Kuhusu Q-net binafsi ninaweza kusema haya....
-Ni wale wale, pyramid scheme fulani, wachache sana (wa mwanzo) wanaweza kuvuna kwa kutumia migongo ya wengine wengi (wanaofuata nyuma).
-Ukitaka uanze kuvuna chochote (kurudisha mtaji wako) kupitia Qnet inabidi ukubali kwanza kutoa (kulizwa!) milioni 5 zako kwanza na kisha uhakikishe watu wengine zaidi ya 20 hivi wanajiunga katika mnyororo unaohusiana na wewe. Sasa kimbembe sio tu kuzipata hizo milioni 5 za kujiunga, kimbembe kikubwa zaidi ni mtiti wa kushawishi watu wengine wajiunge. Unaweza kuwa kichaa, ukakonda, ukadhoofu, ukachoka au kuchukiwa hadi na ndugu, marafiki au majirani zako.
-Tofauti kubwa ya mfumo wa Qnet na network marketing zingine ni kuwa, mnyororo wa kuunganisha watu huwa ni watu wawili wawili (Binary). Muundo huo una faida na hasara pia. Mambo mengine ni yale yale tu na tofauti zilizopo hazina msingi.
-Tatizo kubwa lililopo katika biashara ya Qnet ni gharama za mwanzo za kujiunga kuwa kubwa sana (Kwa sasa ambazo ni wastani wa milioni 5) huku ukizugwa kuwa unanunua bidhaa au huduma, kitu ambacho huenda 99% ya watu waliopo Qnet hapa Tz hakikuwa kivutio chao cha awali cha kupenda kujiunga.
-Makosa makubwa yanayofanywa na member wa Qnet kiasi cha kuonekana ni biashara ya kitapeli ni kitendo chao cha kuwapa matumaini hewa ya uongo na kweli kwa kuwaaminisha watu wanaowashawishi kujiunga kuwa watakuwa mabilionea chap chap kitu ambacho sio ukweli. Na hapo huwa wanawaaminisha kuwa biashara zingine zote au kazi za kuajiriwa ni kupoteza muda na hazina manufaa. Wakati kiuhalisia ni rahisi kupiga pesa kwa kubet kuliko kuvuna hata senti tano kwa Qnet.
-Ukweli mchungu kuhusu Qnet ni kuwa pesa yoyote utakayovuna kupitia Qnet ni matokeo ya mtu mwingine kulizwa haswaa. Hivyo kama utatajirika kwa Qnet basi ujue wazi kabisa hayo ni matokeo yalitokana na kutengeneza ufukara kwa member wengine wa Qnet.
-Kuhusu salamu yao ya Good morning! Binafsi sioni tatizo. Ni kitu cha kawaida na kina maana nzuri. Kivipi? Kwanza ni utambulisho wao, hivyo wanaweza kufahamiana na kuwafahamisha wengine wao ni akina nani. Pili, kwa kuwa wanafanya biashara kutumia online platforms na wapo dunia nzima, tofauti za masaa baina ya nchi na nchi ni kubwa, hivyo kuwa na salamu inayofanana wanapowasiliana regardless ya majira ya nchi yako ni jambo zuri. Mwisho, Good morning! maana yake ni kumekucha! Tupo macho, hatuja lala, ndio kwanza tumeamka, bado mapema sana, tuna nguvu mpya, tuanze sasa kazi nk.
Hivyo hiyo ni motivation greeting kwa watu wengi duniani wanaokuwa busy katika mishe mishe zao.
Yote kwa yote simshauri mtu yoyote kujiunga katika hii biashara ya Qnet, maana uwezekano wa kulizwa ni zaidi ya 90% na kwa wale wachache waliofanikiwa au watakaofanikiwa kupitia hii biashara basi walipigika na kupambana mnoo kwa muda mrefu (ikiwemo kutumia uongo au ujanja mwingi wa maneno) pamoja na bahati kuwaangukia upande wao.