Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mabadiliko ni qnet?😂😂😂.Mjinga ni yule ambaye ubongo wake hautaki kuendana na mabadiliko ! poor on you
Sent using Jamii Forums mobile app
Mabadiliko ni qnet?[emoji23][emoji23][emoji23].
Akili huna. Tafuta mume akutunze huku anakupiga mjeledi taratibu. Qnet haitakusaidia.Unajua ukiwa mfuska huwezi kuelewa maada kama hizi zikiwekwa mezani !
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha kujibu kwa jazba naskia nyinyi matajiri wa Qnet hamtakiwi kuwa na jazba but acheni kuwatapeli baadhi ya Watanzania kwa uelewa wao ambao may be n mdogo kuhusu hizi issue za Qnet et all,ndiyo ninaamini katika matikiti,machungwa,mananasi,pilipili hoho na pilipili za mwendo kasi,mihogo,mahindi,na vitunguu maji tena muda huu vinalipa kweli kweli hivi vitunguu maji,acheni kuumiza watu mkuu.Hizo ndo akili za ngamia ! wewe una amini katika kilimo cha matikiti maji kuwa utatoboa basi komaa mkuu siku moja utanunua fuso ucjali
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dawa ya mswaki shilling ngapi? Hata wakina MO wenye mkwanja mrefu hawawezi kuingizwa kwenye chaka hilo. Dah![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nilipelekwaga office za Forever aisee wanakutamanisha balaa ila bidhaa hawakwambii bei zake hadi ujiunge nao kadri maelezo alivo zidi kuyatoa naona huu uongo wanamsifia kila yule dada Blandina...ile muda nataka kuondka nikamvuta pembeni yule jamaa nikamuomba nauli kama alistuka fulani akaongea huku anajikaganyag kanyaga tu mara sitembeagi na cash sijui nini blah blah kibao nikaona hapa hamna kitu... kuja kuulza kwa wanaofahamu ndo naambiwa ungemuuzia nani dawa ya mswaki elf 50?
Nikasema duh kweli ukiitwa kwenye fursa jua wewe ndo fursa
Akili huna. Tafuta mume akutunze huku anakupiga mjeledi taratibu. Qnet haitakusaidia.
Yaweza kuwa kweli,waliojiunga kuwapata chambo wengine hakuna kikibwa ,wanasuffer sana mkuu..Amejenga nyumba mkuu within this 3 yrs ! na huko Malaysia anaenda kwa pesa zake zinazotokana na juhudi zake za network marketing.Nawafahamu hao marafiki zangu miaka mitatu ya nyuma walikuwa ktk hatua gani kimaisha na sahizi wapo wapi, mmoja kati yao kapiga hela ndefu na mwaka jana kawekeza ktk kikimo chha mihogo eka 120 huko Tanga maeneo ya Mkata, kikubwa hapa naona physical progress siyo blabla ! na wanajitoa kwelikweli kufanya kazi across the whole country,upo hapo nyonyo
Sent using Jamii Forums mobile app
Qnet haoMimi nilupelekwa saa 10 watu wanasalimiana good morning nikaona hapa matapeli nikawatoroka
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa jamaa wa AIM GLOBAL mimi nilitarajia katika kipindi hiki cha janga la covid-19 wangenunua hata ventilators mbili tu waziweke mloganzila utajiri wao upo kwenye maigizo ya kupiga picha na magari ya watu na kupost ili kutumika kama chambo kwa wengine ili wavutike na kununua bidhaa zao ambazo kimsingi ndio chanzo chao cha mapato.Hahahaha hawa wajinga walini block kwenye whatsap
Eti karibu AIM BLOGAL ALLIANCE, yani ile naanza ku type kua ahsante nikastukizwa attachment imetumwa kucheki ni jamaa mmoja kanyuka suti kali halafu kashikilia mi noti ya misimba pembeni kuna gari kali
Kwa chini akaweka na ujumbe naitwa mr flani ni mshiriki wa global alliance karibu kwa maswali ya namna ya kufanya ili upate pesa
Moyoni Nikajisemea "aah inamaana akili yake imeridhika kabisa na hicho kipicha kua kinatosha kua ushahidi ili mimi niwaamini?"
Hivi nini kinachowafanya wahisi watu wote wenye mionekano kama yao ni watu wenye mafanikio ya kimaisha kwa kumilika pesa nyingi? Na kwanini wamejijengea dhana potofu kwamba muonekano wa nje wa mtu husadifu hali ya kimaisha yake?
Kwanini vazi la suti wamelipa kipaumbele sana katika kuji brand ili kuwaaminisha watu kua wako serious?
Ni mfano wa bongo movies wanavyo act kua jambazi lazima awe na sura mbaya halafu avae mikoti mirefu myeusi pamoja na glass za tinted wakati ili mradi tu kuwashawishinwatu kua jamaa ni jambazi, hapo washajijengea dhana kua akikaa mshakaji ambaye ni handsome halafu havai makoti na miwani watazamaji wanaweza kua bored wasivutiwe kua haiwezekani jambazi akawa huyo mtu wakati kila ukimuangalia huonekana innocent
Lakini ukiangalia movies za hollwood utakuta sekta ya jambazi anakaa mtu yeyote yule na anafit na movie bado ipo katika ubora wake ule ule ambao hata mtazamaji hapepesi macho pembeni ya runinga.
Tunawaona matajiri wakina billget jeffbozes, jack ma na huyu mmiliki wa facebook ambaye hadi watu walimsema kwamba anarudia rudia kuvaa shati moja kila siku yenye rangi ya kijivu. Hao wote matajiri huwezi ukakuta wamepiga picha wameshika hela kama swaga, picha ambayo unaweza bahatika kuiona unakuta ni kumbukumbu siku ambayo alitoa mabilioni ya pesa kuwasaidia wasiojiweza.
Sasa hawa wa global alliance wanadai kua campuni hiyo ilianzishwa na malegend wawili huko ufilipino ambao ni mabilionea wa kidunia, lakini huji kuwakuta wakioneaha picha za hao matajiri kuwasaidia masikini wasio jiweza wakati sera ya campuni yao ni kusaidia vijana
Niliwajibu hovyo sana, halafu kinachokera ni usumbufu wao.Mkuu hawa jamaa wa AIM GLOBAL mimi nilitarajia katika kipindi hiki cha janga la covid-19 wangenunua hata ventilators mbili tu waziweke mloganzila utajiri wao upo kwenye maigizo ya kupiga picha na magari ya watu na kupost ili kutumika kama chambo kwa wengine ili wavutike na kununua bidhaa zao ambazo kimsingi ndio chanzo chao cha mapato.
Mkuu ulimuliza maswali makini sana! Hongera kwa hilo.Kwa sababu kama mtu ana miliki 175M anashindwa kukukopesha 500k ili nawe uanze kufanya hiyo biashara ,basi ujue hiyo biashara ina mlolongo mrefu sana na inachukua muda sana kupata mafanikio.Ingelikuwa inaleta returns kwa haraka basi wangekua wanakopesha kama kweli lengo lao ni kudaidia vijana kuondokana na hali za kiuchumi,zaidi ya hapo Inaonekana watu ndo mtaji kwao!.Jamaa akaanza kunipa dondoo
Mi ni mshindi wa pili kwa ukanda huu wa afrika mashariki nimevuna milion 175 za kitanzania kupitia hii kampuni. Nadhani ujumbe katika picha umeuona.
Unachotakiwa nikutoa laki5 kwa ajili ya kutengeneza pair ambayo ndio mzunguko wa pesa yako utakapokua unafanyika. Sisi tutakupa package ambayo ndani yake ina vidonge vya asili ambavyo vinauwezo wa kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemo vifonda vya tumbo nk.
Kwaiyo hiyo package utaamua ukauze au utumie kwa faida yako, huo utakua ni uamuzi wako maana hatuna mamlaka nayo hiyo package kwasababu ishakua mali yako.
Kwaiyo ukitoa hiyo laki 5 tunakufungulia account yako halafu tunakuwekea balance la shl. 70 kama kiasi cha kuanzia kisha tunakupa na hizo package za dawa
Utachotakiwa kufanya ni wewe uanze kutafuta watu uwashawishi wajiunge watoe hiyo laki 5 kamaili utengeneze pair uanze ku-make mkwanja.
Akanikaribisha kuuliza maswali
Mimi: hii kampuni yenu mmesema imelenga kuwasaidia watu sindiyo?
Yeye: Ndiyo hususani vijana maana ndio taifa la leo
Mimi: ok na dau la kujiunga ili kupata hiyo package ndio umedai laki tano in cash au kuna malipo ya nusunusu?
YEYE: ni cash hatupokei pesa nusu
MIMI: katika kipindi hiki cha corona shughuli zangu za utafutaji zimeathiriwa sana na hili janga, nina shauku ya kujiunga na kampuni lenu je mnanisaidiaje sina mshiko?
YEYE: kwa hapo ndugu hatuwezi kukusaidia, kwasababu hiki sio kikoba wala saccos
MIMI: swala la kusaidia si lipo katika ajenda zenu na ni moja ya policy zenu katika kuitangaza kampuni yenu?
YEYE: kama ujuavyo mashirika mbali mbali yamedhurumiwa na watu kwa kukopesa pesa, wako wapi tala saizi wanalia so hatuwezi kufanya hivyo
MIMI: yani unamiliki milion 175 halafu unaogopa kukopesa laki 5 kwa kuogopa kutapeliwa? Kama unavyodai kua mchongo huu haunaga hasara kwanini uweke possibilities za kudhurumiwa?
YEYE: Unajua katika makosa ambayo hatutakiwi kufanya katika kampuni hii ni kumuamini mtu, halafu inaendekeza uzembe kwasababu watu kama wewe watakua wanakuja kukopa kila siku
MIMI: kama kuaminiana ni swala ambalo haliwezekani Mbona wewe unanishawishi mimi nikuamini nitoe pesa yangu nikupe wewe ili nije kumiliki nyingi zaidi? Huoni kwa kauli yako unanipa wasi wsi juu ya ahafi yako ambayo umeitoa muda mfupi uliopita?
YEYE: hii ni campuni ipo duniani kote swala la wewe kudhurumiwa na sisi halipo, kizuri zaidi ni kwamba kampuni yetu ishakua registered kiserikali na malipo yetu tunayafanya kupitia bank ya NMB
MIMI: Sasa kama hiyo kampuni inatambulika kiserikali basi ndo unatakiwa ufate sheria ambazo unazitangaza huku, au hizi sheria za kusaidia hazitambuliki na serikali?
YEYE: zinatambulika na ndiyo tunakusaidia ila hatukukopeshi
MIMI: Sasa kama mtu anakuja na pesa yake hapo unakua umemsaidia nini?
YEYE: Mkuu si tunakupa package ya dawa tunakua tumekusaidia afya yako
MIMI: Anhaa kama msaada wenu ni dawa ina maana member wanaotakiwa ujiunga hapo wanatakiwa wawe wagonjwa? Na je wakija wagonjwa kujiunga hiyo package mnagawa bure kuwasaidia?
YEYE: mkuu mbona huelewi?
MIMI: Haya tufanye nimeelewa, vipi kulingana na hufuma zenu zimewalenga wagonjwa sasa kulingana na situatiin ya sasa je hizo package zenu za dawa je wagonjwa wa corona nao wanajumuishwa hapo kwenye hiyo tiba yenu au?
YEYE: typing....
Blocked
Mkuu nenda na wewe jiunge nao upige mipesa. Ndani ya miaka minne utupe mrejesho!Amejenga nyumba mkuu within this 3 yrs ! na huko Malaysia anaenda kwa pesa zake zinazotokana na juhudi zake za network marketing.Nawafahamu hao marafiki zangu miaka mitatu ya nyuma walikuwa ktk hatua gani kimaisha na sahizi wapo wapi, mmoja kati yao kapiga hela ndefu na mwaka jana kawekeza ktk kikimo chha mihogo eka 120 huko Tanga maeneo ya Mkata, kikubwa hapa naona physical progress siyo blabla ! na wanajitoa kwelikweli kufanya kazi across the whole country,upo hapo nyonyo
Sent using Jamii Forums mobile app