The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Mimi nimekutana na wengi hasa wanawake wako kwenye dating sites kutafta watu. Nilikutana na mmoja wa kwanza tukapeana namba kesho yake anataka kujua nafanya wapi kazi, nafanya kazi gani, nalipwajwe, kama mshahara mdogo nijiunge na yeye, nimamblock.Jamaa akaanza kunipa dondoo
Mi ni mshindi wa pili kwa ukanda huu wa afrika mashariki nimevuna milion 175 za kitanzania kupitia hii kampuni. Nadhani ujumbe katika picha umeuona.
Unachotakiwa nikutoa laki5 kwa ajili ya kutengeneza pair ambayo ndio mzunguko wa pesa yako utakapokua unafanyika. Sisi tutakupa package ambayo ndani yake ina vidonge vya asili ambavyo vinauwezo wa kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemo vifonda vya tumbo nk.
Kwaiyo hiyo package utaamua ukauze au utumie kwa faida yako, huo utakua ni uamuzi wako maana hatuna mamlaka nayo hiyo package kwasababu ishakua mali yako.
Kwaiyo ukitoa hiyo laki 5 tunakufungulia account yako halafu tunakuwekea balance la shl. 70 kama kiasi cha kuanzia kisha tunakupa na hizo package za dawa
Utachotakiwa kufanya ni wewe uanze kutafuta watu uwashawishi wajiunge watoe hiyo laki 5 kamaili utengeneze pair uanze ku-make mkwanja.
Akanikaribisha kuuliza maswali
Mimi: hii kampuni yenu mmesema imelenga kuwasaidia watu sindiyo?
Yeye: Ndiyo hususani vijana maana ndio taifa la leo
Mimi: ok na dau la kujiunga ili kupata hiyo package ndio umedai laki tano in cash au kuna malipo ya nusunusu?
YEYE: ni cash hatupokei pesa nusu
MIMI: katika kipindi hiki cha corona shughuli zangu za utafutaji zimeathiriwa sana na hili janga, nina shauku ya kujiunga na kampuni lenu je mnanisaidiaje sina mshiko?
YEYE: kwa hapo ndugu hatuwezi kukusaidia, kwasababu hiki sio kikoba wala saccos
MIMI: swala la kusaidia si lipo katika ajenda zenu na ni moja ya policy zenu katika kuitangaza kampuni yenu?
YEYE: kama ujuavyo mashirika mbali mbali yamedhurumiwa na watu kwa kukopesa pesa, wako wapi tala saizi wanalia so hatuwezi kufanya hivyo
MIMI: yani unamiliki milion 175 halafu unaogopa kukopesa laki 5 kwa kuogopa kutapeliwa? Kama unavyodai kua mchongo huu haunaga hasara kwanini uweke possibilities za kudhurumiwa?
YEYE: Unajua katika makosa ambayo hatutakiwi kufanya katika kampuni hii ni kumuamini mtu, halafu inaendekeza uzembe kwasababu watu kama wewe watakua wanakuja kukopa kila siku
MIMI: kama kuaminiana ni swala ambalo haliwezekani Mbona wewe unanishawishi mimi nikuamini nitoe pesa yangu nikupe wewe ili nije kumiliki nyingi zaidi? Huoni kwa kauli yako unanipa wasi wsi juu ya ahafi yako ambayo umeitoa muda mfupi uliopita?
YEYE: hii ni campuni ipo duniani kote swala la wewe kudhurumiwa na sisi halipo, kizuri zaidi ni kwamba kampuni yetu ishakua registered kiserikali na malipo yetu tunayafanya kupitia bank ya NMB
MIMI: Sasa kama hiyo kampuni inatambulika kiserikali basi ndo unatakiwa ufate sheria ambazo unazitangaza huku, au hizi sheria za kusaidia hazitambuliki na serikali?
YEYE: zinatambulika na ndiyo tunakusaidia ila hatukukopeshi
MIMI: Sasa kama mtu anakuja na pesa yake hapo unakua umemsaidia nini?
YEYE: Mkuu si tunakupa package ya dawa tunakua tumekusaidia afya yako
MIMI: Anhaa kama msaada wenu ni dawa ina maana member wanaotakiwa ujiunga hapo wanatakiwa wawe wagonjwa? Na je wakija wagonjwa kujiunga hiyo package mnagawa bure kuwasaidia?
YEYE: mkuu mbona huelewi?
MIMI: Haya tufanye nimeelewa, vipi kulingana na hufuma zenu zimewalenga wagonjwa sasa kulingana na situatiin ya sasa je hizo package zenu za dawa je wagonjwa wa corona nao wanajumuishwa hapo kwenye hiyo tiba yenu au?
YEYE: typing....
Blocked
Wa pili hivyo hivyo nashtukia niko kwenye group napewa semina mara naambiwa ni download zoom sijui ujinga gani.
Baada ya seminar nikaulizwa umeelewa nikasema ndio wakati hata sikujua walikua wanajadili nini, unajiunga lini nikasema hata kesho, utaweka account ngapi nikasema 7 maana yake 3.5m, yaani toka simu hiyo simu sio simu, kila saa napigiwa, tunaweza kukuona, tumupe account, tukufuate kila mara najibu niko busy ntawatafta. Hii wiki ya 2 sasa hawakati tamaa.
Natafta namna ya kuwasumbua. Siku niwaambie waje sa 5 usiku mabwepande kuchukua hela maana nasafiri usiku wa sa 9 wakiniambia wamefika nawaambia nimetoka mara moja niko mbagala kama mnaweza kuja kuchukua sawa.