kata ya mpepai mgombea wa CCM alikataliwa tangu mwanzo.
Wananchi wakaamua kupiga kura ya wazi kwa kusema hadharani kwenye kampeni kuwa watampa Fulani. Ajabu matokeo yakaonesha CCM ameshinda ndipo kila MTU akaingia ndani mwake akachukua panga/rungu/nyengo wakazingira kituo Cha kuhesabia kura na kuamuru mgombea wao wa act aliyeshika NAFASI ya 3 stangazwe kinyume na hapo watagawana majengo. Na ikawa hivyo akatangazwa.Mbinga Mjini watu wamekamatwa na kura zilizopigwa tayari,kigoma,kwanza,ubungo,kagera n.k utapingaje kwamba hazikuwepo?
 
Huyu Dada bora awaachie CCM hilo Jimbo, akatae huo uteuzi

Itakuwa vizuri aungane na wabunge wa Chama chake waliozulumiwa haki zao
Chadema wanahitaji hiyo ruzuku yake na kumbe akina Halima, Bulaya, etc watakuwepo kupitia viti maalum.
 
Ni haki yake, mimi ningemshauri aende bungeni akachukue posho na mishahara isaidie kuimarisha chama cahake.
Naimani atakuwa na familia na malengo yake binafsi pia. Tena ni single mother na watoto wakusomesha.
 
Hizo kauli zenu za vitisho ndizo zilizowafanya watanzania waamue kutowachagua.
Walie na kusaga meno kwa lipi?
Nyie sifieni ,shangilieni hiyo dhulma ya kuiba kura Ila yakikukuta hamna wa kukutetea au kukusemea...kamaliza upinzani Sasa ataanza kuwashughulikia nyie ccm ndani kwa ndani.
 
Back
Top Bottom