Aina gani ya Madini inapatikana kwenye eneo unaloishi/Unalotoka au unalolifahamu!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Wadau,
Ni ukweli ulio wazi kwamba kwenye nchi yetu ya Tanzania karibu kila wilaya kuna madini ya aina fulani yenye thamani.

Wakuu ninaomba tubadilishane uzoefu katika eneo hili.

Ni aina gani ya madini yanayopatikana katika eneo unaloishi, ambalo ulishawahi kuishi, ulilotoka au unalolifahamu?.

Ni vyema kama unafahamu ukaongezea na nyama nyama kama vile kijiji, changamoto za kufika/kuishi kwenye eneo husika n.k.

Ni katika kubadilishana uzoefu tu na kujaribu kufunguana vichwa juu ya fursa zilizoko ndani ya nchi yetu ili atakaye weza azichangamkie.

Natanguliza shukrani.
 
Ruvuma, kitai, sapphire, blue-green/pink.
 
Morogoro, mvuha, rhodolite-gololi
 
Mkuu kitai ni kata au ni nini? hizo sapphire soko lake liko wapi! hasa!

sina ramani, nitakuelekeza kwa mwelekeo kadri nikumbukavyo.
Inawezekana kitai ni kata ila sina uhakika muda mrefu umepita, unatokea Songea mjini ukiwa unaelekea Mbinga, ukifika maeneo ya Gereza la Kitai unakata kulia, machimbo yapo kijiji kinaitwa Amani makolo mwisho wa kijiji kuna sehemu inaitwa Masugulu.

Wathai ndio wanunuzi wakubwa wa hii kitu baada ya kufahamu jinsi ya kuibadilisha kupandisha ubora wake.
 
Mkuu hizo rhodolite soko lake liko wapi hasa mkuu?Mvuha ni kijiji?

zinauzika vizuri popote ndani ya nchi kwa jiwe la gram na kuendelea, ni moja ya Rhodolite zenye magonjwa machache kabisa na ubora wa juu kuonekana kwetu.
Mvuha ipo njia ya kwenda Kisaki kutokea Morogoro mjini.
 
Niliona utafauti nikiwa msumbij japo wachmbji nwalewale toka tz ila pana afadhali kidogo kule kuna wadhamini

kaka, the truth is UNAANDIKA VIBAYA yani inabid utumie nguvu sana kukuelewa.

na kwani hauwezi kuandika maelezo yako kwenye paragraph moja??

After all, ahsante kwa elimu.
 
Kinachokuongoza kwamb madin yapo ni crystal.unapoanz kuchmb unakut crystal itakuongoz mpka unakuta madini.

Kijana mbona unadanganya unajua maana ya crystal?
Nikusaidie tu madini kuwepo kwenye mwamba hutegemea nq nature ya deposition inaweza ikawa ni vein, wall rock alteration etc
 
asante kw masahisho.sijazungumzia uwepo wa madin yanasababishw na crystal.HAPANA. embu rudia hapo ju kusoma MAELEZO ANGU
 
Kuna eneo moja singida lina dhahabu ya kutosha wachina wameibeba sana..
 
Morogoro, Matombo, Spinel
 
NJO ENDABASH KARATU KUNA WATU WAMESHNDW KUENDESHA MIGODI HAWANA PESA.UKIZAMINI UNAPIGA HELA CHAFU..Km vp ni pm.
 
Ruvuma, Mtwara pachani - kijiji, Aquamarine.
 
mi nauliza kama eneo lako lina madini, sheria inaruhusu kuyachimba mwenyewe au wakiinyaka tu taarifa unahamishwa eneo?
 
mi nauliza kama eneo lako lina madini, sheria inaruhusu kuyachimba mwenyewe au wakiinyaka tu taarifa unahamishwa eneo?
ukigundua eneo lako lina madini, haraka unatakiwa unakimbia ofisi ya madini ya kanda unaomba leseni ili usije kuondolewa na uchimbe kihalali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…